Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameahidi kuimaliza vita kati ya Ukraine na Urusi ndani ya saa 24 tu endapo akipewa tena Urais wa Marekani.
Trump ambaye tayari ameonesha nia ya kugombea tena Urais kwenye uchaguzi ujao wa mwakani 2024 ametoa kauli hiyo Florida, Marekani ambapo amesema ataimaliza vita hiyo akishatangazwa Mshindi tu hata kabla ya kuapishwa.
“Nikishinda tu sitosubiri hadi kuapishwa, nitampigia simu Rais wa Urusi, Putin na Rais wa Ukraine, Zelensky na kuwaambia tunapaswa kuonana, nawahakikishia nitamaliza vita hivi, nitamwambia Putin hivi na kumwambia Zelensky vile na tutakuwa na dili ya kumaliza vita ndani ya saa 24 tu”.
Trump amekosoa pia kitendo cha Rais Biden kuidhinisha pesa za kuisaidia Ukraine kwenye vita hivyo na kusema kufanya hivyo ni kama Marekani inachochea vita zaidi na kufanya Watu wengi waendelee kupoteza maisha “Namjua Putin hawezi kukubali kushindwa vita kwa kumtunishia msuli au kumuonesha ubabe, bali kwa njia bora za mazungumzo, Urusi imeshinda vita nyingi ina silaha na mbinu kibao za vita huwezi kuishinda kirahisi kwa kutumia mabavu”.