Trump: Nitaimaliza vita Ukraine ndani ya saa 24

Trump: Nitaimaliza vita Ukraine ndani ya saa 24


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameahidi kuimaliza vita kati ya Ukraine na Urusi ndani ya saa 24 tu endapo akipewa tena Urais wa Marekani.

Trump ambaye tayari ameonesha nia ya kugombea tena Urais kwenye uchaguzi ujao wa mwakani 2024 ametoa kauli hiyo Florida, Marekani ambapo amesema ataimaliza vita hiyo akishatangazwa Mshindi tu hata kabla ya kuapishwa.

“Nikishinda tu sitosubiri hadi kuapishwa, nitampigia simu Rais wa Urusi, Putin na Rais wa Ukraine, Zelensky na kuwaambia tunapaswa kuonana, nawahakikishia nitamaliza vita hivi, nitamwambia Putin hivi na kumwambia Zelensky vile na tutakuwa na dili ya kumaliza vita ndani ya saa 24 tu”.

Trump amekosoa pia kitendo cha Rais Biden kuidhinisha pesa za kuisaidia Ukraine kwenye vita hivyo na kusema kufanya hivyo ni kama Marekani inachochea vita zaidi na kufanya Watu wengi waendelee kupoteza maisha “Namjua Putin hawezi kukubali kushindwa vita kwa kumtunishia msuli au kumuonesha ubabe, bali kwa njia bora za mazungumzo, Urusi imeshinda vita nyingi ina silaha na mbinu kibao za vita huwezi kuishinda kirahisi kwa kutumia mabavu”.

Trump is a real deal now in US

Biden anaenda kuanguka vibaya sana 2024 election..

Lazy Joe kaumiza dunia nzima, gharama za maisha zimepanda sana, in short, Biden mshenzi na nyoko sana asshole kabisa 😡😡
 
Nani asiyejua kwamba trump dish [emoji341][emoji341][emoji341][emoji341][emoji341][emoji341][emoji341][emoji341][emoji341] lake Huwa Linayumba mara kwa mara??
 
Huyu mzee hapa anatudanganya. Huu ni uongo mwepesi sana.

Kwamba vita iishe ndani ya saa 24? Give me a break?!

Fact ni kwamba, vita ilianza mwaka 2014. Trump akaingia madarakani mwaka 2017. Ameondoka madarakani mwaka 2021, kaacha vita inaendelea.

Hi sera anayotembea nayo Mzee Trump ni sera ambayo iko kinyume kabisa na maslahi ya Marekani. Hata viongozi kadhaa na wazee wenzake ndani ya chama cha Republican hawakubaliani naye. Baadhi wameshatoka hadharani kumpinga.
 
Back
Top Bottom