adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 17,595
- 39,893
Kwa muda mrefu Papa mkuu wa kabisa katoliki duniani "Pope Leo" ambaye ni Mmarekani amekuwa mstari mbele kukemea mauaji na vita mbalimbali zinaondelea duniani mfano Gaza alikemea Hamas, mauaji yanayofanya na serikali ya Israel kwa watoto na raia, kupiga mabomu mpaka Kanisani Gaza nk
Na kwenye mgogo huu wa Vita kati ya Iran na USA & Israel amekuwa mstari wa mbele kutaka vita visitishwe na mauji wa raia, kuzuia mlango wa bahari na kuharibu miundombinu ya kiraia kusitisha.
1. Kumwambia Pope ni "mbaya kwenye mambo ya sera za nje na yeye (Trump ) haushabikii
“Hatupendi papa ambaye atasema kwamba ni sawa kuwa na silaha ya nyuklia… Yeye ni mtu ambaye hafikirii kwamba tunapaswa kushughulika kwa uzito na nchi inayotaka silaha ya nyuklia ili iweze kulipua dunia,” Trump aliwaambia waandishi wa habari, akiongeza, “Mimi si shabiki wa Papa Leo.”
2. Hamtaki Papa anayeikosoa USA na kudai Papa amewekwa hapo Kwa sababu yeye ni Raia wa Marekani
“Na sitaki Papa ambaye anamkosoa Rais wa United States,” aliongeza.
" Leo hakuwa kwenye orodha yoyote ya kuwa Papa, na aliwekwa hapo na Kanisa kwa sababu alikuwa Mmarekani, na walidhani hiyo ndiyo njia bora ya kushughulika na Rais Donald J. Trump.”

===
Rais wa Marekani, Donald Trump, amemkosoa na kumshambulia kwa maneno makali Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV akisema ni Papa dhaifu kwenye kushughulikia masuala ya uhalifu na ambaye hayupo vizuri kwenye kushughulikia Sera za Kigeni huku akisema anamshangaa kuona Papa Leo anaona ni sawa Iran kuwa na silaha za Nyuklia na amekiri kuwa yeye Trump sio Shabiki wa Papa Leo na haoni kama anafanya kazi nzuri.
Trump ametoa maneno hayo makali kupitia mtandao wa Truth Social ambapo ameandika “Papa Leo ni dhaifu katika suala la kukemea uhalifu na ni mbaya sana katika kushughulikia Sera za Kigeni, anaongelea hofu ya Utawala wa Trump lakini hataji hata kidogo hofu ambayo Kanisa Katoliki na Mashirika mengine yote ya Kikristo yalipata wakati wa COVID wakati walipokuwa wakikamatwa Mapadri, Wahudumu na wengine wote kwa kufanya Ibada za Kanisa hata walipokuwa nje na walipokaa umbali wa futi kumi na hata ishirini.
“Mimi nampenda sana Kaka yake Louis zaidi kuliko yeye kwasababu Louis ni Shabiki wa MAGA (Make America Great Again) kabisa, yeye anaelewa na Leo haelewi, simtaki Papa ambaye anadhani ni sawa kwa Iran kuwa na silaha za Nyuklia, simtaki Papa ambaye anadhani ilikuwa vibaya Marekani kuishambulia Venezuela Nchi ambayo ilikuwa ikisafirisha na kuingiza dawa za kulevya kwa wingi mkubwa Nchini Marekani na mbaya zaidi ikiwatoa wafungwa wake wengi, wakiwemo wauaji, wauza dawa za kulevya, wauaji na kuwaingiza katika Nchi yetu, hatutaki Papa anayesema ni sawa kuwa na uhalifu duniani na hatutaki Papa anayeona ni sawa kuwa na silaha za Nyuklia” Ameandika Trump.
Pamoja na hayo, Papa Leo amekuwa akikosoa vita inayoendelea kati ya Marekani & Israel na Iran mara kadhaa na ameukosoa utawala wa Trump kwenye hatua za kushughulikia vita hiyo.