Rais wa Marekani, Donald Trump, amemkosoa na kumshambulia kwa maneno makali Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV akisema ni Papa dhaifu kwenye kushughulikia masuala ya uhalifu na ambaye hayupo vizuri kwenye kushughulikia Sera za Kigeni huku akisema anamshangaa kuona Papa Leo anaona ni sawa Iran kuwa na silaha za Nyuklia na amekiri kuwa yeye Trump sio Shabiki wa Papa Leo na haoni kama anafanya kazi nzuri.
Trump ametoa maneno hayo makali kupitia mtandao wa Truth Social ambapo ameandika “Papa Leo ni dhaifu katika suala la kukemea uhalifu na ni mbaya sana katika kushughulikia Sera za Kigeni, anaongelea hofu ya Utawala wa Trump lakini hataji hata kidogo hofu ambayo Kanisa Katoliki na Mashirika mengine yote ya Kikristo yalipata wakati wa COVID wakati walipokuwa wakikamatwa Mapadri, Wahudumu na wengine wote kwa kufanya Ibada za Kanisa hata walipokuwa nje na walipokaa umbali wa futi kumi na hata ishirini.
“Mimi nampenda sana Kaka yake Louis zaidi kuliko yeye kwasababu Louis ni Shabiki wa MAGA (Make America Great Again) kabisa, yeye anaelewa na Leo haelewi, simtaki Papa ambaye anadhani ni sawa kwa Iran kuwa na silaha za Nyuklia, simtaki Papa ambaye anadhani ilikuwa vibaya Marekani kuishambulia Venezuela Nchi ambayo ilikuwa ikisafirisha na kuingiza dawa za kulevya kwa wingi mkubwa Nchini Marekani na mbaya zaidi ikiwatoa wafungwa wake wengi, wakiwemo wauaji, wauza dawa za kulevya, wauaji na kuwaingiza katika Nchi yetu, hatutaki Papa anayesema ni sawa kuwa na uhalifu duniani na hatutaki Papa anayeona ni sawa kuwa na silaha za Nyuklia” Ameandika Trump.
Pamoja na hayo, Papa Leo amekuwa akikosoa vita inayoendelea kati ya Marekani & Israel na Iran mara kadhaa na ameukosoa utawala wa Trump kwenye hatua za kushughulikia vita hiyo.
Kila siku lazima aje na kibweka hana jambo dogo matamshi yake kama muhuni wa mtaani jambo la kupuuzia anafanya anafanya kuwa topic kubwa.Pamoja na kukosa akili, hekima, na busara, Trump pia hana impulse control.
Familia yake inabidi iingilie kati lakini sidhani kama wana ujasiri huo.
Hizi propaganda za kusema Iran anataka nuclear ili alipue Dunia zimesha pitwa na wakati,US ndio taifa pekee lililotumia silaha ya nyuklia kuangamiza watu huko Ngasaki na Hiroshima Japan,eti leo hii US ndio hataki wengine wawe na hiyo silaha na kuwapangia wengine wasiwe na hiyo silaha coz yeye ndio taifa pekee lililotumia hiyo silaha so far,The whole world knows the truth now,LEO TRUMP KAMVUNJIA UKIMYA KWENYE TRUTH POST YAKE.
1. Kumwambia Pope ni "mbaya kwenye mambo ya sera za nje na yeye (Trump ) haushabikii
“Hatupendi papa ambaye atasema kwamba ni sawa kuwa na silaha ya nyuklia… Yeye ni mtu ambaye hafikirii kwamba tunapaswa kushughulika kwa uzito na nchi inayotaka silaha ya nyuklia ili iweze kulipua dunia” Trump aliwaambia waandishi wa habari, akiongeza, “Mimi si shabiki wa Papa Leo.”
Kumbe Papa Leo aliwekwa hapo coz ya Uraia wake tu!2. Hamtaki Papa anayeimosoa USA na kudai Papa amewekwa hapo Kwa sababu yeye ni Raia wa Marekani
“Na sitaki Papa ambaye anamkosoa Rais wa United States,” aliongeza.
" Leo hakuwa kwenye orodha yeyote ya kuwa Papa na aliwekwa hapo na Kanisa kwa sababu alikua ni Mmarekani.
#Uzi tayari
The truth is Israelis rejected Jesus.Nitarudi baadae kwa updates In Shaa Allaah .
Kuna baadhi ya vijana kikiristo wao Netanyahu na Marekani wamemuweka mbele kushinda hata Bible na Yesu kwa maana hata wafanye kinyume na ukiristo wauwe walipue kabisa it's Ok Kwa sababu ni Taifa teule na Netanyahu
Wengine waneenda mbali kabisa wanamuona Netanyahu kama Mungu , hata Yesu aje leo akisema Mimi sikubaliani na Netanyahu basi wao watamkataa Yesu.
Hao WaIsraeli wa Nzega , Kibaigwa , Kybakari , mwanarumango na Katavi
Trumpa anaongoza nchi haongozi familia yake,madhara ya uongozi wake kama yapo yanaiathiri nchi zaidi na sio familia yake,sasa kwanini unasema familia yake ndio iingilie kati? hii ni issue ya kitaifa sio issue ya kifamilia.Pamoja na kukosa akili, hekima, na busara, Trump pia hana impulse control.
Familia yake inabidi iingilie kati lakini sidhani kama wana ujasiri huo.
Trump ni kiongozi wa hovyo kuliko wote waliowahi kutokea dunianiMoja kwa moja .
Kwa muda mrefu Papa mkuu wa kabisa katoliki duniani "Pope Leo" ambaye ni Mmarekani amekuwa mstari mbele kukemea mauaji na vita mbalimbali zinaondelea duniani mfano Gaza alikemea Hamas , mauaji yanayofanya na serikali ya Israel kwa watoto na raia , kupiga mabomu mpaka Kanisani Gaza nk .
Na kwenye mgogo huu wa Vita kati ya Iran na USA & Israel amekuwa mstari wa mbele kutaka vita visitishwe na mauji wa raia , kuzuia mlango wa bahari na kuharibu miundombinu ya kiraia kusitishaView attachment 3571750
LEO TRUMP KAMVUNJIA UKIMYA KWENYE TRUTH POST YAKE.
1. Kumwambia Pope ni "mbaya kwenye mambo ya sera za nje na yeye (Trump ) haushabikii
“Hatupendi papa ambaye atasema kwamba ni sawa kuwa na silaha ya nyuklia… Yeye ni mtu ambaye hafikirii kwamba tunapaswa kushughulika kwa uzito na nchi inayotaka silaha ya nyuklia ili iweze kulipua dunia,” Trump aliwaambia waandishi wa habari, akiongeza, “Mimi si shabiki wa Papa Leo.”
2. Hamtaki Papa anayeimosoa USA na kudai Papa amewekwa hapo Kwa sababu yeye ni Raia wa Marekani
“Na sitaki Papa ambaye anamkosoa Rais wa United States,” aliongeza.
" Leo hakuwa kwenye orodha yoyote ya kuwa Papa, na aliwekwa hapo na Kanisa kwa sababu alikuwa Mmarekani, na walidhani hiyo ndiyo njia bora ya kushughulika na Rais Donald J. Trump.”
#Uzi tayari
Wewe Pimbi jadili kilichopo mezani,bila kuingiza uislamu kwenye kila mada hua muwasho wako hautulii sio?kwangu yote ni sehemu ya demokrasia Papa ameongea kama mkuu wa kanisa Katoliki na lbda citizen wa USA na aana haki hiyo, hakuna alitangaziwa fatwa na kuuuwa au kuchomwa kisu kwa kutoa maoni yake, yote heri tu ni demokrasia.
salman rushdie alichomwa kisu huko new york na islamic republic affiliated jihadists kwa kutoa maoni yake tu, ayatola khomeini alimtangaia fatwa mjapaani na mwishowe mjapani wa watu kuuwa ...
View attachment 3571756