Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Mleta mada ameleta mada kwa usahihi kabisa kiupeo lakini wachangia wa mada walio wengi hapa JF katika hili mpaka sasa wameonyesha upeo duni mnoo.
Ngoja nichangie kitu.
1. Upepo wa kura za maoni uliokuwa unampa Trump nafasi ya kushinda hapo awali wakati akichuana na Biden umeendelea kubadilika kwa kasi tangu Kamala ateuliwe, na kwa sasa upepo huo unampa Kamala nafasi nzuri ya kushinda. Hii ina maanisha nini? Trump ana wakati mgumu zaidi na huenda akaangushwa ikiwa hali hii itaendelea hivi hivi na ikiwa kura hizo za maoni zinaakisi maoni halisi.
2. Mleta mada ameleta kura za maoni kutoka taasisi kadhaa tofauti tofauti za USA ambazo huendesha zoezi la kura za maoni kwa weredi mkubwa. Ni taasisi hizo hizo pia hapo awali zilionyesha Trump akiongoza dhidi ya Biden, na ziliendelea kuonyesha Trump akiongoza dhidi ya Kamala pale mwanzoni japokuwa kwa tofauti ndogo. Kwa sasa zinaonyesha Kamala Harris anaongeza. Hii inamaanisha nini? Kwa sehemu kubwa kura hizo za maoni huenda zimebeba uhalisia kuliko agenda ya kumpigia kampeni mgombea fulani.
3. Kura hizo za maoni hulenga mfumo mzima wa kumpata Rais wa USA na huchukua maoni kiujumla na kimajimbo. Kura hizo za maoni hutumiwa na vyama na wagombea wa pande zote katika kujitathimini na kujipanga zaidi. Kupitia kura hizo za maoni chama cha Democrat na Biden mwenyewe waliamua kufanya maamuzi magumu ya kubadili mgombea wake na kumpitisha Kamala Harris dakika za mwishoni.