Try Again: Tunaenda kupata ushindi Misri.

Hivi wale wachezaji wanaofunga magoli katika zile nafasi walizopata washambuliaji wa Simba hutumia mbinu gani? Wana bahatisha au kuna siri gani?
 
Kama nyie mna matumaini ya kumfunga Mamelodi kwao , iweje simba muone hawezi kumfunga Ahly kwao?.
Huu ni mpira lolote laweza kutokea msikariri.
 
Ila Simba safari hii wamepatikana kwa huyu Try Again ongezea na Mangungu. Wakati Hersi anaingia rasmi kwenye mpira miaka michache iliyopita wajanja wakawa wanampa za uso kwenye usajili. Baada ya miaka miwili/mitatu sasa Hersi walau yupo vizuri kiasi kajifunza kitu kwenye usajili japo mara moja moja huwa bado anaingia mkenge lakini sio mbaya sana. Sasa huyo Try Again mpaka dirisha dogo juzi kati watu wamemwingiza chaka kauza SMG (Baleke na Phiri) kaleta Magobole mawili (Fredy na Jobe) na huku ana gobole lingine - Saidoo kalihifadhi stoo. Mbaya zaidi mjumbe mwenzake wa bodi Kadu kamsanua kuwa "hoya brother Try Again hao mapro ulioleta ungeweza pata wamatumbi wenye uwezo kama huo hapo Tandika tu".

Halafu bila aibu Try Again anawakejeli mashabiki na wapenzi wa Simba kuwa timu inaenda kupata ushindi Misri. Huo ushindi unaenda patikana kwa fowadi ipi? Huyu Try Again aambiwe ukweli kuwa Simba imeacha tiketi yake nusu fainali hapo kwa Mkapa. Huko Msiri ni kwenda tu kukamilisha ratiba. Simba walipata nafasi za wazi sita wakashindwa kuzitumia wakati wenzao mbili tu tena "half chance" wakatumia moja. Kwa kifupi Simba walipaswa kuimaliza mechi kwa Mkapa kwa ushindi wa goli tatu na kuemdelea hayo mengine ya Try Again ni blah blah tu na dharau za Wazi kwa mashabiki, wapenzi na wanachama wa Simba pamoja na wapenda soka wote wa Tanzania..
 
Yuko sahihi

Kiswahili Cha jina lake try again ni kipi

Asilaumiwe kwa kauli yake
 
Japo mi sio shabik wa simba, ila amenikera hapo anapozungumzia "bahati". Hii kiukwel ni kuonana watoto
Mtu mwenyewe anaitwa Try Again asiaminiwe na mwanasimba yeyote atatuingiza chaka kama jina lake
 
Rage alishamaliza kila kitu.
 
Hawa viongozi wa Simba sijui wanatuchukuliaje
 
Japo mi sio shabik wa simba, ila amenikera hapo anapozungumzia "bahati". Hii kiukwel ni kuonana watoto
Jamaa ni mwehu itakuwa,anaongeaje upuuzi hadharani !! Anazungumzia bahati kwenye soka kitu ambacho hakipo kabisa
 
Labda kama atacheza yeye ndiyo ushindi utapatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…