Try Again: Tunaenda kupata ushindi Misri.

Try Again: Tunaenda kupata ushindi Misri.

Hivi wale wachezaji wanaofunga magoli katika zile nafasi walizopata washambuliaji wa Simba hutumia mbinu gani? Wana bahatisha au kuna siri gani?
 
Mashabiki wa simba ifikie wakati mkatae hii tabia ya viongozi wenu kuwaona nyinyi kama mbumbumbu vile.

Yaani kirahisi tu simba ikapate ushindi Misri!! Kweli? Bora hata angesema timu itaenda kupambana ili isifungwe goli nyingi (yaani Khamsa) na Waarabu.
Kama nyie mna matumaini ya kumfunga Mamelodi kwao , iweje simba muone hawezi kumfunga Ahly kwao?.
Huu ni mpira lolote laweza kutokea msikariri.
 
Ila Simba safari hii wamepatikana kwa huyu Try Again ongezea na Mangungu. Wakati Hersi anaingia rasmi kwenye mpira miaka michache iliyopita wajanja wakawa wanampa za uso kwenye usajili. Baada ya miaka miwili/mitatu sasa Hersi walau yupo vizuri kiasi kajifunza kitu kwenye usajili japo mara moja moja huwa bado anaingia mkenge lakini sio mbaya sana. Sasa huyo Try Again mpaka dirisha dogo juzi kati watu wamemwingiza chaka kauza SMG (Baleke na Phiri) kaleta Magobole mawili (Fredy na Jobe) na huku ana gobole lingine - Saidoo kalihifadhi stoo. Mbaya zaidi mjumbe mwenzake wa bodi Kadu kamsanua kuwa "hoya brother Try Again hao mapro ulioleta ungeweza pata wamatumbi wenye uwezo kama huo hapo Tandika tu".

Halafu bila aibu Try Again anawakejeli mashabiki na wapenzi wa Simba kuwa timu inaenda kupata ushindi Misri. Huo ushindi unaenda patikana kwa fowadi ipi? Huyu Try Again aambiwe ukweli kuwa Simba imeacha tiketi yake nusu fainali hapo kwa Mkapa. Huko Msiri ni kwenda tu kukamilisha ratiba. Simba walipata nafasi za wazi sita wakashindwa kuzitumia wakati wenzao mbili tu tena "half chance" wakatumia moja. Kwa kifupi Simba walipaswa kuimaliza mechi kwa Mkapa kwa ushindi wa goli tatu na kuemdelea hayo mengine ya Try Again ni blah blah tu na dharau za Wazi kwa mashabiki, wapenzi na wanachama wa Simba pamoja na wapenda soka wote wa Tanzania..
 
Yuko sahihi

Kiswahili Cha jina lake try again ni kipi

Asilaumiwe kwa kauli yake
 
Japo mi sio shabik wa simba, ila amenikera hapo anapozungumzia "bahati". Hii kiukwel ni kuonana watoto
Mtu mwenyewe anaitwa Try Again asiaminiwe na mwanasimba yeyote atatuingiza chaka kama jina lake
 
Mashabiki wa simba ifikie wakati mkatae hii tabia ya viongozi wenu kuwaona nyinyi kama mbumbumbu vile.

Yaani kirahisi tu simba ikapate ushindi Misri!! Kweli? Bora hata angesema timu itaenda kupambana ili isifungwe goli nyingi (yaani Khamsa) na Waarabu.
Rage alishamaliza kila kitu.
 
Hawa viongozi wa Simba sijui wanatuchukuliaje
 
Japo mi sio shabik wa simba, ila amenikera hapo anapozungumzia "bahati". Hii kiukwel ni kuonana watoto
Jamaa ni mwehu itakuwa,anaongeaje upuuzi hadharani !! Anazungumzia bahati kwenye soka kitu ambacho hakipo kabisa
 
"Bahati haiwezi kuwa kwao kila siku, leo imekuwa bahati kwao, kesho inaweza kuwa kwetu, cha msingi kuwa na morali, umoja, upendo na kujiandaa, hatuwezi kwenda kushinda ugenini kama tutakata tamaa. — Mwenyekiti wa Bodi Simba, Salim Abdallah 'Try Again'

"Mimi naamini kwa timu tuliyonayo, kwa nyinyi mlivyo mimi naamini kabisa tunaenda kupata ushindi, tusikate tamaa hata kidogo morali yetu iwe juu kabisa kupita hii tuliyokuwa nayo mimi naamini mnaweza kufanya hivyo na tukapata ushindi ugenini." — Try Again
Labda kama atacheza yeye ndiyo ushindi utapatikana.
 
Back
Top Bottom