Tsh. Bilioni 6.7 zatengwa kufadhili Wanafunzi 640 kwa 100%, ambaye hatafikisha GPA 3.8 ufadhili unasitishwa

Kila siku kununua vitu kipya badala kuendeleza vilivyopo kwa nia kutafuta sifa binafsi ya mtu. Kuona shule za kata zinazosaidia watu wengi zaidi hazina waalimu wala vifaa vya kufundishia. Shule hazina chakula. Mnataka misaada ya kibaguzi. Kuwabagua watoto kwa misingi ya akili ni dhambi. Watoto watakaopata misaada ni wale baba zao wana uwezo wamesoma shule binafsi za bei ghari. Hizo ndizo zenye waalimu bora zaidi kwa kuwa walipwa vizuri, wana vifaa na maabara nzuri. Shule za kayumba hazina hata burns burner hawezi kulipia tuition topic moja atafaulu wapi?
Pili wengi wataishia njiani kwa sababu mazingira waliosoma sekondari ni tofauti na vyuoni kwetu. Wengi wanashinda wakifika vyuoni. Huu ni usanii mtupu. Hawa Maraisi wetu wetu waliofeli sana shule ndiyo wanawawekea masharti magumu wanafunzi kama kuwakomoa. Uzoefu unaonesha wengi wao waliosoma shule za binafsi wakifika vyuo wanashuka hivyo hawatapata GPA ya 3.8 na siyo rais kupata GPA hiyo kwa masomo ya science
 
Huna akili. Hivi unajua kuna wanafunzi wengi wana uwezo darasani lakini wanashindwa kuendelea na masomo yao kwasababu ya umasikini wao?
Ni busara wangeanzia chini sekondari kuliko na watu zaidi hao waliofaulu form six si masikini ni matajiri. Nani atafaulu masomo bila tuition tena kwa mada moja moja
 
Umeongea point. Ubaguzi siyo issue
 
Hizi hela watafute best brains wawapeleke kwenye world class universities tuwe na wasomi wa kidunia.
Hapo tutaweza hata kulinda na kutumia vema rasilimali zetu.

Tukubali madhaifu yetu tujipangie mikakati ya kujikomboa yuweze kushondana kwa kujiamini. Majirani zetu Rwanda na Kenya, hata Uganda wamejitawanya duniani huko kusaka fursa nasi tuamke.

Tupeleke vijana huko nje wakaibe teknolojia watuletee huku. Haijalishi watabaki huko au watarudi nyumbani, yote mawili ni neema kwa nchi.


Waziri Mkenda tafadhali dimamia hili!!
 
Badala mtoe ufadhili watu waende Marekani na Ulaya ili tupate watu wa kuleta ushindani Duniani huko mnatoa ufadhili wasome vyuo vyetu hivi hohe hahe.

Alafu kesho mnasema tunawasomi wa hovyo.
MABEBERU HATUTAKI, watoe ufadhili twende kwa marafiki zetu wapya, Iran, Syria, Afghanistan na Russia.
 

Tanzania ndio nchi pekee ambayo ukifuatilia, ukichambua, ukidadavua baadhi ya maamuzi yake tena ya kitaifa na kwenye sector kubwa na nyeti unaweza kutoa machozi. Hivi malengo na madhumuni ya Board loarn yalikuwa ni nini? na malengo na madhumuni ya hii Mama Samia Loarn ni nini? Ebu nipeni utofauti. Sioni tofauti zaidi ya kuchukua selection criteria iliyokuwa ikimzuia mtoto aliyetoka familia tajili kutopata mkopo 100% from Laon boards na kumtengenezea njia mbadala ya kupata mkopo 100% tena kwa uhakika kuliko wale wengine.

Wote tunajua more than 85% ya wanaofaulu vizuri wanatoka shule bora, shule za kishua, shule za wazazi wanaojiweza, nyingi kama si asilimia 95% basi na zaidi ni shule za private. Sasa hawa walikuwa hawa meet preliquesite qualification za Nationa Loan Boards, tumewatengenezea njia mbadala wa kufadhiliwa nje ya Loan board , tena bila usumbufu wa wenzao. Hiyo ndio Tanzania.

Hivi lengo sasa ni inclusion or exclusion, na fairness? na equality iko wapi kwa walio watanzania wengi ambao watoto wao wengi wana division II na kuendelea. Kwanza unajua karo ya private nyingi kwa mwaka ni zaidi ya fees na matumizi ya vyuo vikuu vingi kwa mwaka?, kwa hiyo huyu mzazi hasingeshindwa kumlipia mtoto wake. Ebu nambie mzazi wa kajamba nani Nyamtumbo, Tanganyika Katavi, Karagwe Kagera ambaye ameuza sehemu ya kiwanja kumsomesha mtoto wake mpaka form six, tunataka auze nini kilichobakia. Kweli nimekubali kazi na iendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…