Kwenye peak seasoan (high demand) kama mida ya siku kuu hizi - Mbuzi ama Kondoo anakwenda hadi 100,000 shs au zaidi, sehemu ya kufugia - nimeshauri utumie shs.500,000 kununua/ pata eneo lako ili uwafunge/uwafuge hapo, na shs.1,000,000 ujenge banda simple kwa ajili ya mbuzi kulala na mfanyakazi wa kusimamia, ndio unaweza kuanza kununua mbuzi na kuwaleta dar - ila utakuwa na changamoto ya ongezeko ya gharama za uendeshaji (variable costs)Mf.kusafiri hadi shy, sgda, mza ama tabora kuzunguka kwenye minada kwa ajili ya kutafuta mbuzi wa kutosha "mind you" unatakiwa kukodi gari la kuwafikisha dar "sokoni", kukodi watu wa kuwachunga mpaka mzigo utimie kabla ya kupata usafiri, mie naona ni bora kuwa na rachi yako ya mbuzi na wanunuzi wafike wenyewe kwenye banda/ranchi yako na kuchukua wenyewe kwa ghrama zao badala ya wewe kuhangaika na ukusanyaji, jambo lingine kwa kuwa na rachi yako mwenyewe ni fursa nzuri kwako ku- diversify biashara yako hiyo - hata kwa kupata mkopo wa benk kwa ajili ya expansion - maana utakuwa na aridhi na mifugo inaonekana kwa hio inakuwa rahisi kwako kujenga hoja kwa afisa mikopo yeyote na ukapata mkopo kuliko hilo wazo la kimachinga la kufuata mbuzi huko mikoani na kuileta dar