- Thread starter
- #21
Thanks,najaribu kuelewa. Kiufupi ni kwamba niliagiza press heat machine,nikaletewa pamoja na Epson printer na hizo transfer paper ambazo Ni light pamoja na dark,kwa bahati mbaya sijaanza kutumia kutokana na ratiba yangu ilivyokaa japo kulingana na tutorials mbalimbali nilizopitia nimeona kama kuna papers zaidi ya hizi natakiwa kutumia hasa kama nataka kuprint vitu kama mugs/plate. Pia nimeona Kuna sylicon paper inatumika japo haikuwa included kwenye hizi karatasi walizoleta,je,naweza kuipata separately na inauzwaje/wapi? Na hata nikitaka kuprint mfano namba/jina kwenye jezi natakiwa kufanyaje?
sylicone paper ni non stick paper kusaidia wino usibaki kwenye heat press ama tshirt isiungue na joto la heat press, ni karatasi isiyoungua..
karatasi zinazofanya kazi kama hizi zinauzwa super market kwa jina la baking paper.. karatasi za kuokea mikate, so hata ukinunue baking paper itafanya kazi..
ama unaweza agiza aliexpress special ya heat press haifiki hata elfu 30 mpaka ikufikie mkononi kila kitu.
kuhusu namba na majina ni unanunue herufi na namba za vinly kwa bei ya jumla.. kisha unakuwa unaprint tu.. zile namba huwezi kuzitengeneza wewe mwenyewe.. unless uwe na mtaji mkubwa sana ununue vinly plotter machine.. ila watu wote wanaoprint Tanzania namba na herufi uwa wanazinunua separate kwa bei ya jumla