TSN yawasimamisha kazi waliofanya uzembe wa kuandika Rais Samia amefariki

Nasikia kwa sheria yetu hiko tu kukiandika ni kumtakia mabaya Rais na kosa lake lina adhabu sawa na uhaini. Mwigulu Nchemba PHD of Cross Multiplication atafafanua zaidi.
PhD
 
Mbona kama waliosimamishwa sio waliohusika!!!

Hawana mhariri hawa??
 
Wamefanya vizuri acha nafasi zao wapewe wengine wafanye kazi kwa weledi. Kuna watu wapo mitaani wana hangaika na ajira huku wengine wakifanya kazi kwa maringo na mazoea. Natumai kuna watu wawili wapya wameajiriwa leo TSN.
 
Jana kulisambaa Tangazo lilitolewa Kwenye Gazeti la Serikali la Daily news Likiwa na Makosa Mengi ya kuandishi, Baada ya Lile Tangazo kusambaa Kwenye social media, DG Wa TSN akachukua Hatua ya Kuwasimamisha Wafanyakazi Wawili Wa TSN+ Wakala wa kujitegemea.

Je tUnadhani Ni Sahihi Kwa Mkurugenzi Wa TSN Kuwasimamisha Wale Watu Wawili KwaYale Makosa Ya Tangazo La Stamico?

Maana Yangu Ni Kwamba, Msimamizi wa huduma kwa wateja, yeye akishapokea Tangazo analiandikisha , hatengeneza yeye, linakwenda kwa graphic designer.

Halafu Mhariri ndio anapaswa kulipitia, Hata Huyu wakala wa kujitegemea naye Anakosa gani mpka Na Yeye Ale Ban?

Nadhani Hatua alizochukua DG kwa wale Watu Wa Marketing ni hafifu sana.

Kosa Lipo kwa wahariri na production unit, Yeye DG kawajibisha watu wa marketing.

Kwanza Hata Barua Yao Aina tarehe, haina address Wala Ref. No.... Opine please
 
Kuna baadhi ya mambo utendekaji wake na hii akili yangu ya darasa la saba B hua inagoma kukubali kama ni hali ya kawaida au la labda ni michezo ya kutusahaulisha baadhi ya mambo ya msingi 🤔 🤔
 
Kilichotokea ni uzembe lakini pia ni human error. Hii inaweza pia kuwa imechangiwa na uchovu wa kazi nyingi pamoja na mtiririko wa matukio makubwa mawili yaliyotokea kwa wakati mmoja. Yani akili inaweza kuwa occupied na tukio moja wakati una deal na tukio jingine hivyo kuzalisha makosa ya kiufundi. Kilichotokea ni occupational harzad. Napenda kuwaombea radhi wahusika wa uzembe huu kutoka kwa wote walioathirika na tukio hili pamoja na mwajiri.
Warning letter inawatosha.
 
Nimeshawahi kupeleka matangazo pale Daily News.

Yule desk officer anayepokea hulipitia lile tangazo na kukushauri pale inapobidi ikiwemo matumizi ya lugha stahiki kwa sababu tangazo linakuw kwa matumizi ya umma.

Kama ni kweli wamesimamishwa hao watu unaowaita wa Marketing basi hatua hiyo ni sahihi kabisa tena walipaswa kuchapwa na viboko!
 
Kwa hiyo hao watu wa mwanzo wakikosea basi hata baada ya kuchapwa pia habari isihaririwe
 
Maamuzi yanaonyesha kabisa boss itaka kujisafisha mapema
 
Inasemekana tangazo lilienda vizuri sema grafix designer alikopi na kupate tangzo lingine la kifo.mhariri nae hakuona.wameonewa
 
dhana ya uwajibikaji katika kusimamia maslai ya umma
 
TSN nao wamekurupuka ,Kukosea kupo...Hayo ni makosa ya kibinadamu.
Hapa nawaza kumbe hukumu kwa makosa kwa watumishi wa umma inatofautiana katika ofisi!! Hakuna onyo wala karipio kali kwanza kabla ya kusimamishwa/kufukuzwa?
 
Shida ya kujifanya wainglishi mamaee wanatuulia Rais kipenzi mama yetu kwa maneno, conspiracy theories, wahojiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…