Tsunami kamwe haitokuja kutokea Tanzania kwa sababu zifuatazo (Jifunze usiogope)

Tuwe makini na wapotoshaji kama mtoa mada. Ni watu wenye maneno mengi lakini ni upotoshaji mtupu.
Wewe usiponielewa inatosha! wenye akili wamenielewa ...na nimekwambia jaribu hata mwenyewe hapo weka maji kwenye beseni zalisha wimbi utanielewa
 
Bomu kulipuka sio lazima iwe ni vita, linaweza kulipuka kwa bahati mbaya ikiwa nyambizi iliyosheheni mabomu hayo ikiwa ndani ya ukanda wetu wa bahari ya hindi.
Tsunami yenyewe ilikuwa Nini Mwaka ulee ambako walimwengu waliokuwa Holiday Nchi Gani Ile sijui waliathirika Kwa Maelfu na ambayo Hata Mawimbi yake yalifika Mpaka huku Bongo yetu lakini yakiwa yamepungua Nguvu ndio ikawa Salama yetu ?

SI tulielezwa na Wataalamu kwamba kulitokea Tetemeko la Nchi baharini lililozua Mawimbi makubwa yalisababisha Maafa tuliyoyaita Tsunami ?
Kwa Tanzania SI Nchi TU Iko Duniani humu ?
Kwani Iko Sayari nyingine ?
Kama ilitokea Kwa Wenzetu na Kishindo chake tukakiona Hadi huku, Kwa Nini Tanzania isitokee hivyo Siku Moja ??
Tusijipe Faraja Sana...
.
 
Mungu alijua watakaoishi mwambao huu akili zao wanazijua wenyewe akaona atuwekee ulinza mapema
Hahaha.. aisee!

Lakini mbona tsunami iliyorindima huko Indonesia (maelfu ya km kutoka Tz) kama miaka 20 nyuma iliua na kusababisha madhara kwa baadhi ya watu pwani ya Dar, au ulikuwa hujazaliwa?
Fikiria ingekuwaje kama tsunami ikitokea hapo jirani kama vile Comoro, nk
 
brother unataka hoja ipi, Sayansi ni hiyo niliyoeleza hapo! elewa ndugu yangu siyo had ukasome!
HATA NEWTON hakusoma sehemu bali alifunuliwa tu!
na mimi nimekufikishia huo ujumbe kawambie wasomi wenzako kwamba SUNAMI HAIWEZI TOKEA TANZANIA
...Kwa hiyo na Wewe Umefunuliwa TU, hukusoma Mahali popote ??? [emoji848]
 
Wamesema itatokea lini?
Leo saa kumi ama?
 
Siyo kuwa lazima itokee hapa, inatokea inakotokea, hapa zinafika athari zake tu.


Tuulize wakazi wa Dar, binafsi nimeshudia mara mbili athari zake Dar. Moja ile msasani yote unayoijuwa ilijaa maji.

Moja Ikulu na Gymkhana Club, Ohio ilijaa maji yote ile. Maji yalifika mpaka viwanja vya Karimjee. Fikiria Ocean Road ilijaa maji ya bahari, si unaona kule oalivyo juu, lakini palijaa maji, mpaka ikaamuliwa ujengwe ule ukuta kando ya bahari. Watu wakajipigia pesa, kile kiukuta ndiyo cha kuzuwia maji ya bahari ya kijaa?

Nilikuwa namfahamu yule mkandarasi, Marehemu Mazhar Khan, alikuwa kijana mjanja mjanja wa mjini, nilipomuona nilicheka sana, akasema mimi nimeona kazi ya kujenga ukuta, nime tender nimeipata, nimeambiwa nijenge ukuta haraka sa, niikatae?

Jamaa sijuwi walimtisha mzee Nyerere ikija tena hii itafika mpaka ndani Ikulu, Mzee aachia mbiombio bila maneno.
 
Ilikuwa miaka gani hiyo?
 
Usipotoshe watu tsunami ya 2004 ilifika hadi bongo na iliondoka na watu 10..kenya na mwambao wa somalia iliondoka na watu 100.
Acha ujinga huo majanga hayatabiriki ni vyema kuwa na utayari muda wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…