TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Naomba niwashauri kitu. Mjitahidi kutanua huduma zenu na kujitangaza ipasavyo.
Ikiwezekana shusheni bei ya vifurushi vyenu, na pia kuhamasisha huduma yenu ya T - Pesa, ambayo kimsingi inasua sua sana ukilinganisha na Mpesa, tigo pesa, Airtel money na pia halopesa!

Nasema hivi kwa sababu nimeanza biashara ya miamala! Ukiondoa kuyumba kwa biashara kutokana na changamoto ya serikali kuongeza tozo kwenye miamala, wenzenu wanapata wateja. Ila TTCL Tanzania hakuna kabisa wateja!

Mnakosea wapi? Mnashindwa vipi na Wageni! Ilhali nyinyi ni wenyeji na mko chini ya serikali! Kimsingi mnatakiwa muwe na nguvu, mfanye zaidi biashara na kujulikana zaidi kuliko haya makampuni ya Mabeberu.[/I]
 
Hongereni na kila la kheri mtakaojiunga na kamari ya TTCL!! Wameshindwa kuhudumia wateja kwenye vitu vidogo kabisa kama kuunga vifurushi vya sms, internet...ndiyo wataweza miamala!!? Wataweza kushindana na wazee wa "ile pesa nitumie kwa namba..."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…