TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

UZINDUZI WA T-PESA APP:

T-PESA yazindua huduma ya T-PESA App ikiwa ni katika kuendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kifedha. Sasa ni rahisi na Salama ukiwa na T-PESA App. #NafuunaSalama
#RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 1997356

View attachment 1997359

View attachment 1997362

View attachment 1997364
Naomba niwashauri kitu. Mjitahidi kutanua huduma zenu na kujitangaza ipasavyo.
Ikiwezekana shusheni bei ya vifurushi vyenu, na pia kuhamasisha huduma yenu ya T - Pesa, ambayo kimsingi inasua sua sana ukilinganisha na Mpesa, tigo pesa, Airtel money na pia halopesa!

Nasema hivi kwa sababu nimeanza biashara ya miamala! Ukiondoa kuyumba kwa biashara kutokana na changamoto ya serikali kuongeza tozo kwenye miamala, wenzenu wanapata wateja. Ila TTCL Tanzania hakuna kabisa wateja!

Mnakosea wapi? Mnashindwa vipi na Wageni! Ilhali nyinyi ni wenyeji na mko chini ya serikali! Kimsingi mnatakiwa muwe na nguvu, mfanye zaidi biashara na kujulikana zaidi kuliko haya makampuni ya Mabeberu.[/I]
 
UZINDUZI WA T-PESA APP:

T-PESA yazindua huduma ya T-PESA App ikiwa ni katika kuendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kifedha. Sasa ni rahisi na Salama ukiwa na T-PESA App. #NafuunaSalama
#RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 1997356

View attachment 1997359

View attachment 1997362

View attachment 1997364
Hongereni na kila la kheri mtakaojiunga na kamari ya TTCL!! Wameshindwa kuhudumia wateja kwenye vitu vidogo kabisa kama kuunga vifurushi vya sms, internet...ndiyo wataweza miamala!!? Wataweza kushindana na wazee wa "ile pesa nitumie kwa namba..."
 
Back
Top Bottom