Kiukweli wanapata mishahara ya bure tu hakuna wanalolifanya. Inasikitisha sana na wenye mamlaka wamekaa tu kimya unashindwa hata kuelewa kuwa hivi hii nchi ina laana au ni nini?
Facilities za ofisi pia wanatumia bure kuanzia furnitures, Umeme, viyoyozi, internet kwaajili ya kuperuzi nk mpaka unashangaa mbona Waziri husika yupo kimya tu au tuseme bado anatafakari futari waliyomuandalia kipindi cha mfungo kwanini hasemi hata jambo ni kwamba hizi kelele hazisikii au haelewi matatizo yanayolikabili shirika? Msajiri wa hazina alikutana na wenyeviti wa bodi pamoja na viongozi wao sina hakika kama alieleweka kwenye ule mkutano juu ya dhana ya mashirika ya umma kujiendesha kibiashara.