TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Ttcl hamko serious na vifurushi vyenu.
Nilikuwa na laini yenu nikasema leo niweke ni jaribu.
Nikanunua bando la bandika bandika bandua.
Tatizo masharti yenu yamenishinda .
Mnatoa gb 4.
Lakini mmeweka limit mchana mb 500.
Alafu usiku kuanzia saa 6 mpaka saa 12 asubuhi ndo unatumia gb 3.5.
Haya masharti kwa kweli ni magumu

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Naomba Rudisheni kifurishi cha night toboa pack cha 10gb usiku kwa tshs 1000 na boom pack ya siku 600mb kwa tshs 500.

Mtatusababishia tena tuhame mtandao japo tunaupenda jamani kutokana na vifurushi vya sasa
 
Pole sana.
Tupo kwenye maboresho ya vifurushi vipya ambavyo vitampa uhuru mteja wetu.
Natumaini utavifurahia.
 
 
Kwahiyo hili tangazo ni kwa wakazi wa Dar tu, vipi mikoani?

Generally speaking TTCL mna miundombinu mizuri lakini customer care ni 0 marks
  1. Ukipiga simu kuomba msaada kuna mawili, wasipokee au wapokee lakini usisaidiwe kabisa kwa kisingizio cha "mhusika yupo kwenye conference call!
  2. Waweza kuomba msaada wa kuingiza vocha kwenye simu, huwezi kupata ile 24/7 customer support service, ukiona vocga haiingi kwenye simu baada ya saa za kazi basi hapo imekula kwako. ...subiri mpaka kesho na kama ni Ijumaa basi nika kumtoa mtuhumiwa polisi kama atakuwa amekamatwa Ijumaa
 
Jongea Maeneo ya Viwanja vya Social Center - SINGIDA-Mjini ukiwa na kitambulisho cha Taifa ilikuweza Kusajiliwa Laini yako mpya Au ya Zaman ya TTCL Co-orporation
# rudinyumbanikumenoga ufurahie ofa Kubwa ya Dk, sms na Gb za Kutosha
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Dkt Zainabu Chaula akiongozana na Mkurugenzi Mkuu TTCL Corporation Waziri Kindamba na Mtendaji Mkuu wa UCSAF Justina Mashiba watembelea ujenzi wa minara ya mawasiliano katika kisiwa cha Rubondo katika eneo la hifadhi Pongo View na Kijiji cha Bulongero ambapo mawasiliano yanategemewa kuwashwa hivi karibuni.

Sehemu ambayo minara itazinduliwa na kuwashwa kwa kasi ya spidi kali ya 4.5G ni pamoja na:
[emoji819]Chato
[emoji819]Bukome
[emoji819]Igando
[emoji819]Nyabilezi
[emoji819]Bwera.


Rudi Nyumbani Kumenoga.
 
Kwahiyo huko ndiyo kuna watumiaji wengi?
 
Mnazingua kishenzi yaani.

Kampuni ipo tangu hatujapata uhuru mpaka leo hata hallo tel inawazidi uwezo

Shame on you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…