TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Natumia TTCL laini mwaka sasa. Kero zangu ni hizi hapa:

1. Menu ya TTCL ya kuangalia salio la bando ni ya kidwanzi kuliko udwanzi wenyewe. Yaani unaingia menu, unabonyeza kuangalia salio, HAFU ETI ANATOKEA SUB MENU ANAKUULIZA SALIO LA SMS, DAKIKA, AU MB, unajifanya fala unabonyeza dakika, ANATOKEA TENA ANAKUULIZA DAKIKA ZA TTCL KWENDA TTCL AU KWENDA MITANDAO MINGINE??????? SERIOUS??????????

2. Vifurushi vya SMS wamevibana sana. Mfano Chat Kijanja ndio ninao jiunga eti Buku 1 unapata SMS 1000 kwa week. Hakuna vifurishi vya SMS unlimited. Igeni kwa wenzenu.

3. Internet ikifika usiku haina kasi kabisa. Yes tunajua ni peak hours kila mtu yupo Quarantine kwake anatumia ila kwenu too much inaelekea kuna kitu mnabinya.

4. TTCL anzisheni App ya T-Pesa.

Kama wameshataja wadau hayo sorry ila mengine wataongeza wakuu.
 
Sina uhakika kama utajibu.. Ila yangu ni haya:
1. Meneja Masoko wenu ameshindwa kazi.. Hampo popular.. Yaani kuna siku niluamua hadi kupiga simu kuulizia menu ya T-pesa.

2. Kuna kipindi nilienda Jijini Mbeya kikazi.. Kule ukinunua kifurushi cha internet ya TTCL basi ujue umeamua kutoa sadaka.. Hutatumia hata Mb 1. Ile ni extremely slow.

3. Hamna utaratibu wa kuwachombeza wateja.. Wenzenu wana vi sms au call kukbushia jambo
Haha kutoa sadaka🤣🤣🤣🤣
 
Freelancer wa TTCL wanalalamika wanakuja ofisini kununua laini 50 lakini wanalazimishwa kununua laini 20 hivyo kwa mwenzi inabidi harudi zaidi ya Mara mbili tatizo nini
 
Nyumbani kumejoga na tumerudi..

Swali langu ni kwanini mmebadirisha bei za vifurushi bila kutupa taarifa sisi wateja wenu.

Pili kwanini ttcl inapatikana katikati ya miji tu..ukitoka kidogo nnje ya mji hupati huduma kama inavyotakiwa hasa upande wa data..

Hongereni kwani upande wa voice mpo vizuri mno
kwa vifurushi wamezingua sana
 
Mimi huwa si mteja wa TTCL, ila kuna location fulani fulani huwa nikienda natumia mtandao wao.

Leo kuna kifurushi cha internet cha bandika bandua saa 24 (@TSH. 1000/=) kiliandikwa GB 4.. Sasa nashangaa nimejiunga nikawasha data, nikadownload "Dream League Soccer 2020" (MB 316) nkapat ujumbe et nimebakiwa na MB 50. Je, hii maana yake nini?
Hukosoma vizuri, bandika bandua kama ni 4GB huwa wanatenganisha, usiku labda 3 na mchana 1. Uwe unasoma kwanza na kuelewa menu.
 
Back
Top Bottom