TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Mnajiharibia Soko
Mmepunguza Bando la Mwezi ......

Mnasababisha sisi wengine tuanze kutafuta Mitandao mengine

Tuliwapendea kwenye Bando za GB
Leo ovyo kuliko Halotel

Ovyo kabisa
 
Ndugu mteja Deceiver, Kibaha kuna ofisi ya TTCL maeneo ya Mkoani jirani na ilipo shule ya Kibaha Independent Pre & Primary School.


Rudi Nyumbani Kumenoga
pale kuna majengo ya ttcl, ofisi kama ofisi nakataa! tatizo la finger print tu iliandikwa emai kwenda head office na nikaambiwa niende kesho yake kwa majibu, utasema kuna ofisi hapo?
 
Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation lazindua Promosheni ya KARIBU NYUMBANI inayolenga kuwakaribisha Wateja wapya.

Katika Kampeni hiyo wateja wapya watapata Dakika,SMS na MB.


# RudiNyumbaniKumenoga

Kila ukijisikia unafungua Uzi mpya badala ya kuendeleza ule wa mwanzo!
After all, mna bore ktk huduma zetu! Mlianza vizuri lakini baada ya kujiaminisha kuwa mmeteka wateja wengi, mkaamua kupunguza vifurushi. Sasa mmeiona ngondo, mmeamua kurudi kivingine.
 
[emoji16] [emoji16] [emoji16]
Mkuu nimewachoka vifurushi vyao kidogo halafu wezi pia bado kama bandika bandua wanakupa 4gb 500mb cha mchana ikifungua whats tu zimeisha atii doooh,kifurushi cha toboa wameondoa ukiweka line ya chuo mb kutoka 500mb mpaka 150mb no way bora nirudii kwa size yako tigo
 
Hakiki namba zako kuepuka usumbufu.




JINSI YA KUPATA RUHUSA YA TTCL ILI KUTUMIA NAMBA YA ZIADA.

A.KUHAKIKI NAMBA KUU.
1. Piga *106#

2. Chagua namba 4 (Hakiki namba)

3. Ingiza namba ya kitambulisho.

4. Chagua namba "1" kuhakiki namba kuu.

5.Ingiza namba ya simu kuu.

B.KUHAKIKI NAMBA YA ZIADA
1. Piga *106#

2. Chagua namba 4 (Hakiki namba)

3.Ingiza namba ya kitambulisho.

4. Chagua namba "2" kuhakiki namba za ziada.

5. Chagua namba unayotaka kuhakiki iwe ya ziada kisha chagua matumizi ya hiyo namba.

MENGINEYO
Huu ni ujima, huu ni ujinga wa wataalamu husika wa kufanya mambo kwa staili ya zimamoto. Namba zote zilisajiliwa kwa alama za vidole, tukiaminishwa ni fulproof. Hata mwaka haujapita linakuja la uhakiki. Hakuna mwenye namba nyingi bila matumizi nazo. Kuna mawakala, ofisini namba za kazi na binafsi nk. Binadamu amezaliwa huru na hata umbane vipi, ipo siku atakudai uhuru huo kwa nguvu.
 
Habari yako Mr. Kamugisha.
Je, unapata tatizo lipi unapotumia huduma za TTCL?

Internet inaload tu uwezi hata fungua You tube, uwezi soma email, ipo slow uku mikoani, yaani ukitoka nje ya mji kidigo TTCL ndio bye bye, vijijini ukija na line ya TTCL unakuwa umefanya kazi bure

Cha kushangaza mitandao mingine inapata huduma toka kwenu na inafanya vizuri ila nyie sasa dah!!

Acha tu tuendelee kuwaombea

Tunatamani tubaki na line moja ya TTCL ila sasa mnatukatisha tamaa!!
 
Internet inaload tu uwezi hata fungua You tube, uwezi soma email, ipo slow uku mikoani, yaani ukitoka nje ya mji kidigo TTCL ndio bye bye, vijijini ukija na line ya TTCL unakuwa umefanya kazi bure

Cha kushangaza mitandao mingine inapata huduma toka kwenu na inafanya vizuri ila nyie sasa dah!!

Acha tu tuendelee kuwaombea

Tunatamani tubaki na line moja ya TTCL ila sasa mnatukatisha tamaa!!
Ooh pole sana
 
Imekuwa kero ss , nilivyonunua line nilisajiliwa, nilipata NIDA nikasajikiwa tena, nikapoteza line kisha nikasajikiwa tena ss uhakiki wa nn wakat namba tayar mnazo ?
 
Back
Top Bottom