TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Sijacheki tena ila kama mmerudisha kwa hiyo 2500 basi endeleeni kuweka hivyo hivyo 2500 maana kama Halotel na Airtel wana 4G wanafanya 1500 basi nyumbani kutanoga zaidi maana kupanga ni kuchagua..
 
Imekula kwenu mliozoea kutukana ovyo
IMG_20200918_174951_642.JPG
 
Msimamizi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano,TTCL Corporation na Mamlaka ya Uendeshaji wa Mkongo Zanzibar (ZICTIA) wasaini makubaliano baada ya kufanikisha kuunganisha Mkongo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mkongo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo , katika hafla iliyofanyika Ofisi za Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Zanzibar.


Tukio hilo lilishuhudiwa na Katibu Mkuu Dkt.Mustafa Aboud Jumbe, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji na Katibu Mkuu Dkt.Zainabu Chaula, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Mawasiliano)
120096426_10159003060047884_4353134919640427324_n.jpg
120006772_10159003059852884_5231555860706497112_n.jpg
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (T-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)

- Maeneo gani? (Tukifahamu maana ulipo, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate msaada toka kwa wakala wetu aliye karibu nawe)

- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?

- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza.

- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.


Zifuatazo ni ofisi zetu za huduma kwa wateja ndani ya jiji la Dar es Salaam.


1. POSTA
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Samora, jengo la Extelecom ghorofa la Chini.


2. KARIAKOO
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Makamba/Msimbazi, jengo la Akamba Bus Service.

3. UPANGA
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Magole/Maliki, karibu na Diamond Jubilee.


4. MAGOMENI
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Minaki/Fundiki, karibu na Manispaa ya Kinondoni.


5. KIJITONYAMA
[emoji654][emoji654][emoji654]Kijitonyama Sayansi, barabara ya Ali Hassan Mwinyi/ Rose Garden.


6. OYSTERBAY
[emoji654][emoji654][emoji654]Barabara ya Haile Selassie.


7. UBUNGO
[emoji654][emoji654][emoji654]Jengo la Ubungo Plaza/ Ghorofa la chini.


8. MBEZI BEACH
[emoji654][emoji654][emoji654]Mbezi Makonde/ Jengo la Shamo Tower.


9. TABATA
[emoji654][emoji654][emoji654]Tabata Bima, barabara ya Segerea karibu na kanisa la Romani Katoliki.


10. CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.
[emoji654][emoji654][emoji654]Jirani na tawi la benki ya NBC, jirani na kilipo kituo cha polisi cha UDSM.


11. BARABARA YA PUGU
[emoji654][emoji654][emoji654]Barabara ya Mwalimu Nyerere, karibu na Sigara.


12. WAGENI
[emoji654][emoji654][emoji654]Uwanja wa ndege.


13. PUGU
[emoji654][emoji654][emoji654]Jengo la Quality Centre, ghorofa la chini.


14. KISUTU
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Mchafukoge/Libya jengo la Haad Plaza.


15. TEGETA SHOP
[emoji654][emoji654][emoji654]Jengo la Kibo Complex, ghorofa la chini.


16. MWANANYAMALA SHOP
[emoji654][emoji654][emoji654]Mwananyamala A, barabara ya Mwinjuma yalipo makutano ya Mwananyamala A.


17. KURASINI
[emoji654][emoji654][emoji654]Kurasini Exchange Area, jirani na Chuo cha Diplomasia.


Wasiliana nasi:
[emoji337]022 210 0100
[emoji390] 0738 151 511
[emoji273]www.ttcl.co.tz


#RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 1529645


Karibu.

Rudi Nyumbani Kumenoga


Utaratibu wa kuangalia salio kwenye line zenu mrefu mno moaka unachosha inakuwa kama unaomba kazi maswali mengiiiiii! Kwanini isiwepo code moja tu kama tigo *102*01 inakupa aina zote za salio alilonalo mteja badala ya kujibu maswali mengi kama vile unajaza kufurushi
 
Utaratibu wa kuangalia salio kwenye line zenu mrefu mno moaka unachosha inakuwa kama unaomba kazi maswali mengiiiiii! Kwanini isiwepo code moja tu kama tigo *102*01 inakupa aina zote za salio alilonalo mteja badala ya kujibu maswali mengi kama vile unajaza kufurushi
Asante kwa ushauri wako ndugu mteja.
Na pia pole sana kwa changamoto.
Tatizo la kuangalia salio litatatuliwa ndani ya mwezi huu.
Nakutakia mchana mwema.
 
Back
Top Bottom