TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Wekeni

Hebu wekeni T-Connect Plus ya mwezi inayoleta mantiki hata kama ni equivalent to weekly bundle manake ni ujinga kifurushi cha wiki kuwa Sh.10,000 kwa GB10 halafu kifurushi cha mwezi kuwa Sh 70,000 GB40 au eti GB15 kwa Sh 30,000...
Habari, Ahsante kwa kuwasiliana nasi.Tumepokea ushauri wako na tunaufanyia kazi.
Ahsante
 
Nyie ni wapumbavu wakubwa hivi customer care hamna watu tunapiga simu hazipokelewi maana yake nini halafu shirika likibinafusishwa mnapiga kelele au hamjui mnatumia kodi zetu
Habari, ahsante kwa kuwasiliana nasi.
Tunaomba kujua changamoto unayoipata pindi utumiapo huduma zetu za TTCL kwa msaada zaidi.
Ahsante
 
Hivi customer care wa ttcl kupokea simu ni hiyari au lazima, nimepiga nusu saa nzima wananiwekea muziki.
Halafu kwanini tunajiunga na internet mnatufungia insta picha hazifunguki, blog kama salehjembe hazifunguki halafu mnalalamika mapato madogo
Habari, ahsante kwa kuwasiliana nasi.
Tunaomba kujua changamoto unayoipata pindi utumiapo huduma zetu za TTCL kwa msaada zaidi.
Ahsante
 
Nyumbani hakujanoga tena bali kumedoda !!!!!!!!!
Aisee nimeingia Mjini leo toka porini huko nimekuta :-
Hakuna tena toboa tobo ya kushushia mizigo, Bandika bandua nayo nikijaribu kuunga kile cha 10GB kwa 2500 napata ujumbe " sorry,your input is invalid" wamekiacha kile cha 4GB tu.
Nikasema niende Boom nako wanakupa 350M kwa Jero japo kwenye Menu wanasema ni 600MB ,
Habari, ahsante kwa kuwasiliana nasi.
Tunaomba ututumie PM namba yako ya TTCL kwa msaada zaidi.
Ahsante
 
Sijuhi TTCL mnahujumiwa au mnajihujumu....siku ya tatu leo T-PESA haipokei pesa kutoka MPESA, sasa jiulize vifurushi tutajiungaje?
Habari, ahsante kwa kuwasiliana nasi.
Tunaomba kujua changamoto unayoipata pindi utumiapo huduma zetu za TTCL kwa msaada zaidi.
Ahsante
 
Huu mtandao una matatizo gani maana huku niliko leo siku ya tatu hatuna mawasiliano kwanini mimi niko Mbondo.
Habari, ahsante kwa kuwasiliana nasi.
Tunaomba kujua changamoto unayoipata pindi utumiapo huduma zetu za TTCL kwa msaada zaidi.
Ahsante
 
sim card yangu ya ttcl wakati mwingine inaandika ,sim came off,then inakuwa haisomi kwenye simu yangu nkiiuliza huduma kwa wateja naambiwa iko active
sasa naomba kuuliza hili tatizo lipo kwa sababu gani na solution yake nin?
Habari, ahsante kwa kuwasiliana nasi.
Tunaomba namba yako ya TTCL kwa msaada zaidi.
Ahsante
 
Kwa mara ya kwanza ttcl kuwasha mtandao wao Malampaka Simiyu ni septemba 2019. Nilifurahi maana nilikuwa nikirudi likizo nyumbani haisomi.
Habari, ahsante kwa kuwasiliana nasi.
Tunaomba namba yako ya TTCL kwa msaada zaidi.
Ahsante
 
Kampuni ya serikali lakin bado haifanyi chochote, makampuni mengine ya uwekezaji wako bize wana rahisha japo me gine yana usumbufu na ujanja ujanja mwingi, nyoe mko bize kutoa GB 9 usiku, for what?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Habari, ahsante kwa kuwasiliana nasi.
Tunaomba kujua changamoto unayoipata pindi utumiapo huduma zetu za TTCL kwa msaada zaidi.
Ahsante
 
Ni aibu, narejea tena ni aibu. Ukipiga simu huduma kwa wateja TTCL huwezi amini utaenda bafuni kuoga na kurejea bado unaambiwa subiri kwani simu yako ni muhimu. Hii ni muda wote.
Jaribu TRA, utapokelewa na kama si muda wa kazi utaambiwa.
TTCL mnasindwa wapi?
Habari, ahsante kwa kuwasiliana nasi.
Tunaomba kujua changamoto unayoipata pindi utumiapo huduma zetu za TTCL kwa msaada zaidi.
Ahsante
 
Back
Top Bottom