TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Siyo kweli asubuhi niliona ila sasa hivi ukiingia kwenye menu ya Tpesa hamna option ya kununua vifurushi ambako ndio unapata bando tamtam customer care wanadai bado mnafanya mabadiliko
Tafadhali tunaomba uwe mvumilivu wakati wataalam wakiendelea kutatua changamoto hiyo.

#RudiNyumbaniKumenoga
 
Admin wa id ya ttcl kajibu maswali magumu, kashindwa kujibu swali jepesi, iko wapi menyu ya kulipia bando kupitia t pesa?
Ndugu mteja, wataalam wetu wanaendelea kutatua changamoto ya kununua bando kupitia T PESA.
Tafadhali tunaomba uwe mvumilivu.


#RudiNyumbaniKumenoga
 
Moja, T-pesa mbona hamna option ya kununua vifurushi, na vocha zenu zilivyo mpaka uzifungie safari ofisini.

Mbili, naomba kuuliza ni wizi/uongo mnafanya lile bando la tamtam GB 1 siku tano cha ajabu hata siku haiishi nalo limeisha tofauti na muda kiasi nilikuwa nafika hata siku tatu na mtu mwenyewe matumizi sio ya kasi hyo kumaliza GB 1 kwa masaa.
 
Moja, T-pesa mbna hamna option ya kununua vifurushi, na vocha zenu zilivyo mpaka uzifungie safari ofisini.

Mbili, naomba kuuliza ni wizi/uongo mafanya lile bando la tamtam GB 1 siku tano cha ajabu hata siku haiishi nalo limeisha tofauti na mda kiasi nilikua nafika hata siku tatu,na mtu mwenyewe matumizi sio ya kasi hyo kumaliza GB 1 kwa masaa.
Hiyo gb 1 siku tano, walikuwa wanauza sh. Ngapi?
 
Moja, T-pesa mbna hamna option ya kununua vifurushi, na vocha zenu zilivyo mpaka uzifungie safari ofisini.

Mbili, naomba kuuliza ni wizi/uongo mafanya lile bando la tamtam GB 1 siku tano cha ajabu hata siku haiishi nalo limeisha tofauti na mda kiasi nilikua nafika hata siku tatu,na mtu mwenyewe matumizi sio ya kasi hyo kumaliza GB 1 kwa masaa.
Mkuu bundle ni kama ndoo ya maji..matumizi yako ndio yatadetermine ndoo ya maji ikae siku ngapi
 
Alafu mpo kama mmeridhika tu kutusumbuaga wateja wenu, kuna changamoto ni za muda mnoo tunalalamikaga lakini kama hamtatui sijui.

Network yenu ya manati unaweza ukawa hata mjini isishike, vocha saasa kama huna T-pesa na hujui kununua kupitia kagaconnect au m-pesa direct ndio ujiandae uifungie safari.
 
Mkuu bundle ni kama ndio ya maji..matumizi yako ndo yatadetermine ndio ya maji ikae siku ngapi
Bando hilo hilo, matumizi yangu ni yale yale lilikua linafika hadi siku siku tatu hayana tofauti na matumizi haya haya ambayo bando halimalizi hata siku washaanza kunijazia text kama za umetumia asilimia 75 sijui nini, na ndo swali langu liko hapo.
 
Bando hilo hilo, matumizi yangu ni yale yale lilikua linafika hadi siku siku tatu hayana tofauti na matumizi haya haya ambayo bando halimalizi hata siku washaanza kujijazia text kama za airtel umetumia asilimia 75 sijui nini, na ndo swali langu liko hapo.
Mkuu matumizi hayawezi kuwa sawa...piece kali zinaongezeka lila siku
 
TTCL punguzeni zaidi data, hiyo ni biashara ili mkiweza mteke soko hilo baadae mnatoa na promotion za kumwaga siku mkiongeza kidogo wananchi hawatapiga kelele na siku za sikukuu mnakua na promotion yenu ni kama hapa Telcom SA wanakimbiza mno wana data za mwezi za bei nzuri kwa hiyo mzunguko upo juu hao MTN na Voda wameweka mpaka watu wa kuzunguka mtaani ila hiyo telkom ni kiboko...
 
Back
Top Bottom