A
Anonymous
Guest
Habari,
Mimi ni mkazi wa Morogoro mjini.
Changamoto niliyokutana nayo TTCL Morogoro ni kuwa nilituma maombi kwa ajili ya kuja kufungiwa fiber internet kwenye eneo langu la kazi lakini maombi hayo hayakujibiwa mpaka nilipoenda ofisini kwao kuwauliza.
Wakaniambia subiri zamu yako ikifika utahudumiwa, wakaniambia wasiliana na fundi anatehusika na kuweka fiber aje kuangalia eneo lako kama kuna nafasi.
Nikampigia fundi, akaniambia akimaliza huko aliko atanipigia Ili aje lakini hakupiga nikasubiri mpaka mwaka ukaisha na maombi nimetuma toka mwezi wa nane 2025.
Nikaja kumpigia Tena fundi nikamuuliza vipi fiber napata? Akasema kile kifaa Cha fiber ambacho kwa mwezi unalipia 55,000/- vimeisha na havijaletwa muda ila kifaa ambacho kipo ni Cha 100,000/-
Mimi nimeona kama Kuna Hali ya upigaji au utoe hela kidogo Ili upate kile Cha kulipia 55,000/-
Mbona mikoa mingine kama Mbeya vipo vya kutosha mpaka wanatembeza mitaani? Kwanini Morogoro havipatikani wanasingizia havijaletwa na havipatikani?
Kwakweli hii TTCL Morogoro hawako serious, na pia eneo nililopo wanasema nafasi zimejaa. Yaani ni shida!