Tuache kudanganyana, Ajira zina afadhali zaidi kuliko kujiajiri, watu wengi waliojiajiri ndio wapo kwenye utumwa

sijawahi na sitaki hata kuajiriwa na wala sjatoka familia ya kishua but mishe nazopiga kukunja 5m to 10m kawaida sana kwa mwezi

But mpaka nimefikia level hii ni kwamba nimepmbana kwa jasho na damu mzee japokuwa sometime nakula loss mpaka ya 6m but still fighting

kujiajiri kutamu mno sema kunamtaka mtu mwenye roho ya paka
 
Kwa upande wangu kujiajiri ni bora maana nimefanya hivo miaka yote japo changamoto zipo, lakini unakabiliana nazo tu, tena kwa nchi zetu za dunia ya tatu ni afadhali kujiajiri maana hata fursa ni nyingi wakati kwenye dunia ya tatu kuajiriwa malipo ya waliowengi hua ni kidogo sana
 
Mtu anaelipwa 700k halaf hela haikut mwezi ujao labda wenye sekta za ovyo kuna watu wana marupurupu huo mshahara hawaugusi yaan wapo humo serikalin so msikariri
 
kotekote kuzuri tu kama umekaa pazuri.

Sasa kama umeajiliwa na kazi unaijua na mshahara wako kwa mwezi ni 15m net au zaidi unashida gani zaidi ya kuenjoy.

Kama umejiajili na una kipato cha 15mil na zaidi kimesimama shida nini.. hapo ni kipato tu.
 
Mtu anaelipwa 700k halaf hela haikut mwezi ujao labda wenye sekta za ovyo kuna watu wana marupurupu huo mshahara hawaugusi yaan wapo humo serikalin so msikariri
(Halaf ,Haikut,serikalin,so )rekebisha hayo maneno Kisha tuendelee na mjadala husika itakuwa ngumu sana Kwa mtu kama wewe kuweka akiba kutokana na mshahara wakati hayo maneno yanakushinda kuandika.
 
Wewe utakua dalali wale wanaosumbua watu wanaotaka kuuza nyumba zao na viwanja vyao.
 
Huu ushauri ungeenda kuutoa kwa Waajiriwa wenzako
 
Ushauri wa kijinga sana huu,
 
Twende Mbele turudi nyuma, saiz kila mtu anapambana aajiriwe kwanza, hayo mambo ya kujiajiri yanakuja baada ya kuajiriwa.
Sio kila mtu.
Ajira inategemea mshahara kwakweli. Kuna mtu anataka kukupa kazi unapiga hesabu unaona hii ajira haifai bora niendelee na mishe zangu sio kuchukua gross sijui 800k.
Ila kuna ajira zina mshahara na marupurupu yani huwazi mara mbili
 
Uzuri wa kujiajiri kipato kina leverage ila lazima ukumbane na ups and downs lazima ukubaliane nazo.

Kuna hatua ya kujiajiri unafikia angalau unapumbua na hapa lazima uwe nawe umeajiri watu wako wa kukufanyia kazi.

Kuajiriwa ni kuwa na mipaka ya kipato na kama ni kidogo utajamba cheche maana kama matumizi na gharama za maisha zinapanda daily ,lazima uwe smart kujiongeza pembeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…