Tuache kudanganyana, Ajira zina afadhali zaidi kuliko kujiajiri, watu wengi waliojiajiri ndio wapo kwenye utumwa

Kuna siku nilikua nachangia 1 ya Thread za Member wa Humu JF

Niliandka kama comment lakini leo ile comment kuna mtu kaifungulia Thread kabisa

its simple and clear hiki ndio kinachopatikana kwa wafanyabiashara👇

 
.....nadhani hii itakuwa battle mpya JF kati ya waajiriwa na wajasiriamali/wafanyabiashara sababu naona kila mtu anavutia alipo,....lakini jaji mzuri katika hili ni yule aliewahi kujiajiri na kuajiriwa, anaweza kujipima mwenyewe.......
 
Ukweli ndio huo. Kuna watu wengi sana walifunga biashara hapo katika awamu ya tano, lakini hatujasikia walioacha ajira awamu hiyo. Hiyo inaonyesha kwamba biashara sio kitu kinachotabirika kimapato, upepo mdogo tu unaweza ukakupoteza mjini
Hamkuacha kazi sababu mmefungwa na kiinua mgongo. Ila ratiba ya matumizi na chakula nyumbani tunajua mliyoyapitia
 
Wananiona nina Pesa kwasababu siendi kwenye sherehe zao,

kadi zao nachangia michango minono,swala la pesa si tatizo

wanahisi na ringa,najiskia,najiona eti Najikuta,NK lakini ukweli wa

yote hayo namna gani npo labda wataujua nikifariki nikiwaacha hapa duniani

lakini binafsi nimechagua BIASHARA ndoa yangu takatifu niliyoifunga 2012 ambayo

nilisema ni kifo tu kitanitenga nayo basi ni BIASHARA na kadri umri unavyozidi kwenda

mahaba yanazidi kukolea kwa huyu mwali wangu, Nishaachwa na Wanawake kibao

kwa kukosa tu MUDA wangu wakihisi nina wanawake wengine hahaha Vile Sijali sasa

What is Love? How do you know your in Love?

When its hurt but i still wanna stay... i have a pure love na BIASHARA aisee inaniepusha

na mengi inanikutanisha na wengi,SAD enough connection ninazozipata sina muda

wa kuzitumia...Probably nilizaliwa nifie kwenye biashra hahaha... ila bana eeeh

Biashara sio ya Kila Mtu,ukiona ngumu Ajira kibao TAMISEMI wanatangaza daily...

Siwezi Ajiriwa kulipwa hela za kupimiana wakati nakuingizia mamilioni ya pesa...NEVER
 
Uarabuni wanaenda wafanyabiashara, sisi waajiriwa tunawasubiri watuletee kodi tuzile za dezo
Kumbe unapenda dezo? Kuwa makini mkuu, sasa dezo hizo za kurisk kufa kwenye misafara ya mikoani ili ujilipe per diem si bora uwe unaenda tu pale New Africa Casino utakutana na wanaume wakupe pesa bure kabisa bila kujichosha.
 
Kumbe unapenda dezo? Kuwa makini mkuu, sasa dezo hizo za kurisk kufa kwenye misafara ya mikoani ili ujilipe per diem si bora uwe unaenda tu pale New Africa Casino utakutana na wanaume wakupe pesa bure kabisa bila kujichosha.
Ndipo huwa unaenda huko halafu unasema biashara inalipa? 🤣.
Kumbe biashara yenyewe ndio hiyo? Hapa siachi ajira kabisa, wewe endelea tu kwenda New Afrika !
 
Ndipo huwa unaenda huko halafu unasema biashara inalipa? 🤣.
Kumbe biashara yenyewe ndio hiyo? Hapa siachi ajira kabisa, wewe endelea tu kwenda New Afrika !
Si mtoto wa kiume unafurahi kabisa eti unapata pesa za dezo. Sasa kuliko unasaga soli kudandia daladala huko Mbagala kwenda Posta we lala jioni nenda pale utapata za dezo ambazo hazitakuletea karaha ya kupakazana jasho huko Mbagala charambe
 
Mimi nina bamdogo wangu anaishi jijini hapa amejiajiri yeye kila siku anafunga biashara yake saa nne usiku namwonaga anateseka sana na hana sikukuu wala jumapili, akishatoka kanisan anaingia kwenye biashara yake mpaka saa 4 chakula cha usiku anakula saa tano hadi saa sita. Lakini nina bamdogo mwingine yeye ameajiriwa na kwenye hiyo kazi yake kuna mda anakua free anakaa home mpaka itokee kazi anaitwa anaenda na analipwa mwisho wa mwezi hela nzuri. Hapo ushauri tusifate mkumbo wa kutamani kuwa kama Azam na Mo kwasababu Mungu ametuumba watu wachache tuwe matajiri wakubwa na watu wengi tuwe na maisha ya kiwango flan cha kawaida. Embu fikiria kila mtu akiwa kama Mo tajiri namba moja Tanzania tuwe ni watu milion60, Haiwezekani
 
Wewe hapo ni tofauti na watu wengi waliojiajiri hapa bongo wengi waliojiajiri ni watumwa wa kulipa kodi ya frem na kodi ya TRA hawawezi kwenda likizo kama hiyo unayoisemea wewe
 
Muajiriwa anayejisifia anapata 2m per diem akijiandalia tu ziara ya mkoani anakesha kwenye vibanda umiza akibet sh 3500 na 3700
Kadi nyekundu na penati zimenipa kilo moja


View attachment 2374182


////////////////////////////////////////////////////////////////////////
////////////////////////////////////////////////////////////////////////

View attachment 2374222
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…