Tuache kudanganyana, Ajira zina afadhali zaidi kuliko kujiajiri, watu wengi waliojiajiri ndio wapo kwenye utumwa

Tuache kudanganyana, Ajira zina afadhali zaidi kuliko kujiajiri, watu wengi waliojiajiri ndio wapo kwenye utumwa

Uncle bright
Braza Mimi ni mtumishi wa umma kwa muda wa miaka 11 (since 2012)
Nilianza chini sanaa kutoka ofisa wa chini sanaa mpaka sasa Nina haka la masters.

Ila pia ni mfanyabiashara kwa miaka mi 2 sasa (2021).

In nutshell:-
Ni Bora kubwa sanaa kujiajiri kwenye biashara kuliko ajira ya serikali.

Na muda mwengine najuta kwanini sikuanza biashara mapema.

Ajira na hasa hii ya serikali ni UFALER MKUBWA SANAAA.

#YNWA
Waambie wakuskie wanasema nawatukana sana
 
Najua kwa haraka haraka mtafikiria kunijibu kwamba "Mwajiri hawezi fikia mafanikio ya Mo ai Bakhresa" ....vuta pumzi tulia!! Hao kina Mo watoe akilini mwako maana wapo kundi tofauti kabisa ni wafanyabiashara waliofikia mafanikio ya biashara zao kujiendesha hata wakiwa wamelala.

Mtu mwenye ajira hapa bongo serikalini ana nafuu zaidi maana mwisho wa mwezi mwajiriwa ana uhakika ila aliejiajiri ni juhudi zake, akipoteza mda imekula kwake.

Mwajiriwa hata akifiwa, akiumwa, akioa/kuolewa, anapewa kalikizo.. hapo kila jumamosi na jumapili yupo free, bado ana likizo ya mwezi moja kila mwaka, sherehe za serikali na za dini haendi kazini, Ana muda mwingi wa kuweza kupumzika na familia na kufanya shughuli za kijamii.

Wafanyabiashara wengi nawajua tangu nimepata akili za kuijua dunia mpaka leo hii wao siku ya kupumzika ni christmas tu, wenye nafuu huwa wanapumzika jumapili pekee, siku zingine hizo ni bampa to bampa wanaondoka alfajiri wanarudi usiku, yani hata muda wa kuspend na watoto hawana,

Ukiwa kwenye ajira unaweza kujiajiri pia

Nani mtumwa hapo
Akili za kitumwa hizo.

Principle ya kutokuwa mtumwa ni kujituma.

Ulifikiri kujiajiri ni kutokufanya kazi?
 
Mimi nadhani ajira ni utumwa mkubwa, kwanini mtu akupangie kipato?
Unaweza ukajipangia kipato lakini hakitimii sasa ! 😁 Si inategemea na wateja wako, ambao hawaaminiki kama watabaki na wewe au watahamia kwa mwingine!
 
Kuajiriwa hakuna uhuru wa kipato kwa mwezi unalipwa mara1 na kwa mwaka mara12 labda upate bonus au ofa za xmass na mwaka mpya
Unaweza ukawa umejiajiri na kujilipa kila siku, yaani mara 30 kwa mwezi, lakini jumla yake haimfikii anayelipwa mara moja kwa mwezi
 
Binafsi nimeacha ajira yenye mshahara wa 1,050,000 Gross take home ilikuwa 830,750 niliacha nikafanga mishe zangu za kajiajiri Leo Nina staff 3 na maisha yanakwenda japo kuna maswala kadhaa nimepunguza kama matumizi yasio na ulazima kipato napata mpaka mara 3 ya mshahara wangu nilikuwa nakupata
Tena uombee uzima na nguvu kila siku. Lakini siku ukiugua ukalala kitandani wiki mbili tu, utaiona tofauti
 
Utasikia Job Security
Ukweli ndio huo. Kuna watu wengi sana walifunga biashara hapo katika awamu ya tano, lakini hatujasikia walioacha ajira awamu hiyo. Hiyo inaonyesha kwamba biashara sio kitu kinachotabirika kimapato, upepo mdogo tu unaweza ukakupoteza mjini
 
Inategemea uko wapi huko serikalini. Mimi hapa nipo najaza fomu ya ruhusa, tunaenda kujifungia huko nje ya mji ili tujilipe perdiem ndefu za nje ya mkoa. Kazi ya kufanya siku tano tumejaza wiki mbili. Tunakula kodi za wafanyabiashara waliojiajiri
Hata uajiriwe na nani, ila kujiajiri ni Bora sanaaa.

Wapo walioacha Kazi za mamilioni wakafungua biashara.

#YNWA
 
Tena uombee uzima na nguvu kila siku. Lakini siku ukiugua ukalala kitandani wiki mbili tu, utaiona tofauti
Mambo yanakaa sawa ila ajira ni risk sana kuliko biashara ila biashara hata ikipata anguko Kuna dalili utaziona mapema
 
Tena uombee uzima na nguvu kila siku. Lakini siku ukiugua ukalala kitandani wiki mbili tu, utaiona tofauti
Sasa ndugu yangu mbona watu wanafukuzwa kazi mara nyingi tu tena kuna watu walitolewa kama wafanyakazi hewa, wengine ofisi zinapunguza wafanyakaz etc

hauko serious we jamaa
 
Kujiajiri hupelekea kila siku unaumiza kichwa na kupata pressure za ajabu ajabu juu ya biashara yako. Ndo maana wengi wao huzeeka mapema.

Hali kadhalika mawazo na hofu juu ya mwenendo na maendeleo ya biashara yako.

Kujiajiri kumesababisha watu wengi sana kuwa wachawi kwa ajili ya kuboresha vipato vyao.

Kujiajiri ni safari ya kupanda na kushuka, na pia haieleweki na hata Maendeleo ya watu wake hayaeleweki pia.
Na kikukweli wengi waliojiri ndio watumwa wa biashara zao.
Na ukifanikiwa unaogopa kuibiwa na kuuwawa.
 
Sasa ndugu yangu mbona watu wanafukuzwa kazi mara nyingi tu tena kuna watu walitolewa kama wafanyakazi hewa, wengine ofisi zinapunguza wafanyakaz etc

hauko serious we jamaa
Ndio uone jinsi kuajiriwa kulivyo kuzuri. Hata wasio na vyeti, wanafoji ili mradi tu waajiriwe. unadhani ni kwa nini mtu asiye na cheti hataki kujiajiri?
 
Kujiajiri hupelekea kila siku unaumiza kichwa na kupata pressure za ajabu ajabu juu ya biashara yako. Ndo maana wengi wao huzeeka mapema.

Hali kadhalika mawazo na hofu juu ya mwenendo na maendeleo ya biashara yako.

Kujiajiri kumesababisha watu wengi sana kuwa wachawi kwa ajili ya kuboresha vipato vyao.

Kujiajiri ni safari ya kupanda na kushuka, na pia haieleweki na hata Maendeleo ya watu wake hayaeleweki pia.
Na kikukweli wengi waliojiri ndio watumwa wa biashara zao.
akili za kijinga kabisa ulitaka wote waajiriwe au ilidhani kujiajili hakuna changa moto tambua kazi kubwa kuliko yote duniani nikuzalisha hela na kuishi kwa kutumia fwaida na kukuza mtaji
 
akili za kijinga kabisa ulitaka wote waajiriwe au ilidhani kujiajili hakuna changa moto tambua kazi kubwa kuliko yote duniani nikuzalisha hela na kuishi kwa kutumia fwaida na kukuza mtaji
Ameweka comparison yake, wala hajasema kila mtu aajiriwe. Hebu soma mtiririko wa post za uzi, utaona ni kwa nini ameandika hivyo. By the way, kwani si kweli kwamba mtu anayejiajiri analazimika kuumiza kichwa chake kuhusu biashara yake?
 
Ukweli ndio huo. Kuna watu wengi sana walifunga biashara hapo katika awamu ya tano, lakini hatujasikia walioacha ajira awamu hiyo. Hiyo inaonyesha kwamba biashara sio kitu kinachotabirika kimapato, upepo mdogo tu unaweza ukakupoteza mjini
Maana yake we ni muoga wa maisha, unatumika miaka 30+ unasubiria mafao

Mwingine akikomaa miaka 30 humkuti kwa lolote
 
Back
Top Bottom