Tuache kudanganyana, Ajira zina afadhali zaidi kuliko kujiajiri, watu wengi waliojiajiri ndio wapo kwenye utumwa

Tuache kudanganyana, Ajira zina afadhali zaidi kuliko kujiajiri, watu wengi waliojiajiri ndio wapo kwenye utumwa

What's the point here?

Kwamba waajiriwa hawapati hii laki 9?

If yes, kama ukiajiriwa unapata laki 9 na ukiuza unapata laki 9 nini point ya kuuza genge?
Point ni kuwa hao anaoona wana maisha mabovu nao wanaingiza hela sawa na yeye aliyeenda shule miaka mingi. .

Yeye kaonyesha kuwa waliojiajiri ni watumwa which is not true. I stand to be corrected but I know what I am saying. .
 
Uongoo, kuna mtu analipa kodi kubwa kama mfanyakazi, tena mfanyabiashara ana chance ya kukwepa kodi.
Wewe unaongea kitu gani? Nina frem Kariakoo unajua nalipa sh ngap kwa mwaka?

Mfanyakazi analipa kodi kubwa kuliko mfanyabiashara? uchumi wetu unabebwa na wafanyabiashara kuliko wafanyakazi. .
 
Muajiriwa anayejisifia anapata 2m per diem akijiandalia tu ziara ya mkoani anakesha kwenye vibanda umiza akibet sh 3500 na 3700
Hv ukitaka ku quote comment ya mtu kutoka kwny uzi mwngne kama hvo unafanyaje?? Natumia browser
 
Aisee, kwa hiyo una mdharau mfanyakazi wako.

Akiondoka akajiajiri nani atakufanyia kazi.

Wakiwa wafanyakazi wengi means shughuli si nyingi pia.
You are not reading between the lines. Do not take it literally. The point is hata waliojiajiri wana wafanyakazi wao. .
 
Hv ukitaka ku quote comment ya mtu kutoka kwny uzi mwngne kama hvo unafanyaje?? Natumia browser
Hapo kwenye maneno report, edit, delete, quote and reply huoni quote?
 
Hizi si ndio running cost zenyewe?!

Kwa gharama za nyumbani aliyeajiriwa halipi?
I am trying to show the responsibilities wanazochukuw waliojiajiri. Which you guys are looking down on. .
 
Acha uongo salary ya 700k Kwa mtu mwenye nidhamu ya pesa anasevu 200k-300k na sio pungufu ya hapo..

Kumbuka Kuna watu wanaishi Kwa salary za 300-400 na wanakomaa.
Hii salary na huko kusave sio kuishi ni kusurvive. Ina maana matumizi yako kwa mwezi ili usave yasizidi 400k. Labda uwe unaishi peke yako hauna familia. Kama una familia ni mwendo wa kujibana sana. Na maana yake ni kwamba kwa mwaka mzima kipato chako ni milioni 8.4.
 
Khahahahah,ama kweli.Tanzania bado tuna safari ndeeeeeeefu sana.

Nini maana ya kuendesha maisha kwa uhuru?.Ukijua kuchanganua hilo,basi utakuwa huru kwa kila jambo lako.ndo maana unaambiwa maisha yako ni siri.

Maana yake uwe huru.Mwajiriwa ni mtumwa kwa mwajiri wake,ndo wanaoongoza kuuwana,kutiliana mikosi,kugombea vyeo,uchawa,umbea,unafiki,na uzandiki.Vimejaa kwao asilimia kubwa.Japo kwenye biashara havikosi,ila miongoni mwa waajiriwa ndo topu.

Wenye akili,anaajiriwa ila bado anafanya biashara.

Mtoa mada,yamkini upo kwa wazazi bado,ila samahani.elimu uliyoipata ikusaidie,na sio uisaidie.

Mfano mzuri,waajiliwa ni wangapi,na waliojiajiri ni wangapi kwa takwimu za haraka haraka.

Bora kuwa mtumwa kwa kitu changu,kuliko cha mtu.maana plani zinakuwa nyingi sana.
 
Najua kwa haraka haraka mtafikiria kunijibu kwamba "Mwajiri hawezi fikia mafanikio ya Mo ai Bakhresa" ....vuta pumzi tulia!! Hao kina Mo watoe akilini mwako maana wapo kundi tofauti kabisa ni wafanyabiashara waliofikia mafanikio ya biashara zao kujiendesha hata wakiwa wamelala.

Mtu mwenye ajira hapa bongo serikalini ana nafuu zaidi maana mwisho wa mwezi mwajiriwa ana uhakika ila aliejiajiri ni juhudi zake, akipoteza mda imekula kwake.

Mwajiriwa hata akifiwa, akiumwa, akioa/kuolewa, anapewa kalikizo.. hapo kila jumamosi na jumapili yupo free, bado ana likizo ya mwezi moja kila mwaka, sherehe za serikali na za dini haendi kazini, Ana muda mwingi wa kuweza kupumzika na familia na kufanya shughuli za kijamii.

Wafanyabiashara wengi nawajua tangu nimepata akili za kuijua dunia mpaka leo hii wao siku ya kupumzika ni christmas tu, wenye nafuu huwa wanapumzika jumapili pekee, siku zingine hizo ni bampa to bampa wanaondoka alfajiri wanarudi usiku, yani hata muda wa kuspend na watoto hawana,

Ukiwa kwenye ajira unaweza kujiajiri pia

Nani mtumwa hapo
images(6).jpg
 
Wapo wengi sana... Messi na Christiano Ronaldo wameajiriwa... Hao ni Masikini?
Hata huku akina Chama na Mayele wana pesa, ila huwezi kuwaita matajiri mbele ya kina Mo, GSM, Bakhressa, Rostam na wengine wengi. Ni kama huyo Messi na Ronaldo huwezi kuwaweka meza moja na kina Elon, Jeff Bezos, Bill Gates na wengine wengi
 
Hao wanatumia vipaji vyao ni kma Jay z au diamond mkuu ....usifananishe kipaji na taaluma....unalinganisha mshahara wa daktari bingwa au lectures na salary ya mbwana samatta
Unakwepa Swali.

Mesi na Ronaldo wamejiajiri au wameajiriwa?
 
Hata huku akina Chama na Mayele wana pesa, ila huwezi kuwaita matajiri mbele ya kina Mo, GSM, Bakhressa, Rostam na wengine wengi. Ni kama huyo Messi na Ronaldo huwezi kuwaweka meza moja na kina Elon, Jeff Bezos, Bill Gates na wengine wengi
Unaleta hoja mpya.

Hoja inayozungumzwa hapa ilikuwa kwamba hakuna mtu Tajiri aliyeajiriwa....Yaani huwezi kuwa tajiri kwa kuajiriwa.

Nimetoa mfano wa waajiriwa Mesi na Ronaldo... Sasa swali langu ni jepesi sana, Messi na Ronaldo (ambao ni waajiriwa) ni matajiri au ni masikini?
 
Kati ya watu wasio na furaha ni walioajiriwa,hakuna siku mshahara umetosha, masimango huko kazini, fitina na wafanyakazi wenzako, ajira huisha ghafla hata kama ni mkataba wa miaka mitano kazi ikiisha unapewa mshahara wa mwezi mmoja tuu kama wa notice, baada ya hapo utaishije..?
Kwamba walio na furaha ni waliojiajiri kufundisha twisheni au ?
 
Maisha ya kweli katika Dunia hii ni kujiajiri kuajiriwa ni uchuro, hua nikisikia mimi ni mfanyakazi wa nyoko nyoko yaani nakuona bwege tu, mwanaume unaajiriwa na unajisifu umeajiriwa huu ni undezi na utumwa wa fikra. Unawezaje kusifia utumwa wa kuajiriwa.
 
Back
Top Bottom