Blood of Jesus
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 4,486
- 8,098
Hata aliyejiajiri hupangiwa kipato na soko.
YESU NI MWOKOZI
YESU NI MWOKOZI
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna jibu nilikuwa nalitafuta point 👇Unajua mzigo wa PAYEE?
Mfanyakazi anaukwepaje?
Hiyo frame si ni moja ya mtaji pia?
Anyways, hiyo gharama ya frame unalinganisha na mshahara/makato na mfanyakazi Wa level gani?
Bila wafanyakazi kulipwa mzunguko Wa fedha mtaani huwa ukoje?
Kiufupi tunategemeana.
Hizi argument sio mara ya kwanza we are getting out of the point. Ila wewe ukiwaza mfanyabiashara unawaza machinga kwa sababu sio walipa kodi. Ila kodi nyingi sana zinatuhusu wafanyabiashara. .Kutokana na mada hii, nilitaka kusema "bila shaka mtoa mada ni mtumishi/muajiriwa" na kwa bahati nzuri kuna mstari ndani ya chapisho unathibitisha hivyo.
Nilitaka kusema hivyo kutokana na ufahamu mdogo niliouona wa mtoa mada juu ya kodi. Anachokijua yeye kuhusu kodi ni VAT na PAYE tu na kwa maana hiyo anahisi wenaobeba mzigo mkubwa kuhusu kodi ni wafanyakazi na hawalalamiki kama wafanyabiashara.
Lakini kwa faida ya mtoa mada ni kwamba "biashara" ndo msingi wa kodi zote, bali kuna aina nyingi za kodi na tozo zinazotokana na biashara zinazolipwa na wafanyabiashara.
Kuwatazama wafanyabiashara kama "mawakala" wa serikali wa kukusanya kodi ya VAT inayolipwa na mlaji wa mwisho si sahihi. Nasema mtazamo huu si sahihi kwasababu kodi hii haimhusu mlaji wa mwisho tu bali pia mchuuzi (mfanyabiashara) kwakuwa na wao hununua bidhaaa au huduma wanazojihusisha nazo kwani maana ya biashara ni kuuza na kununua.
Baadhi ya kodi na tozo zinazowahusu wafanyabjashara ni kama ifuatavyo.
1. VAT
2. Corporate tax
3. Withholding tax
4. Railway development tax (RDL)
5. Import/export duty
6. Leseni za biashara
7. Tozo za kimamlaka kama vile PVOC, import permit, product registration kutoka TBS, TMDA, GCLA, FIre, OSHA, NEMC n.k kutegemea aina ya biashara husika
8. Tozo za leseni za biashara za halmashauri n.k
9. Tozo za usajili wa mtoa huduma/msambazaji kutoka GPSA n.k
Kwahiyo ili kujua ni nani mlipa kodi mkubwa kati ya wafanyabiashara na wafanyakazi inatakiwa kwanza viwango na aina ya kodi zinazowahusu na kabla kuhitimisha.
Ishu ni kipato, we unaejiajiri leo hii uanze mtaji wa laki 3 kuuza pweza vs mbunge baada ya miaka 5 huwezi kumfikia hata ugale galekotekote kuzuri tu kama umekaa pazuri.
Sasa kama umeajiliwa na kazi unaijua na mshahara wako kwa mwezi ni 15m net au zaidi unashida gani zaidi ya kuenjoy.
Kama umejiajili na una kipato cha 15mil na zaidi kimesimama shida nini.. hapo ni kipato tu.
Mtu aliejiajiri mwenye turnover ya zaidi ya 20M kila mwezi huyo huenda akawa anatengeneza more stake than waajiriwa wapya wengi.Inategemea umeajiriwa wapi au umejiajiri kwenye nini na kwa level gani, chukua graduate wa mwaka mmoja watano waliojiajiri na watano walio ajiriwa kisha linganisha maisha yao utapata jibu
Nikasema na wewe ushaanz dharau wafanyabiashara ukawaita watumwa 😀😀😀Im a hustler bab
Gazeti la 2019
Kwa hiyo kumbe tunajadili kuajiriwa vs kujiajiri kwa mwaka gani?Gazeti la 2019
Vizuri.Kuna kazi nyingine ni bora ujiajiri tu chukulia mtu analipwa 150,000 kwa mwezi huyu ni heri ajiajiri tu kwa sababu akikaza kwenye biashara yake anaweza kupata kipato zaid ya hicho kwa mwezi.
Nb:
Kujiari na kuajiriwa vyote muhimu inategemea mtu binafsi wapi anaona ana nafasi ya kuwa na kipato cha uwakika.
Biashara zinazofungwa nyingi ni hizi ndogo ndogo maduka ya rejareja mtaani hizi biashara zilizopo sehemu za mjini miaka yote zipo tu na zinazidi kukuwa
So Mwalimu nyerere, ma engeneer kama mfugale madaktari kama Dr. Masawe ambao wote walikua waajiriwa hawajaacha alama yoyote?
Ukilima na trekta linaacha alama at that level. Lakini uhalisia mwenye kuacha alama ni mwenye kulitumia kwa matashi yake. Mfugale ni kama trekta in this case. Sidhani alikuwa na ndoto ya kujennga daraja tofauti na kutimiza agizo.So Mwalimu nyerere, ma engeneer kama mfugale madaktari kama Dr. Masawe ambao wote walikua waajiriwa hawajaacha alama yoyo
Ligi za kukosoa vitu vidogo kama hivyo ambapo anaekosoa hata yeye ameelewa ujumbe uliokusudiwa hata me naona ni ligi za kitoto sana na kujikuta ujuaji sana.Kweli ccm hamnazo ss hapo usichokielewa nn au mpaka uandaliwe ubao ufundishwe
Najua kwa haraka haraka mtafikiria kunijibu kwamba "Mwajiri hawezi fikia mafanikio ya Mo ai Bakhresa" ....vuta pumzi tulia!! Hao kina Mo watoe akilini mwako maana wapo kundi tofauti kabisa ni wafanyabiashara waliofikia mafanikio ya biashara zao kujiendesha hata wakiwa wamelala.
Mtu mwenye ajira hapa bongo serikalini ana nafuu zaidi maana mwisho wa mwezi mwajiriwa ana uhakika ila aliejiajiri ni juhudi zake, akipoteza mda imekula kwake.
Mwajiriwa hata akifiwa, akiumwa, akioa/kuolewa, anapewa kalikizo.. hapo kila jumamosi na jumapili yupo free, bado ana likizo ya mwezi moja kila mwaka, sherehe za serikali na za dini haendi kazini, Ana muda mwingi wa kuweza kupumzika na familia na kufanya shughuli za kijamii.
Wafanyabiashara wengi nawajua tangu nimepata akili za kuijua dunia mpaka leo hii wao siku ya kupumzika ni christmas tu, wenye nafuu huwa wanapumzika jumapili pekee, siku zingine hizo ni bampa to bampa wanaondoka alfajiri wanarudi usiku, yani hata muda wa kuspend na watoto hawana,
Ukiwa kwenye ajira unaweza kujiajiri pia
Nani mtumwa hapo
Kwann amefeli mkuu mbona mm namuunga mkonoWe jamaa hapa umefeli vibaya sana