Tuache kudanganyana hakuna gesi iliyowahi kuuzwa na kusafirishwa kwa bomba kwenda nje ya Tanzania

Mkuu Meneja Wa Makampuni,
asante sana kwa uzi huu elimishi
Ubarikiwe sana,
Karibu na pande hizi!.
P
 

Bi dada uko vizuri sana!
 

You must be working in an O&G industry for sure ! Na kemia ndio discipline yako ! Hongera sana
 
Meneja shikamoo,Boss anuniwi!
 
Shukrani.
Hiyo gesi inayotumika kuzalisha umeme Dar es Salaam ni gesi ipi na imefikishwaje Dar?
Hiyo gesi inayotumika kufua umeme Kinyerezi Dar es Salaam ni gesi asilia pia inayozalishwa katika vitalu vya Songo Songo na Mnazi Bay.

Kitalu cha Mnazi Bay kinasimamiwa na kampuni inaitwa PanAfrican Energy Tanzania Ltd lakini pana ubia makampuni mengine.

Na kitalu cha Mnazi Bay kinamilikiwa na Maurel & Prom (hisa 48.06%), TPDC (hisa 20%) na Wentworth Resources PLC (hisa 31.94%). Hivi vitalu viwili viligunduliwa zamani kidogo na gesi yake inapatikana kwenye maji ya kina kifupi na nyingine nchi kavu kabisa.

Lakini gesi inayozungumziwa kuwa itabadilisha uchumi wa Tanzania ni ile iliyogunduliwa kwenye maji ya kina kirefu katika kitalu cha Block 2 Offshore Field. Hiyo ndio gesi nyingi ambayo haiwezi kuzalishwa bila uwepo wa kiwanda cha kuibadilisha hiyo gesi nyingi kuwa kimiminika (LNG) ili isafirishwe kuuzwa nje ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…