Tuache kudanganyana hakuna gesi iliyowahi kuuzwa na kusafirishwa kwa bomba kwenda nje ya Tanzania

Tuache kudanganyana hakuna gesi iliyowahi kuuzwa na kusafirishwa kwa bomba kwenda nje ya Tanzania

Unapo zungumzia gesi ni tofauti sana na mafuta katika swala zima la uhifadhi na usafirishaji.

Gesi ya Mtwara bado ipo zaidi itaanza kuzalishwa mpaka LNG plant itakapokua imejengwa.

Hii inayozalishwa sasa ni kiasi kidogo tu.

Karibuni kwa maswali sasa
Kwa ushauri kuhusu maswala ya gesi na mafuta pia karibuni.

Lakini pia kwa uhitaji wa kuandikiwa propozo za kuanzisha miradi ya vituo vya mafuta na kudizani ramani za vituo vya mafuta vidogo kwa vikubwa karibuni pia.

Mawasiliano: +255747744895
Mkuu Meneja Wa Makampuni,
asante sana kwa uzi huu elimishi
Ubarikiwe sana,
Karibu na pande hizi!.
P
 
Inaitwa gesi asilia (Natural Gas).

Mtwara tuna aina moja ya gesi asilia yenye kiwango kikubwa cha kampaundi ya methane. LNG sio aina ya gesi. Kwanza tambua kwamba LNG kirefu chake ni Liquefied Natural Gas (Gesi asilia iliyo badilishwa kuwa kimiminika).

Tambua kwamba ni gesi iliyobadilishwa kuwa kimiminika ili iwe rahisi kuifadhi na kuisafirisha kwa wingi katika umbali mrefu sana sana nje ya nchi. Ukiibadilisha gesi kuwa kimiminika ndipo unaweza kuisafirisha kwa wingi zaidi. Kipimo kimoja cha gesi asilia kinakua mara 600 ikiwa katika hali ya kimiminika.

Bado LNG haijaanza kuzalishwa Mtwara. Ili kuizalisha LNG kinatakiwa kijengwe kiwanda kinacho gharimu Trillion 70 Tsh.

Hivyo kazi kubwa ya kiwanda hicho itakua ni kuibadilisha gesi asilia kuwa LNG.

CNG kirefu chake ni compressed natural gas yaani gesi asilia iliyo kandamizwa au shindiliwa. Nayo bado ni gesi asilia ila yenyewe imeshindiliwa kwa kutumia mashine ili itumike kwenye magari.

LNG na CNG zote ni gesi asilia na zote zina kampaundi ya methane. Isipokua LNG ipo katika katika mfumo wa kimiminika na CNG katika muundo wa kukandamizwa. Lengo kuu ni kuweza kuifadhi na kusafirisha.

Bi dada uko vizuri sana!
 
Ila naomba tena usichanganye LNG na LPG.
LPG ni liquefied petroleum gas na imeundwa kwa kampaundi za propane na butane.
LPG huwa inazalishwa wakati wa kuchakata mafuta ghafi (crude oil) au wakati wa kuchakata gesi asilia yenye kiwango kikubwa cha butane na propane.
LPG haipo Tanzania, huagizwa kutoka nje ya nchi. LPG ndio gesi tunayotumia kupikia majumbani (Oryx, Mihani, Taifa n.k).

Ili kupata LPG tunazikandamiza butane na propane katika mgandamizo mdogo tu (low pressure). Baada ya hapo butane na, propane zinakua kimiminika.

Ili kupata CNG tunaikandamiza gesi asilia (methane) katika pressure kubwa.

Ili kuipata LNG tunaipoza gesi asilia (methane) katika joto la (-163 °C)

You must be working in an O&G industry for sure ! Na kemia ndio discipline yako ! Hongera sana
 
Ila naomba tena usichanganye LNG na LPG.
LPG ni liquefied petroleum gas na imeundwa kwa kampaundi za propane na butane.
LPG huwa inazalishwa wakati wa kuchakata mafuta ghafi (crude oil) au wakati wa kuchakata gesi asilia yenye kiwango kikubwa cha butane na propane.
LPG haipo Tanzania, huagizwa kutoka nje ya nchi. LPG ndio gesi tunayotumia kupikia majumbani (Oryx, Mihani, Taifa n.k).

Ili kupata LPG tunazikandamiza butane na propane katika mgandamizo mdogo tu (low pressure). Baada ya hapo butane na, propane zinakua kimiminika.

Ili kupata CNG tunaikandamiza gesi asilia (methane) katika pressure kubwa.

Ili kuipata LNG tunaipoza gesi asilia (methane) katika joto la (-163 °C)
Meneja shikamoo,Boss anuniwi!
 
Shukrani.
Hiyo gesi inayotumika kuzalisha umeme Dar es Salaam ni gesi ipi na imefikishwaje Dar?
Hiyo gesi inayotumika kufua umeme Kinyerezi Dar es Salaam ni gesi asilia pia inayozalishwa katika vitalu vya Songo Songo na Mnazi Bay.

Kitalu cha Mnazi Bay kinasimamiwa na kampuni inaitwa PanAfrican Energy Tanzania Ltd lakini pana ubia makampuni mengine.

Na kitalu cha Mnazi Bay kinamilikiwa na Maurel & Prom (hisa 48.06%), TPDC (hisa 20%) na Wentworth Resources PLC (hisa 31.94%). Hivi vitalu viwili viligunduliwa zamani kidogo na gesi yake inapatikana kwenye maji ya kina kifupi na nyingine nchi kavu kabisa.

Lakini gesi inayozungumziwa kuwa itabadilisha uchumi wa Tanzania ni ile iliyogunduliwa kwenye maji ya kina kirefu katika kitalu cha Block 2 Offshore Field. Hiyo ndio gesi nyingi ambayo haiwezi kuzalishwa bila uwepo wa kiwanda cha kuibadilisha hiyo gesi nyingi kuwa kimiminika (LNG) ili isafirishwe kuuzwa nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom