Tuache kufarijiana; Umasikini ni Laana, tuupige Vita

Ombi la kura ndugu katika andiko langu SoC 2022 - Bima ya Afya ya Jamii
 
Wapi jina limetajwa Nguvu ya jina ni elimu pana sio kama unavyodhani
 
 
Laana ya Umasikini au mafanikio ya mtu yeyeto asili yake ni yafuatayo.
1.Nguvu ya jina lake
Emu pitia hapo

Tuchukulie mfano Jina la Adamu kwa kua alilaaniwa na MUNGU basi woote wanaoitwa Adamu wameshalaaniwa

Usichange MwanaDamu na jina la Adamu
 
Dhulma sio chanzo cha umasikini na kumjua na kumcha Mungu sio njia ya kupambana na umasikini..kama ulivosema tuambiane ukweli japo mchungu,Kuna matajiri wengi sana ambao vyanzo vyao vya utajiri ni kudhulumu na wala hawamjui Mungu kwa namna yoyote lakini wanaishi duniani kama wako peponi

Moja kati ya dhana ambazo ukitaka kuzifanya kua ngumu ni kuhusisha utajiri/umasikini wa mali na Mungu hapo utakua unaleta unafiki tu binafsi matajiri wengi niliowahi kua karibu nao na kuwafwatilia ni makatiri kishenzi na hawamjui Mungu lakini ndio wanazidi kutajirika kila siku.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Huwa nina shangaa sana mtu au nchi ikichukulia umasikini ni sifa, hii ni hatari sana.
 
Umasikini ni laana, kwann uwe masikini wakati fursa tele zimekuzunguka.
Ndio maana nakwambia kua masikini ni maamuzi na uchaguzi wa mtu binafsi yeye amechagua kua masikini ila sio laana

Sijui unanielewa vizuri lakini?
 
Ndio maana nakwambia kua masikini ni maamuzi na uchaguzi wa mtu binafsi yeye amechagua kua masikini ila sio laana

Sijui unanielewa vizuri lakini?
Umasikini ni ukosefu wa maarifa au mbinu za kuchukua pesa kwa njia za kihalali toka kwa watu wengine. Huna maarifa thus unakuwa masikini. Ufunguo wa maarifa anao Mungu mwenyewe nani ampe kwa wakati wake
 
Umasikini ni ukosefu wa maarifa au mbinu za kuchukua pesa kwa njia za kihalali toka kwa watu wengine. Huna maarifa thus unakuwa masikini. Ufunguo wa maarifa anao Mungu mwenyewe nani ampe kwa wakati wake
Nikuulize swali jepesi sana kwa mfano mwepesi sana

Kwa mfano

Wewe upo sehemu fulani na kwenye sehemu hio unaambiwa bwana Kalunyq hapa ukichimba chini utaokota mawe na hayo mawe bwana ukienda kuuza na kuyabadirisha kua pesa/fedha unauaga umasiki...

Maamuzi au machaguzi ya kwenda au kutokwenda kuchimba hayo mawe unayafanya wewe km wewe au anayafanya MUNGU?

Ufunguo anao nani hapo?

Umeshapewa tayari uchague uchukue au uache.
 
Uamuzi wa kuwa masikini au kuwa tajiri ni mtu binafsi ndie uamua.
Kupewa ufunguo wa maarifa na Mungu ni kitu kingine na uamuzi wa kuufungua mlango ni kitu kingine.
 
Asante kwa kutoa muda wako ku share nasi kile ulicho nacho kwa manufaa ya wengi watakao soma hapa.

Lakini ndugu mleta mada reference ya mada yako ni maandiko ya biblia ambayo kwa kiasi kikubwa wameandikiwa wayahudi, sisi ambao sio wayahudi au ambao hawatumii biblia au ambao hawaamini katika ibrahimic religion mada hii inawahusu?
 
Uamuzi wa kuwa masikini au kuwa tajiri ni mtu binafsi ndie uamua.
Kupewa ufunguo wa maarifa na Mungu ni kitu kingine na uamuzi wa kuufungua mlango ni kitu kingine.
Kwa kusema hivyo basi unakubari na mimi kwamba umasikini sio laana bali tu ni maamuzi ya mtu binafsi

Vizuri sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…