Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

Uchaguzi 2020 Tuache kutetea Ujinga: Kubadili maneno ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama siyo sahihi

Kamanda hongera kwa kukemea huu ujinga

Asante
Linapokuja suala la Taifa na tunu zake pamoja na alama zake, lazima tusimame wote kama Watanzania kuzilinda na kuzitetea bila kujali vyama vyetu.

Walichokifanya CHADEMA siyo sawa!
Wanaweza kutengeneza wimbo wao wa chama wakawa nao lakini siyo kuchukua wimbo wetu wa Taifa na kuufanyia distortion.

Ule wimbo ni Dua kwa Taifa zima, haifai kuuchezeachezea!
 
Inawezekana ukawa na hoja za msingi, lakini kwangu naona ni kosa kurekodi na kusambaza, na sio hiyo remix kwenye mkutano wa Cdm.

Hata live band huwa tunaona wakiimba nyimbo mbalimbali za wengine na kuweka vikolombwezo, lakini kosa ni kurekodi na kusambaza.

Kilichokuibua ni hicho kitisho cha huyo msajili wa vyama vya siasa. Huyo msajili ni mara ngapi anakalia kimya mambo hayo hayo yakifanywa na ccm?

Kuna siku Magufuli alipokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha, kumbuka jeshi limetengwa kabisa kikatiba na siasa.

Je msajili alikemea hilo, je ww ulikemea jambo lile? Au huu wimbo wa taifa ndio umeona wa maana sana mpaka kuuanzishia uzi?
 
Hata mimi napinga ila ni vizuri kuwe na mizania sawa kwenye hayo makatazo.
View attachment 1527227

Hii nji tunaongozwa na vichaa na majuha....! Kosa Hilo Hilo AKIFANYA CCM IS OK, LAKINI AKIFANYA CHADEMA NI UHAINI....!!
Double standards za kijinga kabisa!!!
Hapa Hakuna kosa kwa CCM Wala CHADEMA.....!!
Jaji Mtungi acha kutumika Kama Tissue za chooni please. Kuongeza maneno/tune ya mwimbo wa Taifa ni kama KIBWAGIZO tu cha kushereheka/kufurahia mkutano/kikao!! Hakuna DHAMBI au jinai yoyote hapo. WIMBO WA TAIFA UNAJULIKANA KWA MANENO, SAUTI NA BETI ZAKE....!!!!
KUIMBA KWA KUONGEZA/BADILISHA MANENO HAKUBADILI WIMBO WA TAIFA....!!!
CCM, MSAJILI, MAGUFULI NA POLISI ACHENI UTOTO!!!
 
Magufuli alipopokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi ulikuwa hujazaliwa? Mbona hukukemea ili tuone huwa unachukizwa na mambo yaliyo nje ya katiba?

Maadamu tu ni MWAKA WA UCHAGUZI MKUU...... Tutasikia vihoja na viroja vingi Sana.....!!Just stay Tuned....!!!Yajayo yanachukiza na kuudhi kupita maelezo!!!
 
Zitto ana busara zaidi kuliko chadema nzima
 
Inawezekana ukawa na hoja za msingi, lakini kwangu naona ni kosa kurekodi na kusambaza, na sio hiyo remix kwenye mkutano wa Cdm. Hata live band huwa tunaona wakiimba nyimbo mbalimbali za wengine na kuweka vikolombwezo, lakini kosa ni kurekodi na kusambaza. Kilichokuibua ni hicho kitisho cha huyo msajili wa vyama vya siasa. Huyo msajili ni mara ngapi anakalia kimya mambo hayo hayo yakifanywa na ccm? Kuna siku Magufuli alipokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha, kumbuka jeshi limetengwa kabisa kikatiba na siasa. Je msajili alikemea hilo, je ww ulikemea jambo lile? Au huu wimbo wa taifa ndio umeona wa maana sana mpaka kuuanzishia uzi?

kuna mambo yafuatayo

1. Si sahihi Wapinzani kufanya ya hovyo eti. kwa kuwa CCM huwa wanafanya ya hovyo

2. wapinzani ili waheshimike na wakubalike kwa wananchi inabidi wawe humble zaidi, wafanye vitu ambavyo ni modest ili kuvutia umma usiwaone watu wasiofuata taratibu na kuheshimu tunu ambazo tumeshazipokea kuwa ni tunu au alama za taifa.
CCM wanaweza kufanya upuuzi, na wakaweza kujiclear easily kwa sababu wana dola, wana all bullying pulpits za kuweza kutwist matendo yao na kushape public opinion in their favor. Wapinzani hawana hiyo luxury ndiyo maana inabidi wawe exemplary.

3. Makosa mawili hayafanyi kosa moja lisiwe kosa

4. Haifai wapinzani kuwapa CCM ammunition ya kuwaondolea credibility mbele ya wananchi. Matendo kama haya yaweka ukuta baina ya wananchi wazalendo kwa taifa lao ambao wamekua toka nursery school wakiimba wimbo wa Taifa kwa heshima zote. Leo ukireplace Tanzania ukaweka Chadema, wananchi hawa hawawezi kuwa comfortable

5. Ni makosa sana kubase argument za "mbona na CCM. hivi, au mbona CCM vile", hizo hazisaidii wapinzani. Ni tofauti sana vijana wa Temeke wasio na uongozi katika chama chochote cha siasa kufanya jambo fulani baya na Baraza kuu la Chadema kufanya jambo hilohilo tofauti yake ni mbingu na ardhi!
 
Chadema na wafuasi wao umefika wakati wa kutoambilika na kutukana yeyote atayeleta usemi wasioutaka. Kwa anayekumbuka ilivyokuwa miezi kama hii mwaka 2015 ataelewa nini namaanisha.

Chadema sasa hivi hakuna mwenye busara wa kuwaambia wenzake hili hapana. Rejea kilichompata Sugu siku ile ya mwisho kuaga mwili pale taifa. Alijaribu kutumia busara kidogo ila walioshika hatamu za chama wakamnyamazisha na kudai ukurasa wake umedukuliwa!

Viongozi wakuu wa chama wanaona sawa kuuimba wimbo wa taifa kwa namna watakayo wao! Sasa hapo unatarajia nini kutoka kwa nyumbu waliozagaa mitaandaoni humu ambao wengine kazi yao kubwa ni hiyo ya ushabiki! Unategemea makamanda waseme Tundu Lissu kakosea! Hiyo bado sana kutokea. Siyo leo wala kesho.

Tarajia utulivu kurejea mara tu baada ya uchaguzi Oktoba kama ilivyokuwa mwaka 2015. Baada ya hapo itakuwa ni visingizio: mara tume, mara polisi, mara busara, ilimradi kujifariji na kusubiri 2025.
 
Hii video uliyoweka, hawa wanaoimba wana nafasi gani ndani ya CCM, Je kitendo chao kilikuwa endorsed na CCM, au ni rogue elements tu zimeamua kuimba?

Anyway,. makosa mawili hayafanyi kosa lisiwe kosa.

hebu linganisha kosa lifanywe na Baraza kuu zima la Chadema, Mwenyekiti akiwepo, katibu mkuu yupo na mgombea uraisi yupo nao wanashiriki kudistort wimbo wa Taifa.

Yaani Baraza kuu zima la Chadema, mbele ya mwenyekiti, na katibu mkuu wake pamoja na wajumbe wanashiriki kudistort wimbo wa Taifa

Hizi video mbili hazilingani aisee!
Hukuona Magu alipost iyo nyimbo kwenye official page yake??? Nakuwa na mashaka sana na consciousness yako ndugu. Unanipa wakati mgumu
 
Back
Top Bottom