Tuache kuweka shida zetu kama ngao ya kuzuia Katiba mpya. Maisha tuliyopitia miaka 6 sidhani kama tupo tayari kupitia tena

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,588
Reaction score
11,668
Nanukuu

Askofu Dkt. Benson Bagonza anasema.
"Hoja ya katiba mpya pamoja na sababu nyingine nyingi, inalenga kupunguza au kuondoa mgongano wa hatari kati ya ukuu wa katiba na ukuu wa Rais. Kwa hali ilivyo, Rais na katiba wako vitani"

CCM wasitudanganye. Wao ndio walioanzisha mchakato wa katiba kwa gharama kubwa wakati watu walijitahidi elimu afya na maji pia. Walipoona wananchi walitaka katiba tofauti na matakwa yao kwanza walivuruga mchakato kwa bunge la katiba CCM tu kisha wakazika.

Kuna WanaCCM Wanapinga Hoja Ya Katiba Mpya Kwa Kisingizio Kwamba Kwenye Ilani Yao Ya 2020 Hawakuahidi Katiba Mpya, Tujiulize Mbona kwenye Ilani Ya 2010 Hawakuahidi Katiba Mpya Lakini Walianza Mchakato 2012? Pili Ilani Yao Ya 2015 Mbona Hawakuahidi Kununua Ndege Lakini Walinunua?

Kenya wamebadili katiba na mpaka sasa wametuzidi mbali sana hata chanjo ya mbwa tunaagiza kwao.

Hatuhitaji KATIBA mpya kwaajili ya kumaliza matatizo yetu Bali tunahitaji kwa nchi kurudi mikononi mwetu wananchi. Hatutaki mambo yale yajirudie tena.

Moja Kati ya ulemavu wa akili uliowazi kabisa ni kudhani kwamba wote wanaodai katiba mpya ni wahuni fulani wa chadema. Huu ni ujinga wa kiwango Cha juu kabisa unaopaswa kupuuzwa kwa nguvu zote na kila aliye na akili timamu.

Pengine CCM wanaogopa katiba mpya, kuhofia kupoteza Dola, Sisi Tuandike katiba mpya nyie Muendelee kutawala hakuna shida kabisa.
 
Hakuna anaesema hataki katiba mpya.

Wapo tunaosema hatuhitaji katiba mpya kwa haraka hii ya chadema hii dharura ya Chadema ndo tunao ipinga..

Otherwise katiba mpya tunaitaka.

How tutaipata na mchakato wa aina gani ni subject to discussions.
 
Kwa Amani na utulivu..
Sio kwa heri au Shari
Hii hali ya Rais wetu kuwa ndie KATIBA. Hawajajifunza lolote kutokana na tuliyoyashuhudia miaka mitano iliyopita?

Amani na Utulivu unaweza kuupata kwa mtawala?
 
pengine labda tuwatishe mtemi jiwe ana Fufuka kesho ndio wataona uharaka na uhitaji wa Katiba Mpya!
 
Hii hali ya Rais wetu kuwa ndie KATIBA. Hawajajifunza lolote kutokana na tuliyoyashuhudia miaka mitano iliyopita?

Amani na Utulivu unaweza kuupata kwa mtawala?

Haihalalishi kumharakisha ndani ya miezi mitatu tu
 
Hakuna anaesema hataki katiba mpya.

Wapo tunaosema hatuhitaji katiba mpya kwa haraka hii ya chadema hii dharura ya Chadema ndo tunao ipinga.
Swala la katiba linataka kutumiwa kama kichochoro cha viongozi wa chadema kupiga hela kupitia vikao vya katiba. Hili linajulikana na wenye akili washaanza kuwapuuza. Kumbuka walijifanya kususia ruzuku huku chama kikiwa mahututi kifedha.

Sasa wana force ili mama akubali, waanze vikao, wapige mamilioni ya shilingi ili wapate hela za kuwalipa kina Mmawia na hawa wanaoandika andika habari za katiba akiwepo mleta mada.
 
Wakati wa Mwendazake chadema walisema watafanya bure bila hata shilingi moja.
 
Ni miaka 30 sasa ya mfumo wa vyama vingi. Maccm yametumia uhuni na janja janja kwa miaka 30 ili kuikwepa Katiba mpya.

Chadema wamemuandikia barua mama ya kuomba kukutana naye kujadili mambo mbali mbali ikiwemo mchakato wa rasimu ya Tume ya Warioba ili kupata Katiba mpya.

Samia kwanini anakwepa kuijibu Chadema iwe kwa barua au hadharani kuhusu ombi la Chadema la kutaka kukutana naye!?

Hakuna anaesema hataki katiba mpya.

Wapo tunaosema hatuhitaji katiba mpya kwa haraka hii ya chadema hii dharura ya Chadema ndo tunao ipinga...
 
Wakati wa Mwendazake chadema walisema watafanya bure bila hata shilingi moja.
Chadema hii iliyotafuna mamilioni ya Sabodo aliyokipa chama ili kijenge ofisi zake, na kuchimba visima vya kuwasaidia wananchi? Au chadema ipi ambayo ingefanya vikao vya bure?
 
Constitution is so important because outlines the limits on the power of the Government and tells us about the rights of the citizens.
 
Ni miaka 30 sasa ya mfumo wa vyama vingi. Maccm yametumia uhuni na janja janja kwa miaka 30 ili kuikwepa Katiba m.

Chadema wamemuandikia barua mama ya kuomba kukutana naye kujadili mambo mbali mbali ikiwemo mchakato wa rasimu ya Tume ya Warioba ili kupata Katiba mpya.

Samia kwanini anakwepa kuijibu Chadema iwe kwa barua au hadharani kuhusu ombi la Chadema la kutaka kukutana naye!?
[emoji91]
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ni miaka 30 sasa ya mfumo wa vyama vingi. Maccm yametumia uhuni na janja janja kwa miaka 30 ili kuikwepa Katiba mpya.

Chadema wamemuandikia barua mama ya kuomba kukutana naye kujadili mambo mbali mbali ikiwemo mchakato wa rasimu ya Tume ya Warioba ili kupata Katiba mpya.

Samia kwanini anakwepa kuijibu Chadema iwe kwa barua au hadharani kuhusu ombi la Chadema la kutaka kukutana naye!?
Kudhani eti kwa kuwa na katiba mpya huduma za kijamii Kama maji, Elimu, huduma za afya, barabara n.k havitapatikana, ni matumizi mabaya ya akili. Kama tangu mwaka 1977 huduma hizo hazijapatikana kwa katiba hii, ni muujiza kudhani zitapatikana kwa katiba hii.
 
Ahsante sana Mkuu🙏🏾 una akili kubwa sana.

Kudhani eti kwa kuwa na katiba mpya huduma za kijamii Kama maji, Elimu, huduma za afya, barabara n.k havitapatikana, ni matumizi mabaya ya akili. Kama tangu mwaka 1977 huduma hizo hazijapatikana kwa katiba hii, ni muujiza kudhani zitapatikana kwa katiba hii.
 
Swala la katiba linataka kutumiwa kama kichochoro cha viongozi wa chadema kupiga hela kupitia vikao vya katiba. Hili linajulikana na wenye akili washaanza kuwapuuza. Kumbuka walijifanya kususia ruzuku huku chama kikiwa mahututi kifedha.

Sasa wana force ili mama akubali, waanze vikao, wapige mamilioni ya shilingi ili wapate hela za kuwalipa kina Mmawia na hawa wanaoandika andika habari za katiba akiwepo mleta mada.
Ati huyu naye alienda shule ?! Elimu yetu ni mbovu kiasi hiki ?! Daahh [emoji87][emoji102]
 
Elimu sio mbovu, isipokuwa vichwa vyenu ndio vibovu kwa kukuruhusu kuwaamini wanasiasa hawa.

images (7).jpeg

images (12).jpeg

images (11).jpeg

images (10).jpeg

images (8).jpeg
 
Back
Top Bottom