Tuache siasa, ajira zipo za kutosha Tanzania kwa wanaojua Kiingereza kwa ufasaha

Kama kiingereza ndo ajira basi Kenya kusingekuwa na unemployed...

Na! Unafikiri kuna mzazi asiyependa mwanae asome kisasa!??

Hela ya kula tu shida....
Sijui kwanini wa bongo wanafikiri kwamba wakenya wote wanajua kiingereza?......zaid ya 65% ya wakenya hawawezi kuzungmza kiingereza wengi wanaishi maisha ya kuungaunga walifaili au wakuenda shule ila wanajifanya ni wasomi,
 
Nilitaka kumwambia hivihivi mtoa mada. Sasa hivi kuna vijana wengi waliosoma shule za English medium tangu primary school na wana degree nzuri tu lakini hawana ajira.

Nafasi za ajira ni chache kuliko wahitimu au walio na sifa
 
Kuna watu kibao wanasoma leo malengo yao wakaajiriwe kwenye idara, vitengo, mashirika na taasisi huko serikalini. Wajue lugha wasijue wao kinacho-matter kwao ni ajira si uwezo wala ufanisi.

Hawataki kisikia cha kujiajiri wala kuajiriwa sekta binafsi!
 
Sijui kwanini wa bongo wanafikiri kwamba wakenya wote wanajua kiingereza?......zaid ya 65% ya wakenya hawawezi kuzungmza kiingereza wengi wanaishi maisha ya kuungaunga walifaili au wakuenda shule ila wanajifanya ni wasomi,
Kiingereza ni kama lugha yoyote. Hata Waingereza wenyewe kinawapa shida. Ni kama sisi na Kiswahili chetu!
 
Nikajua unatuwekea hapa hilo deal la ajira zilipo ili niwatonye machalii wapo weng sana lugha inapanda vzr even Spanish and French. Kumbe huna conn, upande wa lugha za kigeni kujieleza na kuongea kwa ufasaha kuna changamoto kiasi flan.

But umesisitiza ajira zipo ni vzr utuwekee link ya hizo ajira mkuu.
 
Ishu hata siyo kujieleza ishu ni una uzoefu wa kukufanya uitwe kwenye huo usaili ili ujieleze?

NMB wanatangaza nafasi za kazi mpaka wana-readvertise, hawa Access Microfinance na hizi zingine kutwa utaona nafasi ila vigezo vya kukufanya uitwe ukajieleze hauna.

Shida yetu graduates wengi ni uzoefu na connection wala siyo kujieleza kwa kiingereza.
 
Watanganyika hawa wasiojua tofauti ya R na L wala matumizi ya herifu H are doomed to fail. Lugha yao tu hawawezi ndo iwe yai! Mtu kahitimu chuo kabisa anaandika ela, akuna, apana nk. Kifupi hatujui Kiswahili wala kimombo.
Dr. Remmy umongea ukweli kabisa
 
Elimu elimu elimu!

Bado Kuna shida kwenye elimu yetu, wasomi wapo wengi lakini bado hatuendani na matakwa ya ulimwengu huu.

Ulimwengu wa Leo unahitaji watu wanaotumia ubongo wao vizuri sambamba na elimu zao kwa kubuni, kuanzisha miradi , kuchimba na kutafuta ukweli kwenye changamoto zinazotukumba kila siku. Siyo Kama ilivyo sasa kuonesha cheti chenye ufaulu mzuri lakini matendo na mapinduzi ni ziro.
 
Interviews karibia zote za sasa zinaangalia namna applicant anavyo weza ongea 'lugha ya malkia' , hivyo kama hujui ng'eng'e utasugua sana na kutembea na bahasha ya kaki adi upaukee
 
Kwa mtu mwenye akili timamu kujua lugha ya kingereza ni jambo mhimu Sana Wala hakuna ubishi ,pia kwa kijana hata kama kamaliza chuo na kukosea ajira akiamua kutulia na kufanya kazi mtaani na akaachana na anasa ndani ya miaka mitano lazima awe na mtaji wa milion 5,hela ipo lakini vijana stalehe wamaweka mbele .
 
Kingereza sio kiivyo unavyokazia sijui kama unaelewa kazi zinavyofanywa bila connection utaendelea kuwa mwalimu wa kujitegemea kama unajua language
 
Watanganyika hawa wasiojua tofauti ya R na L wala matumizi ya herifu H are doomed to fail. Lugha yao tu hawawezi ndo iwe yai! Mtu kahitimu chuo kabisa anaandika ela, akuna, apana nk. Kifupi hatujui Kiswahili wala kimombo.
Wanasiasa wa ccm ndio lengo lao kuvuruga akili za wananchi ili waendelee kuwatala..huku kuwao wakiupiga mwingi na familia zao.

Huwezi kuwa na lugha mbili za kufundishia katika ngazi tofauti za kieliemu..inshu hapa ni kuchagua moja kama ni kiswahili ama kiingereza iwe kuanzia awali hadi chuo kikuu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kama kiingereza ndo ajira basi Kenya kusingekuwa na unemployed...

Na! Unafikiri kuna mzazi asiyependa mwanae asome kisasa!??

Hela ya kula tu shida....

Kasemea Tanzania, kwa hapa ukijua kiingereza fasaha uwezo wa kupata ajira ni mkubwa. Mimi sithubutu mtoto wangu asome shule inayofundisha kwa kiswahili maana ni kumfubaza.

Ukilogwa mtoto wako akasoma shule ya kiswahili ujue umeliwa.
 
Kingereza sio kiivyo unavyokazia sijui kama unaelewa kazi zinavyofanywa bila connection utaendelea kuwa mwalimu wa kujitegemea kama unajua language

Ukijua kiingereza kwa hapa Tanzania una nafasi kubwa ya kupata fursa kuliko kinyume chake. Habari ndio hiyo ndugu.
 
Uliyoyasema n sahihi kabsa,huwa nachukia sana naposikia mwanasiasa anasema eti kiswahil kimekuwa sana na tunampango wa kukiendeleza sjui nn nn,brah brah kibao
 
Tatizo mnaangalia ajira za ofisini tu ... angalia ajira kwa ujumla sekta tofauti tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…