Tuache siasa, ajira zipo za kutosha Tanzania kwa wanaojua Kiingereza kwa ufasaha

Tuache siasa, ajira zipo za kutosha Tanzania kwa wanaojua Kiingereza kwa ufasaha

Members, Msipende kusikiliza maneno ya sisi wanasiasa kuwa lugha ya Kiswahili ni bora na elimu ya shule za kata ni bora sana.

Hakuna mwana siasa wa zama hizi ambaye mtoto wake anasoma shule ya kata au anasoma masomo ya msingi kwa lugha ya Kiswahili.

Usahili au Interview za sasa anayejua kujieleza kwa Kiingereza kwa ufasaha zaidi ndiye anayepata ajira kwenye Makampuni na mashirika binafsi.

Sekta binafsi zinahitaji watu wanaojua lugha kwa ufasaha ya Kiingereza.

Nilifika ofisi moja hapa Tanzania, hakuna mfanyakazi wa kitanzania anayoongea kiswahili, Wote wanatumia kiingereza fasaha kuanzia mlinzi nje mpaka wahudumu ndani.

Watoto wa watu wenye uwezo na waliosoma shule za kimataifa za kiingereza ndio Wanao kwenda kuongoza sekta zote nchi hii, Na hao watoto wengi ni wabunge, Mawaziri, Wafanyabiashara wakubwa, Wakurugenzi wa taasisi na Mashirika au wale wafanyakazi wa serikali wenye mishahara mikubwa.

Vijana wa sasa wanakosa ajira kwa kushindwa kujieleza kwa Kiingereza fasaha kwenye Usahili wa mahojiano au Oral interview.

Vijana tumieni simu zenu kujiimarisha uwezo wa kuongea Kiingereza Fasaha, Degree bila kuongea Kiingereza kwa ufasaha ajira ni ngumu kupata sekta binafsi na hata taasisi baadhi za Serikali.

Kiingereza cha kufikiria maneno kama oooh, you know sir, Infact Sir. OK no problem..... The... The.... and.... OK you know... know huwezi kupata ajira kwa sasa.

Mtoto wa kihindi Tanzania wa darasa la tano anajieleza vizuri kuliko mwanafunzi wa chuo kikuu.

Mtoto wa chekechea Feza na Class three IST anajieleza kwa ufasaha kuliko mwanafunzi wa chuo kikuu.

Zamani watu walisoma shule za Serikali na waliongea Kiingereza kwa ufasaha lakini sio kwa walimu wa sasa na shule zilizopo sasa.

Shule za Tanzania hasa za serikali na baadhi sekta binafsi walimu wenyewe tu hawajui kiingereza, Je hao wanafunzi watajua Kiingereza?

Jitihada binafsi zinahitajika kwa wahitimu wa sasa kujifunza lugha ya Kiingereza kwa ufasaha.

Kila siku ajira zinatangazwa za Kitaifa na kimataifa, Lakini vijana wetu wanaogopa na hata wakiomba hawawezi kufurukuta na watoto wa nchi jirani za Kenya na Uganda.

Hata sisi wakinga siku hizi familia zetu zinasoma shule za kisasa na vyuo vya kisasa nje ya nchi.

Fuatilieni scholarship vizuri muone watoto wa viongozi wanavyohangaika kuwaombea watoto wao.

Fuatilieni mashirika makubwa ya kimataifa mtawakuta watoto wa viongozi wa kisiasa huko WHO, UNICEF, WORLD BANK, UNESCO, UNHCR, CITI BANK na Bank zote za Kimataifa wapo watoto wao wanaoongea Kiingereza kwa ufasaha.

Ofisi nyingi na Bank kubwa kubwa Dar Salaam hakuna mfanyakazi wa kitanzania anaongea kiswahili ni Kiingereza tu kilichonyooka labda waamue kukuongelesha kwa Kiswahili.

Lini ulisikia watu wenye account Citi Bank, Standard chartered Bank hawajui Kiingereza, kuanzia wateja wa Bank hizo mpaka waajiriwa wanaongea wengi lugha vizuri ya Kiingereza. Hizo Bank ndani watanzania walioajiriwa wanaongea Kiingereza kwa ufasaha kama wazungu, usiyejua Kiingereza hupati kazi sehemu hizo.

Endeleeni kusema elimu ni uelewa wakati ulichokielewa huwezi kukielezea kwa ufasaha kwa lugha ya Kiingereza.
Kuna ukweli fulani
 
Unaandika-"Fuatilieni mashirika makubwa ya kimataifa mtawakuta watoto wa viongozi wa kisiasa huko WHO, UNICEF, WORLD BANK, UNESCO, UNHCR, CITI BANK na Bank zote za Kimataifa wapo watoto wao wanaoongea Kiingereza kwa ufasaha" Hivi hapa kuna jumla ya ajira ngapi kwa mwaka? Sijui kama hata zinazidi 2000.

Acheni uvivu fungueni ajira toka vijijini, kata mpaka mijini. Viwanda vidogo vidogo vina ajira nyingi sana kuliko huko unakokimbilia. Ndani ya Tanzania bado hakujafunguka.

Nitakusaidia kidogo wapi kwenye nafasi za ajira: Eneo la sukari (hapa nchini tu haitoshelezi) - Ajira zaidi ya milioni 1 tumezilalia, Mafuta ya kupikia- Ajira zaidi ya laki 5 zimelala, Eneo la usindikaji (matunda, mbogamboga n.k - ajira zaidi ya milioni 1.5 zimelala .

Endelea kuzitaja ukianzia na uhaba hapo kijijini/mjini kwako. Tena hatuhitaji mashine kubwaaa kivile, Hizi mashine ndogo ndogo zinatosha, zitazowekwa na akina ngosha, wanyalukolo, machinga n.k

Ndugu zangu kuweni huru acheni kutawaliwa na fikra za ukoloni mambo leo, Fikra za akina Lisu and the company.

Tunachohitaji ni kimoja tu: Wabunge waliochaguliwa na wananchi na sio wa VIMEMO.
 
Umeongea ukweli mtupu, Watz wengi Wana degree lakini Kiingereza hakijanyooka.

Tusidanganyane ukienda kwenye oral interview lazima upigwe chini.
 
Kasemea Tanzania, kwa hapa ukijua kiingereza fasaha uwezo wa kupata ajira ni mkubwa. Mimi sithubutu mtoto wangu asome shule inayofundisha kwa kiswahili maana ni kumfubaza. Ukilogwa mtoto wako akasoma shule ya kiswahili ujue umeliwa.
Si kila mtu ana uwezo huo wa kumsomesha mtoto private...

Hakuna asiyependa elimu nzuri kwa mwanae, shida ni uwezo.
 
nashauri zifunguliwe English courses kwaajili ya migraduates ya Tanzania isiyojua kujieleza kwa kiingereza na ikibidi bodi ya mikopo igharamie gharama zote za elimu hiyo maalum

fontfed
you are going to stay inside until Wednesday sawa ndalichako
 
Yote hayo ni ubatili na kujilisha upepo.

Ajira ni hakuna,,,uwe unajua kizungu au hujui kizungu..

Mkuu hao unaowaona wamepata hizo kazi haikuwa rahisi kama unavofikiria,, walipambana sana na wengi walizikosa ilihali kizungu wanakijua.

Kizungu ni Lugha tu
 
Kama kiingereza ndo ajira basi Kenya kusingekuwa na unemployed...

Na! Unafikiri kuna mzazi asiyependa mwanae asome kisasa!??

Hela ya kula tu shida....
Wakenya wanajua kiingereza ??? Toka lini
 
Watanganyika hawa wasiojua tofauti ya R na L wala matumizi ya herifu H are doomed to fail. Lugha yao tu hawawezi ndo iwe yai! Mtu kahitimu chuo kabisa anaandika ela, akuna, apana nk. Kifupi hatujui Kiswahili wala kimombo.
Umeongea kweli kabisa. Kuna mdada mmoja ana masters lakini uandishi wake ndio huo i.e. ela, akuna, apana etc.
 
Yaani nikikutana na Mswahili ambaye hata Kiswahili hawezi, simpi kazi ng'o!

Halafu huwa wanakuwa na madigrii makubwa makubwa lakini haya mambo tuliyofundishwa shule ya msingi hawawezi!

Bora hata ubabaishe Kiingereza. Kiswahili sikuvumilii kabisa.
Watanganyika hawa wasiojua tofauti ya R na L wala matumizi ya herifu H are doomed to fail. Lugha yao tu hawawezi ndo iwe yai! Mtu kahitimu chuo kabisa anaandika ela, akuna, apana nk. Kifupi hatujui Kiswahili wala kimombo.
 
Hivi kitu gani kinakwamisha watoto wasisome kingereza kuanzia vidudu mpaka chuo kikuu Tanzania?
 
Hivi kitu gani kinakwamisha watoto wasisome kingereza kuanzia vidudu mpaka chuo kikuu Tanzania?
Grupu kubwa la watu walioshindwa kwenye kizazi kilichopita hivyo wanaona wivu kubadilisha kizazi kinachokuja Ili nachenyewe kipitie shida kama walizopitia wao za kushindwa kuteka teknologia maana kiingereza kimebeba teknologia ya dunia kwa ukubwa mfano utake kuuza nje vitu vyetu huwezi kuandika kiswahili peke yake ukategemea uteke soko la kimataifa.
 
Pamoja na hilo la lugha, Ila kiukweli watafuta ajira ni wengi kuliko ajira zenyewe.

Miaka yangu 8 mtaani na degree, nimeona mengi Sana. Lugha sawa hatupo vizuri lakini ukweli ulionyooka ni nafasi za ajira ni chache kuliko wahitaji. Usijidanganye kuwa Kila mwenye English nzuri anapata ajira.

Sasa hivi watu wengi mno wanaajiriwa Kwa simu.

Mtu anaulizwa 'kuna nafasi ya kazi kwenye kampuni, je una muda au upo busy'.
Mpaka leo hii bado hakuna ushindani wa soko la ajira.... 😎
 
Back
Top Bottom