Tuache siasa, ajira zipo za kutosha Tanzania kwa wanaojua Kiingereza kwa ufasaha

Yaani nikikutana na Mswahili ambaye hata Kiswahili hawezi, simpi kazi ng'o! Halafu huwa wanakuwa na madigrii makubwa makubwa lakini haya mambo tuliyofundishwa shule ya msingi hawawezi!! Bora hata ubabaishe Kiingereza.

Wengine wanakosea maneno ya kila siku, mtu anaandika Kalibu, ongera maneno ambayo haziwezi pita siku mbili hujayaona yani kusoma hawezi na picha haoni. Mtu asiye makini kiasi hiki nani ampe kazi yake?
 
Hiki kitu mimi huwa kinanishangaza...

Hata kama umesoma kwa kiswahili shule ya msingi, lakini sekondari miaka 6 umesoma kwa kiingereza masomo yote, ukaenda chuoni miaka 4 ukasoma tena kwa kiingereza masomo yote, jumla miaka kumi unasoma kwa kiingereza tu, bado mtu kujieleza kwa hii lugha uliyopatia digrii yako inakuwa ni tabu, ni umbumbumbu gani huu?

Ila na wewe mleta mada sema tu unapigia debe hayo mashule yenu wanayofundisha kizungu tangu chekechea, which I strongly oppose!
 
Wengine wanakosea maneno ya kila siku, mtu anaandika Kalibu, ongera maneno ambayo haziwezi pita siku mbili hujayaona yani kusoma hawezi na picha haoni. Mtu asiye makini kiasi hiki nani ampe kazi yake?
Hizi shule wanazofundisha kizungu tangu shule ya msingi wanatuharibia watoto, siku hizi hawajui kabisa kiswahili, utasikia " nipe ela, atulipi, kila atuwa duwa, abari za hasubui...".
 
Kama kiingereza ndo ajira basi Kenya kusingekuwa na unemployed...

Na! Unafikiri kuna mzazi asiyependa mwanae asome kisasa!??

Hela ya kula tu shida....
Ukweli mchungu,tunaumia tu na kupambana angalau watoto wetu wasije pitia maisha kama yetu
 
Wewe ndiye hujui hata mambo yaliyo wazi. Lugha jifunze ukiwa mdogo. Lugha siyo ya kujifunza ukiwa mkubwa. Halafu unashangaa kwa nini wanaojifunza wakiwa wakubwa hawaongei hata wakijifunza kwa miaka 100. Mbona jibu liko wazi?
 
Watanganyika hawa wasiojua tofauti ya R na L wala matumizi ya herufu H are doomed to fail. Lugha yao tu hawawezi ndio iwe yai! Mtu kahitimu chuo kabisa anaandika ela, akuna, apana, ongera, Kalibu nk. Kifupi hatujui Kiswahili wala kimombo.
Dah. Mwanangu mbona unatupiga na kitu kizito ssana kichwani? 😀
😀 😀 😀
 
Ni story za vijiweni

Watoto wa Tbaijuka au Migiro unafikiri wamependelewa, La hasha

Wamepewa elimu bora
Wewe bado Sana hujui maisha yanavyoendeshwa.
Network, simu ya baba, simu ya Mama inampatia kazi mtu.
Kuna dogo kajitolea miaka 3 kwenye bank. Anaenda kwenye interview za bank hiyohiyo huku barua yake ikiwa imesainiwa na branch manager na kale ka neno "I recommend him" Ila anapigwa chini.

Kuna classmate alivolunteer kwa miaka 3. Siku akaitwa kwenye interview kwenye shirika linalofanya kazi kama zilezile anazofanya kila siku. Wakamuuliza mpaka yakaisha wakaanza Kupigisha story za shirika hili na lenu lipi Bora. Mwisho wakamweka wazi kuwa Ile nafasi Ina mtu.

June mwaka Jana nikienda interview kwenye nafasi ambayo nimeitumikia miaka zaidi ya 4. Mpaka interviewer mmoja ananiambia "Sina Cha kuuliza sababu wewe unajua kila kitu". Na bado nilipigwa chini. Hii nchi iangalie tu.
 
Watanganyika hawa wasiojua tofauti ya R na L wala matumizi ya herufu H are doomed to fail. Lugha yao tu hawawezi ndio iwe yai! Mtu kahitimu chuo kabisa anaandika ela, akuna, apana, ongera, Kalibu nk. Kifupi hatujui Kiswahili wala kimombo.
Haha..!
tumekosa sisi, tumekosa sisi, tumekosa sana..!

tupo hapa tunaiomba 'serekari' yetu 'itulehemu' hivyo hivyo..!
 
🤣🤣🤣🤣Nchi nzito sana na hii
 
Wewe ndiye hujui hata mambo yaliyo wazi. Lugha jifunze ukiwa mdogo. Lugha siyo ya kujifunza ukiwa mkubwa. Halafu unashangaa kwa nini wanaojifunza wakiwa wakubwa hawaongei hata wakijifunza kwa miaka 100. Mbona jibu liko wazi?
Kiukweli mkuu nilikuwa sijui..

Hiki ulichosema ni kwa mujibu wa nini?, kuna utafiti wowote ulifanyika ukabaini hivyo au haya ni maoni yako binafsi tu?
 
Unataka utafiti hata kukwambia kuwa ukipigwa risasi ya kichwa unakufa. Kwamba Dar es Salaam iko Tanzania 🤣. Subiri tafiti sasa.
Kiukweli mkuu nilikuwa sijui..
Hiki ulichosema ni kwa mujibu wa nini?, kuna utafiti wowote ulifanyika ukabaini hivyo au haya ni maoni yako binafsi tu?
 
Kama hata kina Ridhi moko hawajui kiingereza na wamesoma internation school, unashanga nini mtoto wa namnyamba Lindi huko aliyesoma shule ya kata!!!.
 
Unataka utafiti hata kukwambia kuwa ukipigwa risasi ya kichwa unakufa. Kwamba Dar es Salaam iko Tanzania 🤣. Subiri tafiti sasa.
Kwa hiyo suala la kushindwa kujifunza lugha ngeni ukiwa mtu mzima liko wazi sawa na suala la mtu kupigwa risasi ya kichwa na kufa kiasi kwamba halihitaji utafiti?! Unazidi kunishangaza!

Unaposema "lugha jifunze ukiwa mdogo", unamaanisha udogo wa umri gani?
 
ok
 
Sipendi ubishi wa kijinga. Mi siyo mjinga. Umeshinda mkuu. Nakupa kombe🙌 🙌
 
Nasema hivi; to be born british is to win the lottery of life!!!!
Kwa wale wa saint kayumba: kuzaliwa mwingereza ni kushinda bahati nasibu ya maisha!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…