Tuache tabia ya kusimamisha abiria mabasi ya mikoani

Super feo ya Songea Masasi Mtwara ni shida...kuanzia Namtumbo hadi Tunduru full abiria kusimama...abiria wengine wanatoka shambani na mikungu ya ndizi wanaenda kijiji cha mbele nauli ya buku yani hakuna tofauti na daladala kila kjj ni kushusha na kupakia
 
Wanapenda selous na super feo asikuambie mtu, hayo magari mengine siti zinakuwa empty lkn hawapandi,
 
Nipo zangu Tunduru nikakata tiket ya feo masasi to songea,,gari imeingia Tunduru imejaa hatari,

Nikamwambia konda nilikotoka ni mbali sana siwezi kusimama, konda akazama ndani ya bus akamchomoa mnyonge na akamuuliza unashukia wapi? akasema namtumbo,

akamwambia hii siti ni ya huyu dada Simama akae mwenye siti yake[emoji23],akasimama nikakaa zangu,kufika songea gari ikashusha,nikasuubiri feo ya mtwara to mbeya nikadandia hadi shule ya Tanga, nikasubiri feo inayotoka mbeya to mbinga nilipata siti tena ya dirishani mwenyewe alishuka kushangaa[emoji23]alivyorudi ndani ya gari kakuta nimekaa,akasimama hadi mwisho was safari

Kwanza niseme tu super feo/selous nazipenda,najua nikiwepo huku kusini popote nitakapokwenda feo inanifikisha.
 
Umenikumbusha mwaka 2018 nilipanda Buti la Zungu Dar Lindi, kufika mizani ya kule mbele wakatuambia abiria wa kule nyuma watuchukulie bodaboda tukapandie mbele kwa vile eti watapigwa faini kwa ajili ya uzito, halafu wanatuambia kirahisi tu.

Kuna abiria walianza kukubali lakini mimi niliwawashia moto nikasema kwanza hicho kipengele kwenye tiketi hakipo pili mimi abiria sina hasara au faida kama wao wakililipishwa faini kwa ajili ya uzito, hivyo kama wanataka kukwepa hilo watulipe hela au watupunguzie nauli.
Abiria wenzangu wakaniunga mkono, mwisho wakaamua kushuka wao halafu baadhi ya abiria wakasogea mbele
 
Usumbufu wa kijinga sana,

yaani ukiwakazia wanakuwa wapole balaa,kama abiria ni mnyonge utapelekeshwa balaa[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…