Tuache Ufyatu: Ni Kama Bado Tunadeka...

inafikirisha san, na tukipata katba mpya tunaanza kuijaza viraka pia
 
Kama upinzani unaona si imara anzisha chama tukuunge mkono.Hizo akili zenu za kusema hakuna mbadala wa CCM ndiyo umasikini wenu
Huwa tunapigia kura vyama vya upinzani kwa kuwakomoa tu CCM. Ila wanasiasa ni wale wale, tena hao CCM wanaweza kuwa na afadhali
 
Nina imani mlio wengi mnataka katiba mpya ili tu kuweza kukidhi mahitaji yenu ya kisiada lakini ukweli hatuhitaji katiba mpya ili twende vizuri kama nchi bali tuwe tunachagua viongozi walio makini. Na viongozi hao kusema ukweli ha wako nje ya CCM.
 
Kama upinzani unaona si imara anzisha chama tukuunge mkono.Hizo akili zenu za kusema hakuna mbadala wa CCM ndiyo umasikini wenu
Mimi siyo mwanasiasa Mkuu, kila mtu na kazi yake, hawa tunaowategemea wameshindwa kazi, CCM watatawala muda mwingi sababu ya ufake wa hawa wapinzani wetu
 
Jambo kubwa na zuri kuhusu Mama hawajibu, anaacha watendaji wake wafanye kazi, JPM alikuwa anakosea kwenye jambo moja;kuwajibu hawa watu
 
Duh!
P
 
Dr. Kyahoza atupe ulinganisho kati ya Tz na Kenya wenye katiba mpya, hali yao ya kujenga uchumi haiko na utafauti na katiba yao ya zamani.

Kama kuna agenda ya katiba basi watu wadai japo ukumbuke kama hakuna watu madhubuti wa kusimamia mambo yaende katiba mpya sio mwarobaini.

Kenya ni mfano mzuri pamoja na katiba mpya bado kiwango cha rushwa na ma-deal kiko juu.

Ili tujenge uchumi jumuishi ilitakiwa kuwe na tax cuts, gov incentives kwa wawekezaji ikiwemo kutoa financial instruments kwa kuweka uhuria na dhamana ya serikali kwenye kupata mitaji ya uwekezaji.

Sio sawa kuwa na taifa linalo-import basic consumables ambazo tuna uwezo kuzalisha ndani.

Tukiwekeza pia kwenye exports ya final products ya cash crops hilo ni moja ya eneo ambalo tutapiga bao sana tu.

Cha ajabu, sioni mikakati toka wa waziri wa fedha kwenye kujenga uchumi jumuishi; yeye ka-focus kwenye minors kama tozo badala ya kwenye majors namna gani wizara yake iwe chachu fedha zije via FDI uzalishaji utengeneze exports, ambapo exports zitaleta forex.
 
Katiba Mpya itafanya nini na kwanini unafikiri CCM ina maslahi ya kuwa na Katiba Mpya? Wameweza kutawala kwa miaka sitini hivi kwanini leo waamue kuja na Katiba Mpya kabisa?
Katiba mpya wanaona ni kama fagio litakalowaondoa.
Lakini ni bora waongoze huo mchakato.
Kizazi cha ccm kinaendelea kupukutika na hii ni hatari. Dunia inabadilika kwa kasi sana.
Kuendekeza mabavu hakutakuwa na nafasi mbele ya safari.
Hata kama hawaoni katiba ni muhimu ni bora kumbembeleza mtoto kwa kumpa pipi upate kumalizia kazi yako...

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kuwa mzalendo lipa tozo serikali itimize wajibu wake
 
Tatizo siyo katiba mpya, tatizo ni upinzani fake tulionao, leo hii Mdee aliyepiganiwa na kuaminiwa kila kona yupo wapi?
Hilo natia shaka. Nguvu dhidi ya upinzani imepindukia ni kama kuuwa mende kwa nyundo. Dhana ya upinzani si kwa vyama tu hata ndani ya watu.
Fikiria ni watu wangapi hawaridhishwi na yanayojiri, ni wapinzani tayari lakini watajitokeza vipi huku mdomo wa mamba uko wazi.
Kwa hiyo walau kupunguza hofu ni vizuri kuwa na utaratibu mzuri wa utawala yaani katiba.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Slaa ni balozi
Sawa tu, waliona jiwe ni kubwa na gumu kuvunja kwa nyundo na fataki hawawezi kuipata. Siku za kuishi si nyingi sana wakaona bora wapokee mkate ni rahisi kumega na ni mtamu.
Yupo rafiki yangu, ni kada ni mfanya biashara, tenda ni nyingi kwa sababu ni kada tu kimbelembele. Eti sio ccm kindakindaki bali kinafikinafiki
Wanaotoka wanatukana kinafiki kumbe shida ni mkate tu.
Kujenga nchi si kazi lelemama si sawa na kula nchi. Wengi watachagua kula nchi. Ni hao walioacha kuchimba dhahabu wakakimbilia kuokota karanga!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kama kiashiria cha kuchoka kufikiri zaidi na zaidi. Duni itayumba watu wakichoka kufikiri

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
juzi tu ukisema kidogo sukuma gang, mara mataga mara ...

kimya sasa

kurudi kumsema vibaya wanashindwa, so lazima waseme anahujumiwa, ni wasaidizi wake..yeye hawezi eti

mara tozo, mara fuel....mara kodi za nyumba kupitia luku

aliyepigiwa kura na kushinda alikuwa JPM, mama hana kura zake ni zile zile za wasiyempenda

JPM anaishi na ataishi tu, anashinda vita akiwa kalala
 
Kwa kifupi "Mama" anaupiga mwingi!
 
Umekumia muda mwingi kujadili hulka za marais. Wote aliekuwepo na alioko wameshindwa kutekeleza ipasavyo katiba iliyopo hivi sasa.
Hili ni tatizo la kuendelea kujadili na kutatua badala ya kujikita kujadili hulka zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…