Okrap
JF-Expert Member
- Jul 13, 2022
- 1,112
- 2,311
Nimejiuliza sana tena sana, kwanini tunadanganyagwa na wanasiasa tusiowapenda kwa kupewa vijizawadi visivyo na tija maishani?
Wanasiasa hao huja na vijizawadi vya kipuuzi kama vile chumvi ya mawe, kofia, tisheti na sabuni za vipande na kuwapa wapiga kura ili wawachague na wakishapewa kura huhamia Dodoma na Dar kula bata huku wakiwaacha wapiga kura waliowahonga chumvi na sabuni wakibaki maskini milele!
Baada ya miaka 5 hurudi tena jimboni kuhonga vijizawadi hivyo hivyo na wakishapewa kura huhamia tena Dodoma na Dar kula bata.
Kwa nini tumekubali kuwa wajinga miongo na miongo?
Tushikamane wandungu kuukataa huo ujinga.