Tuache Unafiki: Bashe alichukua hatua sahihi kumaliza tatizo la sukari. Hongera Dr. Tulia kwa kumlinda na kulinda maslahi ya nchi

Tuache Unafiki: Bashe alichukua hatua sahihi kumaliza tatizo la sukari. Hongera Dr. Tulia kwa kumlinda na kulinda maslahi ya nchi

Ok, wewe unayeijua sekta hii vizuri tusaidie ufafanuzi wa hoja hii,

Wazalishaji wa sukari walimtaarifu waziri kwa barua juu ya uhaba wa sukari tangu mwezi novemba kutokana na uwepo wa elnino. Wakamkumbusha tena Desemba, akatoa vibali Februali akitaka sukari iwe imeingizwa ndani ya siku 14 jambo ambalo anajua haiwezekani. Hoja,

1.Je kati ya waziri na wazalishaji nani alisababisha uhaba wa sukari?

2. Kwa nini alichelewa kutoa vibali na baadae akavitoa akijua kwa muda huo wazalishaji hawataweza kuingiza sukari na badala yake akatengeneza kampuni zake za mfukoni zisizo na sifa kinyume na Sheria na kuzipa tenda ya kufanya biashara ambayo hawaijui na hawajawahi kuifanya?

3. Kwa nini hata kiwango cha sukari iliyopendekezwa na bodi kuingizwa tani laki 3 waziri alizidisha na kuingiza tani laki 4.1

4. Kwa nini Waziri mwenye vyombo vya dola alishindwa hata kutangaza rasmi na kusimamia bei elekezi hadi sukari hiyo hiyo iliyoagizwa kwa vibali vyake ikauzwa sh 10,000 kwa kg huku akiwa ametoa msamaha wa kodi kwa makampini hayo ya mfukoni hayo? Ni hasara kiasi gani taifa limepata au fedha kiasi gani hayo makampuni ya mfukoni (utakatishaji) wameifisidi serikali?

5. Je wewe unaonaje hali ya usalama kwa taifa kwa mtu asiyejua UBORA wa kitu chenyewe kupewa kazi hiyo hata bila kuthibitishwa na vyombo husika, kampuni za simu, stationary, store, nk zenye usajili tata na mtaji usiozidi 1,000,000. Huu ni utakatishaji wa fedha ulio dhahiri.
Halafu hii sukari ukiondoa zile tani 50 unaweza kukuta iliyobaki yote aliagiza Mo kupitia hivyo vikampuni uchwara na Mo akampa Bashe cha juu
 
Kamati ya bunge bado haijatoa maamuzi kuhusu hivyo Mpina anaviita "vielelezo", na ndio maana ameshitakiwa kwenye kamati ya maadili.

Alichokifanya ni kuwahi kuongea na media ili ku control narrative ya jambo zima, yaani kama ikitokea kuna ushahidi unaopingana na vielelezo vyake basi iwe too late, story tayari iko nje na watu wanamwamini yeye.

It is malicious and unprofessional, na anastahili kupigwa rungu zito maana ni mpotoshaji.
Vipo vielelezo vingine havihitaji kuthibitishwa na hiyo kamati, maana tayari tulikwisha visikia ktk bunge kupitia kamati ya bunge, mfano ni barua za kuagiza sukari zilinukuliwa bungeni, je hapa napo panahiji subiri wakati tayari kamati ilishaweka ktk kumbukumbu za bunge? Vielelezo vingi vya Mpina tayari vipo ktk kumbukumbu ya bunge hata kabla ya kutolewa kwa ushahidi huo.
Halafu hii sukari ukiondoa zile tani 50 unaweza kukuta iliyobaki yote aliagiza Mo kupitia hivyo vikampuni uchwara na Mo akampa Bashe cha juu
Hivi ndiyo picha halisi,
 
Kama Mpina anaweza pewa info zote zile kwa ajili ya ufisadi wa sukari tu, wakati hiko cha mtoto tu kwenye upigaji unaoendelea kwenye kilimo.

Unadhani raisi mwenyewe anapewa mangapi ya mawaziri wake na hayafanyii kazi.

Badala ya kumlaumu Mpina inatakiwa kuangalia picha kubwa kuna watu wamechoka na uwizi unaondelea serikalini ndio maana wamempa info.

Huyo mama atafukuza kila mtu huko Ikulu anaedhani anatoa siri ya mafaili yake asiyotaka kuyasoma.

Halafu Bashe wizara yake mwaka huu budget yake ni tsh 1.3 trillion, sehemu kubwa gharama ni miradi yake ya hovyo and overstated,

Unadhani hiyo hela ya upigaji anayopelekewa huko atakula peke yake, yeye nani:. Sio rahisi hivyo kutolewa hapo kwa budget ya tsh 1..3 trillion wakati hilo ndio chaka lao la wizi kwa sasa.

Either you are with or without them, wengine tubaki kupiga kelele za chura tu; aziwanyimi usingizi wenye nchi.
 
Wakuu kwa sukari bashe mtamuonea tuu...
Ipo hivi mahitaji ya ndani ya sukari ni Tani 420,000...na uwezo wa viwanda vya ndani uzalishaji wake ni tan 280,000 hapa kuna ombwe la tani 140,000 za sukari ambayo itabidi iagizwe nje ili kukidhi mahitaji...

Mwaka jana kukawa na uhaba wa sukari sababu wazalishaji wa ndan au viwanda vya ndani kudai mashamba yalijaa maji...hii ilipelekea uhaba wa sukari hivyo sukari ikaanza panda bei...baadhi ya maeneo ilifika mpaka kilo sh 7,000...waziri bashe akatoa vibali kwa viwanda vya ndani kuagiza sukari nje ili kuzuia mfumuko wa bei ya sukari.,

Sasa wafanya biashara wa ndani kwa njama zao hawakutii agizo kupelekea sukari kupanda zaidi...Bashe alivyo ona agizo halijafanyika akawafutia vibali hivi viwanda vya ndani .,

Maamuzi aliyo chukua ni kuwapa vibali wafanya biashara wenye uwezo wa kuagiza sukari nje ili tu kuzuia mfumuko wa bei ya sukari na hapa ndio tunaona mpaka makampuni ya simu yalipewa tender ya kuagiza sukar nje na bei tuliona zilirudi mahali pake...ingawa ni nje ya utaratibu lakini ilitibu tatizo...

Kama wewe ungekuwa bashe ungefanyaje??? Binafsi nampa maua yake...sijajua tatizo lake na mpina lakini kwenye hili mnyonge mnyongeni haki yake apewe..
Hivi Tanzania hii ukiacha hao wazalishaji ni kweli hatuna makampuni sahihi na yenye vigezo halali kisheria ya kupewa tenda hizo?

Je kuna uwazi wa kiushindani japo wa muda kidogo uliifanyika kupata makampuni hayo?

Kama hayo madogo hayakuzingatiwa kwa nini tusiseme kuwa Waziri naye alitumia fursa hiyo kujinufaisha?
 
Watz tuna akili matope kweli ,,sie shida yetu ni sukari ya kutosha na iwe bei nzuri ,
Mambo ya kampuni haina sifa hio ni hoja za kisiasa hazina mantik ,maana ingekua kampuni hazina uwezo bhc zisingeweza kuagiza
Hoja ya sukari kuagizwa nyingi ety sukar ya ndan tutashindwa kuuza ,huo ni ujinga wa kiwango kikubwa sie wananchi ni wateja sio wauzaji ila mlivo mind kama vile mna hisa kwenye viwanda vya ndani
 
Mimi
Ndugu yangu, kwa mlolongo wa kodi na ukiritimba uliowekwa na serikali, hakuna siku itakuja kutokea sukari ya Tanzania (au bidhaa nyingine yoyote inayozalishwa nchini) kuwa na bei nafuu kuliko inayotoka nje! Never!!
Mimi naona kama hivyo viwanda vya ndani vipo kwa ajili ya kumuumiza mwananchi kwa kigezo Cha kulinda soko la ndani ni bora wavifunge kwa maana havina faida kwa wananchi.
Wavifunge tu watafute kazi nyingine ya kufanywa. Mbona viwanda vingine vinafanya kazi vizuri kama viwanda vya IPP , MO na BAKHRESA ?! Kwanini tatizo liwe kwenye viwanda vya sukari tu?! Kwani hivyo viwanda vingine havilipi Kodi na ushuru?!
 
Tatizo la kuagizwa hiyo sukari nn haswa? Ni kuogopa ushindani? Sisi walaji wa mwisho tunachotaka ni bei nafuu na maisha yetu yawe nafuu.

Mambo ya kulia lia kumuumiza mwananch hatutaki. Kwamba viwanda vilindwe sukari iadimike then tuuziwe tena bei ya juu? Acha sukari iwe nyingi nchini, wiwanda vizalishe, wafanyabiashara waagize,, bei zishuke, na wao watatafuta masoko ya nje wakashindane na wenzao huko!!
Safi sana ndugu
 
Hapo unaweza kuta kule kijijini kwenu Wazazi wako wana maisha magumu sana na vitu kama Chai ni anasa kubwa sana kwao. Wewe uko mjini na usha undergo evolution na sasa unaushi kwa kulamba miguu wanaume wenzako na kujikomva komba kwao
😂😂😂😂😂
 
Mimi

Mimi naona kama hivyo viwanda vya ndani vipo kwa ajili ya kumuumiza mwananchi kwa kigezo Cha kulinda soko la ndani ni bora wavifunge kwa maana havina faida kwa wananchi.
Wavifunge tu watafute kazi nyingine ya kufanywa. Mbona viwanda vingine vinafanya kazi vizuri kama viwanda vya IPP , MO na BAKHRESA ?! Kwanini tatizo liwe kwenye viwanda vya sukari tu?! Kwani hivyo viwanda vingine havilipi Kodi na ushuru?!
Ukiondoa kodi na ushuru mwingine kwenye sukari, kilo moja ya sukari itauzwa chini ya shilingi 1,000. Sasa hapo ndio utajua anaemuumiza mwananchi ni nani.
 
Kama ni mfuatiliaji, utaelewa Mh. MPINA hapingi kuagiza sukari nje. Yeye ana pinga utaratibu na kampuni zilizo pewa vibali. Hivi hata kibanda cha stationary kweli chenye mtaji wa milioni moja kupewa kibali cha bilion mia? Bado tuna support buu ujambazi? Wahindi wana sajili vikampuni vya mfukoni na kupewa vibali? Vibali vina tolewa kwa hongo ya Tsh 300 kwa kila kilo? Nyie hamuoni huruma kwamba hiyo 300 ni wewe una kuja kjilipa? Sasa kuna tofauti gani na hivyo viwanda vinavyo tengeneza uhaba?
Niko na Mpina tuache kutetea ujinga. Ccm ni majambazi.
Kwani huyo mpina ni TADEA au UDP?!
 
Sio tu akili timamu, bali nazijui hizo mishe nje ndani, nilishakuwa mdau kwenye uzalishaji wa sukari zaidi ya miaka 10. Niulize chochote kuhusu Kilombero sugar, Mtibwa sugar au Kagera Sugar.
mlinzi mkuu wa geti la kilombero sugar anaitwa nani?
 
Bashe tapeli yule na sasahivi ameanzisha Movement ya kumpaka Mhe. Rais mafuta kwa mgongo wa chupa. Kile kile alichokifanya kumwibia Lowassa pesa zake na 4U Movement Leo hii anawatumia vijana walewale ameanzisha Movement inaitwa TK Movement wamkoshe mama huku yeye akiumiza Wakulima kwa kuwaibia mabilioni.

Ufuta bei alikuwa 4500 lakini ndani ya wiki tatu umeshuka mpaka 3100 na wanunuzi ni ndugu zake wakinunua kwa maelekezo yake yeye huku cha juu akitambaa nacho..
 
Ukiondoa kodi na ushuru mwingine kwenye sukari, kilo moja ya sukari itauzwa chini ya shilingi 1,000. Sasa hapo ndio utajua anaemuumiza mwananchi ni nani.
Na hayo makampuni yanayoagiza sukari nje ya nchi wanaiingiza nchini bila kulipa Kodi na ushuru ?! Kwanini sukari ya nje iuzwe bei rahisi wakati imesafirishwa toka mbali, na bila shaka waagizaji wasukari wanalipa Kodi na ushuru kama ilivyo kwa waagizaji wa bidhaa nyingine kama Vyombo vya moto na spea zake, halafu sukari inayozalishwa hapa hapa TZ iuzwe bei juu kwa kisingizio Cha Kodi na ushuru?!. Kwanini viwanda vya sukari vy TZ visifanye utafiti katika nchi nyingine zinazozalisha sukari kuona wao wamewezaje kuzalisha sukari kwa bei rahisi?!
 
Kwa hiyo kama makampuni ya kuzalisha sukari yalifanya uhuni wa kuficha sukari naye waziri akaamua kufanya uhuni kutoa vibali vya kuingiza sukari kihuni zaidi na kienyeji?
One wrong does not justify another.
Unatakiwa ujue taratibu za manunuzi serikalini zipo iwe emergence procurement au single source Waziri kaboronga kutoa vibali kwa kampuni zisizokuwa na sifa kwa maslai yake binafsi

Hizi taratibu zinachelewesha maendeleo na haki ya walalahoi sana. Imagine aanze kufuatilia taratibu huku mwananchi anaendelea kuumia kwa miezi kadhaa!!


Sioni shida hata kama angepewa muuza mtumba akaleta hiyo sukari, na lengo la kuuziwa sukari bei ahueni tofauti na za hizo cartels za kipigaji za viwandani!!

As far bei ya sukari itashuka bei wapambana kushindana na products nyingine za huko duniani waache kulia lia tu hapa!!
 
Back
Top Bottom