Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Je hizo timu zilizosajili vizuri na zina makocha wazuri, kwa nini haIjachukua ngao ya hisani?Leo tumeshinda kwa mikwaju ya penati lakini ukweli lazima usemwe, timu yetu haichezi mpira unaovutia, ni ukweli usiopingika kuwa kikosi chetu kina watu wa kazi hasa ambao wana uwezo wa kuleta mataji ya kila aina lakini mfumo anaoutumia Robertinho unaikosesha Simba mabao.
Hivi kweli Simba hii ni ya kucheza mechi 2 bila kufunga goli? Robertinho aaambiwe kama wachezaji hawana uwezo apendekeze, kwanini Kanoute apungue makali wakati tuna Abdallah Hamis?
Timu haichezi mchezo mzuri kabisa, mpira tumeelemewa na Yanga mwanzo mwisho Leo.
Watu wanabisha hata ubingwa wa Argentina kwa World Cup ya 2022, wanasema France ndiyo ilistahili, lakini bingwa ni Argentina. Tuyapuuze haya hayana tija.