Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Unataka kusemaje Pascal Njaa.
 
Karma..Karma....Karma, hivi kuna watu wanasahau kuwa tutakufa wote, na hao wapangaji wana ya kujibu mbele za Mungu. Wale waovu, wauaji na wengine wote wana kesi za kujibu
 
Kweli KARMA ni mwamuzi mzuri..

Ukiua, nawe utauwawa tu..

Sishangai sana kwa haya yanayoendelea...

Sishangai sana Tundu Lissu akiwa na hamu kuona kisasi cha Mungu kikilipwa dhidi ya waliotaka kumuua mwaka 2017...

Bahati mbaya kuwa hawakuytumia muda huu wote kutubu. Walishupaza shingo zao. Sasa kisasi cha Bwana, Mungu Wa majeshi kinatekelezwa....
 
Usihukumu....
P
 
Usihukumu....
P
HAPANA, sijahukumu mtu miye. Nimesema kwa kadiri ya maandiko matakatifu (Neno la Mungu - Biblia) isemavyo..

Hebu soma hapa;

WARUMI 12:19
"...wapenzi, msijilipizie kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imendikwa 'kisasi ni juu yangu Mimi; mimi nitalipa', anena BWANA..."

Unaweza pia kusoma Kumbukumbu la Sheria 32:35; Walawi 19:18; Mathayo5:39 nk nk

Kwa hiyo ndugu yangu Paschal Mayalla, tusifikiri kuwa tunapowatendea watu wengine mabaya kwa sababu na kisingizio chochote hata kama mtu huyo ni mnyonge au dhaifu kisasi gani tukadhani sisi tunaotenda unyama huo tutakuwa salama...

å Waliokosea sana waliompiga marisasi yote yale Tundu Lussu kwa sababu iwayo yoyote...

å Walikosea sana waliomuua kinyama Leopold Lwajabe kwa sababu iwayo yoyote..

å Wanakosea sana watawala wanaotumia nguvu na madaraka yao vibaya kunyanyasa wapinzani wao, wanaowakosoa kwa haki hata isivyo haki, wanaokataa kukubaliana na mawazo au Sera zao...

Watambue kuwa, anayewatetea hawa wote ni Bwana Mungu Muumba wa mbingu na nchi. Mungu anasema hivi: YEYE MWENYEWE NDIYE ALIPAYE KISASI...

Lipo lango la kukimbilia na kuepuka kisasi cha Mungu. Ni TOBA. Ni kukimbilia Golgotha msalabani pa mwokozi Yesu Kristo tukiwa na mafurushi yote ya dhambi zetu na kuzitupa hapo...


Kaka, mimi sijahukumu mtu. Nimesema kwa kuzingatia muktadha wa maandiko matakatifu - Biblia inavyosema...
 
Waliomshambulia Lissu ni watu wasiojulikana.
P
 
Kisasi cha Mungu kupitia aibu ya mauti kitawaweka wazi na kisha kujulikana mmoja baada ya mwingine...

Baadhi walishatangulizwa shimoni. Shina lao ndiyo hilo taratibu linaelekea mavumbini...
Kudhanini jambo baya kulihusisha na mtu bila ushahidi wowote pia ni dhambi!.

Kumsingizia marehemu jambo lolote ni dhambi kubwa zaidi!.

P
 
Kudhanini jambo baya kulihusisha na mtu bila ushahidi wowote pia ni dhambi!.

Kumsingizia marehemu jambo lolote ni dhambi kubwa zaidi!.

P

Hasingiziwi mtu lolote..

Alikuwa ni kiongozi mwenye dhamana kubwa na nchi hii yote...

Maovu yote yalitendeka mbele ya macho yake. Hakuchukua hatua. Alinyamaza kimya...

Huwezi ukamtenga nayo yote huyu. Yalifanyika kwa amri yake, likely...
 
Hasingiziwi mtu lolote..

Alikuwa ni kiongozi mwenye dhamana kubwa na nchi hii yote...

Maovu yote yalitendeka mbele ya macho yake. Hakuchukua hatua. Alinyamaza kimya...

Huwezi ukamtenga nayo yote huyu. Yalifanyika kwa amri yake, likely...
Not necessarily, sio kweli kwasababu si kila hatua zinazochukuliwa lazima zitangazwe. Kuna mengi makubwa mazuri yanafanyika kimya kimya bila kutangazwa.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…