Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Not necessarily, sio kweli kwasababu si kila hatua zinazochukuliwa lazima zitangazwe. Kuna mengi makubwa mazuri yanafanyika kimya kimya bila kutangazwa.

P

Hiyo unajua wewe Paschal Mayalla..

Kuchukua hatua kisiri na kimya kimya kwa jambo ambalo linapasa hatua zichukuliwe kwa uwazi, ni kifungo chao...

Na naweza kusema bila shaka kuwa, usemalo hili ni uongo na ni kutetea uovu... Stop this pls...
 
Hiyo unajua wewe Paschal Mayalla..

Kuchukua hatua kisiri na kimya kimya kwa jambo ambalo linapasa hatua zichukuliwe kwa uwazi, ni kifungo chao...

Na naweza kusema bila shaka kuwa, usemalo hili ni uongo na ni kutetea uovu... Stop this pls...
Jee kila kitu kinachofanyika ni lazima itangazwe.
P
 
Jee kila kitu kinachofanyika ni lazima itangazwe.
P
Si lazima..

Lakini yale yazuayo sintofahamu ktk jamii, ni sharti yashughulikiwe hatua kwa hatua na kwa uwazi ili jamii iwe aware kinachoendelea kuepuka speculations kama hizi za kumshuku na kumlaumu kiongozi mkuu..

Tupende ama tusipende kuukiri ukweli, katika eneo la haki za binadamu Hayati Magufuli ali - fail spectacularly. Acha tumlaumu kabisa kabisa...

Mfano, ishu ya mauaji ya utata kukaliwa kimya bila jamii kujulishwa ilikuwaje, wahusika kina nani, wamechuliwa hatua gani, ni mbaya sana...

Tunachokuja kuelezwa na kuambiwa baadae eti ni "wasiojulikana".. This is too bad and unacceptable..

Paschal Mayalla, hakuna ishu ambayo iliweka doa la mashaka makuu ya "usafi" wa serikali ya Rais Magufuli kama assassination attempt ya Tundu Lissu mwaka 2017 huku Rais mwenyewe akionesha kutojali kana kwamba alifurahia tendo lile ovu kabisa kuwahi kutokea ktk nchi yetu...

Hii ilituthibitishia moja kwa moja kuwa, tendo lile lilikuwa na baraka zake huyu hayati. Iliendelea vilevile na hakuna lolote lililofanywa na serikali yake zaidi ya danadana na visingizio tu visivyo na mashiko...

Since then, binafsi nilitokea kumchukia Rais Magufuli kupita kiasi na kumuona kama Rais mnyama na muuaji kabisa..

I always prayed hard for KARMA to take its course...

Ni jambo la kushukuru Mungu kuwa waliodhani kuwa ni "immortal", hawawezi kufa wanaonja uchungu wa mauti kabla ya wale waliowatakia vifo kabla ya wakati...

Kweli nimeamini " KARMA" siyo mchezo..

Dawa yao ni TOBA tu. Wakili kuwa walitukosea na walitutendea mabaya sana, else watakufa vifo vibaya na vya ghafla mmoja baada ya mwingine...

Hata sisi wanyonge tunaye Mungu. Tunamwomba siku zote atupe HAKI yetu. Tunamwomba atulipie visasi kwa maadui na watesi wetu na anatusikia. Amen..
 
AMEN, ila ku assume fulani anahusika katika jambo baya bila ushahidi, you just keep it in your heart, kumtaja kwa jina na huku ameisha tangulia mbele ya haki, kama hahusiki ni kumsingizia marehemu, karma yake ni mbaya, itakuhusu!. Siku zote tunasisitizwa, tusihukumu tusije tukahukumiwa.

P.
 
Heri sisi tulijiepusha kulipa kisasi. MUNGU WWENYEWE AMEWANYOSHA KUANZIA KULE juu kijazi, magu, Majuva......hii trinity ukikutana nayo ni kifo
 
Mungu amewa-punish sisi tulikuwa hatuwawezi
 
Mie wasiwasi wangu yaliyofuata baada ya lile shambulio hapo hata kipofu alifunguliwa macho
 
Leo Tarehe 7 Septembre, imetimia miaka 4 kamili tangu Tundu Lissu ashambuliwe na watu wasiojulikana ambao mpaka leo ni miaka 4, bado hawatajulikana.

Tumuombee Lissu afya njema na kwenye kuikumbuka siku hii, Mungu amuepushe kupata kitu kinachoitwa "stigimatta"

Pole sana Lissu, survival yako tuu ni muujiza, mwacheni Mungu aitwe Mungu, mengine yote mwachie Mungu.

P.
 
Lakini hakuwa Speaker 2020, so huu uzi ulikuwa ni sawa na Ramli Chonganishi tu.
Mimi ni mpingaji mkuu wa ramli chonganishi.
P
 
Nimeipenda sana hii aya kwani imejaa ukweli wa neno na Mungu.
 
Tunapo sema kwa Ujasiri kuwa alikuwa muovu na kibaraka wa Ibilisi muwe mnaelewa na Wala hatuna ugomvi binafsi bali ni matendo yake ya kifedhuli dhidi ya Binadamu.
Kama yule mzee hayupo motoni basi hakuna Mungu tuendelee kutenda dhambi.
Mkuu Lituye, mwisho wa uwezo wa binadaamu ni kuyasemea yale tuu ya dunia hii, mtu akiishatangulia mbele ya haki, tumzungumze kwa wema, hoja ni atakuwa wapi kama mbinguni, peponi, kuzimu, toharani, motoni au jehanamu kwenye lile ziwa la moto wa milele, hayo sio yetu ni yake YEYE Mwenyewe ndie ajuaye, jukumu letu ni always kuwaombea marehemu wote na sio kuwalaani!.
Kwa jicho la dunia hii, mtu aweza kuonekana ni mwema kama malaika na mwingine akaonekana mbaya kama shetani, halafu siku ya mwisho unaweza kushangaa na usiamini macho yako pale hao uliodhania wema wakitupwa motoni halafu wale waovu wakipeta peponi.

Mfano you will be surprised kuwakuta Osama, Saddam na Gadafi peponi halafu Bush, Blair na Obama motoni!.
Tuwaombee marehemu wote, wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani...amen.
P
 
Duh yaani unatuombea kifo!.
Huku ni kutupigia ramli chonganishi!.
P
 
Subiri Samia afariki 2024.Hapo ndo tutajua kama Mpango atamalizia mwaka mmoja awamu ya Saba then aendelee tena 2025 -2035
Hii ni ramli chonganishi!.
P
 
Kwa maoni yangu, Tundu Lissu anahitaji ushauri nasaha. Binadamu ukipitia maswahibu na mapito kama aliyopitia, unaathirika ki fizikia, ki emosheni na kisaikolojia, (physical, emotional and psychological), hivyo anahitaji ushauri nasaha jinsi ya kutoka kwenye jinamizi hili na kuendelea na maisha.

Huku kutaja taja majina ya watu, na kutangazia ulimwengu kuwa vyombo vyetu tukuka vya ulinzi na usalama kuwa ndio walio husika, shambulio lake, bila ushahidi wowote, ni kuzidi kuibagaza tuu nchi yetu!.

Ametaja Kikosi kazi kinachojumuisha Polisi, JWTZ na TISS,, hawa ni askari wetu, trained, how could they do such a messy dirty job?. Kwa trained snipers, only one single shot would have finished the job!. Hili hata Mama Samia amewahi kuizungumzia, askari wetu trained wakimiss target by two shots, wanaandika maelezo kujieleza!.

Mimi kwa upande wangu naendelea kusisitiza Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Pia Lissu niliisha mshauri na namshauri tena, ajifunze kunyamaza.


Kitendo cha Rais Samia kukubali kukutana na Lissu ni uthibitisho tosha wa kauli na matendo she is healing this nation.

kwenye bandiko hilo nilisema
Ile voice note ya Lissu ni muendelezo wa ramli chonganishi!
P
 
Nimeangalia mahojiano haya ya Tundu Lissu LIVE: Mahojiano na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu katika Clouds 360 kuhusu waliomshambulia ametaja jina la mtu ambaye hayupo na hawezi kujitetea!.

Kwavile kwa sasa huyo mtu hatunaye na hakuna ajuaye sababu ni kwanini alitwaliwa, it might be ni karma or any other reasons lakini sasa hayupo!, be it ni karma or not, sio busara kuendelea kumtuhumu mtu aliyetangulia mbele ya haki, ambaye hawezi kujitetea!.

Ushauri kwa Lissu, asiendelee kutaja hilo jina la huyo mtu, ikitokea hahusiki, Lissu atajichumia karma ya kuchafua majina ya watu bure, halafu karma ikimrudia watu waanze kumtafuta uchawi!.

Badala ya kutaja watu na kuwachafua, Lissu aende kwenye vyombo winavyohusika, akaripoti na kukabidhi evidence yake huko ili uchunguzi wa kijinai uanze.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…