Tuacheni unafiki, Le Mutuz alikuwa ni mtu wa ovyo na mfano mbovu kwa vijana

Tuacheni unafiki, Le Mutuz alikuwa ni mtu wa ovyo na mfano mbovu kwa vijana

Le Mutuz nimeshaishi naye Marekani Aliadhiriwa sana na maisha ya kule usi copy kulazimisha angeishi kibongo.Alikuwa mpambanaji kwa miaka 30 huko majuu,ameshawahi kuwa baharia,dereva wa malori mfanya usafi na kazi za kila aina nchi za ughaibuni.
Alikuwa hatumii kilevi kabisa cha pombe.
Umasikini wako usimuambikize mtoto wa mwenzio.
By the way wewe uliyemsafi hujatenda dhambi kuwa wa kwanza kumrushia jiwe.
Je wewe hujawahi fanya dhambi ya ngono toka uzaliwe?
Ndege ya serikali ilitolewa kwa ajili yake sio kwa ajili ya umaarufu wa baba yake bali ni umaarufu wake mwenyewe kwa jamii ame fight sana kwenye JAMII.
Kila mtu mungu amempangia fujo zake duniani.
Si ajabu ahera utamkuta amekalia kiti cha enzi wewe humo.
Wewe utakuwa unatoka lile dhehebu la dini wanaojiona wao ndio wataiona mbingu.
Alijua afya yake ndio maana alikuwa hatumii pombe.
 
wengi tulimuhukumu kwa kumjua upande mmoja wa kumuona on social media Ila he was very smart R.I.P boma yee nakupa maua yako ukiwa umelala yooo

Soma hapa umjue lemutuz 👇👇👇👇👇👇

Le Mutuz: Historia ya kweli juu ya maisha yangu (My American experience)
 
Kwanza, ninapenda kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, washikaji na wanaJF walioguswa na kifo cha William Malecella. Mungu awape faraja katika kipindi hichi kigumu cha majonzi.

Sasa, twende moja kwa moia kwenye mada, kupitia mada hii, bila kuficha wala kumumunya maneno, William Malecela (Le mutuz) alijulikana na kufahamika zaidi kama mtu wa ovyo kwa sifa hizi (sifa ambazo alikuwa akijivunia nazo hadharani mitandaoni na mitaani);

1. Mpenda sifa popote.
2. Mpenda pombe.
3. Mpenda umalaya.
4. Mpenda maisha ya kujirusha na kuponda raha.
5. Mpenda kujipendekeza kwa watu maarufu (chawa)

Le Mutuz japokuwa alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 50, akijaliwa kuwa na watoto, akipambana kwa namna mbalimbali kutafuta kipato, huku akitokea kwenye familia ya mzee Malecela yenye heshima kubwa sana kisiasa na kijamii ndani na nje ya Tanzania, lakini mienendo na tabia za Le mutuz zilikuwa zenye kutia aibu na kinyaa, akiishi kama kijana aliyepevuka juzi, aliyekosa malezi yoyote ya kijamii na kidini.

Japokuwa hayo yalikuwa ni maisha yake binafsi (sio busara sana kuyahukumu) lakini ni vyema kusema ukweli na kuweka angalizo muhimu kwa vijana ambao ndio wamejaa mtandaoni kuwa makini na kukwepa kuiga au kujifunza kupitia maisha binafsi ya Le mutuz ambayo yalijaa anasa na uchafu mwingi.

UKWELI USEMWE KIKAMILIFU.

Nakubaliani na no 4 mengine umepuyanga tu humfahamu vizuri Marehemu.Mfano no 5 kama ni rahisi na wewe kawe chawa [emoji1787]
 
Alikuwa wa ovyo Kwa vigezo vya nani?
Kwa vigezo vyako binafsi?
Au Kwa imani yako ?


Why tunapenda Ku judge watu Kwa kupitia vigezo vyetu ambavyo sio universal??

Umalaya unaweza thibitisha?au picha za Instagram na warembo ndo uthibitisho?
Pombe?lini ulimuona akinywa? Au picha Akiwa wavuvi ndo ushahidi wako??


Why mnapenda kuishi kinafiki?kujifanya watu wema Kwa nje huku mna madhambi ya kutisha Kwa Siri huku mnahukumu watu Kwa picha za mitandaoni?

Kifupi hamjui vizuri Marehemu.
 
Back
Top Bottom