Tuambiane ukweli kwa Mpira mbovu uliochezwa na Simba SC Kipindi cha Pili dhidi ya Mbeya City ikicheza na Azam na Yanga itafungwa

Na uto watafika wapi? Tuanzie hapo kwanza!
 
Kwanza,Ni lini Lwanga aliwahi kupewa kadi nyekundu iwe kwenye VPL au international tournament?

Pili,wakati unawaza kuwa Simba inaweza kufungwa na Azam kwa uzembe kama wa jana ukumbuke kuwa na wao Azam kama wakiingia kichwa kichwa kama walivyocheza na Namungo hawatapona kwa Simba.

Tatu,Kuchoka kwa Simba kipindi cha pili ni kutokana na aina ya mpinzani aliyekutana nae,mbona hawakuchoka kipindi cha pili walipokutana na Polisi, Kaizer,Yanga, Gwambina,AS vita nk.... mpinzani unayekutana nae ndio atakufanya ucheze vipi.

Nne, kuhusu swala la Kakolanya.Kusajili kipa wa nje eti ili aje kumpa changamoto manula kwanza kimkakati hii sio sawa,kumbuka kwamba NAFASI za kusajili wachezaji wa kigeni ni KUMI tu.Hizi nafasi kumi unapaswa kuzitumia kwenye maeneo ambayo wachezaji wa ndani wameshindwa kuzipambania mfano beki wa kati, kiungo mshambuliaji (hili tatizo lipo hadi national team), mshambuliaji hatari (hapa Tz yupo Bocco tu) ukienda Yanga hata Azam wageni ndio wanaongoza kwa ku score.

Hivyo basi nafasi ya goli kipa kwa simba tayari tumeshapa mchezaji mzawa tena wa daraja la juu kabisaaa,na ikumbukwe kuwa nafasi za kipa huwa ni nafasi ambazo mara nyingi huwa hazifanyiwi rotation,sasa kusajili kipa wa kigeni halafu aje akae benchi huko ni matumizi mabaya ya fedha pia kimbuni unajifunga mwenyewe kwenye zile nafasi kumi za kusajili wachezaji wa kigeni.

Kinachotakiwa kufanywa ni kocha achague mechi ambazo atacheza kakolanya mfano za FA, halafu za kirafiki na mapinduzi acheze Ally Salim na kwenye ligi kuu na Kimataifa acheze Manula.At least hapo atakuwa amewasaidia sana.

[emoji95]Kitu ambacho nakuunga mkono hapo ni swala la wachezaji kujiamini sana mpaka wakapitiliza.Nadhani hapo benchi la ufundi linapaswa kulitazama kwa jicho la pili.

Pia,swala la mipira ya header bado ni Tatizo sana kwenye beki line ya simba,ni Onyango pekee mwenye uwezo wa kuruka vichwa na Kennedy kwa mbali hawa wengine kina Kapombe, zimbwe,Ame,duchu na gadiel bado ni Tatizo sana.
 
Well said broda. Japo tumeshinda, lakin sijafurahia mchezo kabisa. Simba wamebweteka sana
 
Binafsi Jana niliona tunashinda kwa goli zaidi ya 2, yes kipindi cha pili wachezaji Wali relax na kukosa lile pira biriani!

Benchi la ufundi lifanyie kazi mapungufu na mechi zilizobaki naamini ushindi wa above 1 goal upo pale pale.

Go, go our boys, we trust you and we need wins za kutosha!

Sometimes show them mpo weak, Waje kichwa kichwa then give them hell! Pathetic Uto n the like.
 
Naomba nitoe maoni yangu.
Kadri Simba inavyozidi kupata mafanikio ya ndani na nje ya nchi kwa miaka ya karibuni, ndivyo timu inapoangaliwa na kuchambuliwa zaidi na wachambuzi na wapenzi wa kandanda kwa ujumla. Timu inaweza kufanya makosa ambayo timu zingine yanafanya karibu kila mechi, lakini kwa timu kubwa kama Simba makosa yataonekana zaidi. Ndio faida na hasara za kuchezea timu kubwa popote duniani.
Naomba nitoe mfano. Nilikuwa mchezaji mwandamizi katika timu ya kikapu ya Vijana (Vijana City Bulls) kwenye miaka ya mwanzo ya 90. Umakini/ukali/matayarisho/msukumo (intensity,pressure, preparation,focus) ya mnapocheza na timu kubwa, hususani dhidi ya wapinzani wetu wa jadi Pazi ni tofauti sana na unapocheza na timu zingine. Mnaelewa msipocheza katika kiwango cha hali ya juu, mtafungwa. Si kwamba tulikuwa tunazidharau timu nyingine. Hapana. Tulikuwa tunajua uwezo wa timu zote na vipi tucheze ili tupate ushindi. Kwa Timu kama Pazi, ilihitaji utimamu wa asilimia 100%.
Tukirudi kwa Simba, huwezi kufananisha Simba ilivyocheza na Al Ahly, AS Vita, El Mereikh, FC Platinum,nk na itakapocheza na timu tunazoziita ndogo kama Mbeya City. Utimamu wa mchezo utakuwa mkubwa sana kwenye mechi kubwa. Tungependa wacheze sawasawa kama walivyocheza CAF CL, lakini kiuhalisia haiwezekani. Hata tukiangalia timu kubwa duniani kama Barcelona ya miaka ya nyuma. Inaweza kumfunga mpinzani wake wa jadi Real Madrid 5 - 0, lakini akafungwa au akapata ushindi wa tabu dhidi ya Valencia.
Sina nia ya kuwatetea Simba, lakini ndio timu iliyofungwa magoli machache, iliyofunga magoli mengi, na iliyocheza michezo michache. Hii itakupa picha zaidi ya vipi ilivyo imara. Makosa hayatakwepeka na kuna nafasi kubwa ya Simba kujiimarisha.
Nawasilisha.
 

Ukipunguza mihemko na ukasoma vema alicho kiandika mtoa mada na nilichokiandika utaweza elewa na kupata kitu!
 
Je, hapa sasa Umechambua au Umenichamba au Umeleta ujuaji wako wa Kipumbavu na Kishamba?
 
Umegusia la uwanja,uwanja wa majimaji muusikie,wenyewe huko songea wanauita TANGAWIZI,kwa maana ya ile pitch,Sasa sijui Kama Hilo nalo liliwekwa sawa,ukicheza pasi Sana ni shida.
 

Umechambua vizuri sana.
Ila naomba kuuliza, kujiamini kupitiliza ndio kukoje ?
Ni UPI MPAKA WA KUJIAMINI hasa katika mechi ya Simba dhidi ya Mbeya City ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…