Kwanza,Ni lini Lwanga aliwahi kupewa kadi nyekundu iwe kwenye VPL au international tournament?
Pili,wakati unawaza kuwa Simba inaweza kufungwa na Azam kwa uzembe kama wa jana ukumbuke kuwa na wao Azam kama wakiingia kichwa kichwa kama walivyocheza na Namungo hawatapona kwa Simba.
Tatu,Kuchoka kwa Simba kipindi cha pili ni kutokana na aina ya mpinzani aliyekutana nae,mbona hawakuchoka kipindi cha pili walipokutana na Polisi, Kaizer,Yanga, Gwambina,AS vita nk.... mpinzani unayekutana nae ndio atakufanya ucheze vipi.
Nne, kuhusu swala la Kakolanya.Kusajili kipa wa nje eti ili aje kumpa changamoto manula kwanza kimkakati hii sio sawa,kumbuka kwamba NAFASI za kusajili wachezaji wa kigeni ni KUMI tu.Hizi nafasi kumi unapaswa kuzitumia kwenye maeneo ambayo wachezaji wa ndani wameshindwa kuzipambania mfano beki wa kati, kiungo mshambuliaji (hili tatizo lipo hadi national team), mshambuliaji hatari (hapa Tz yupo Bocco tu) ukienda Yanga hata Azam wageni ndio wanaongoza kwa ku score.
Hivyo basi nafasi ya goli kipa kwa simba tayari tumeshapa mchezaji mzawa tena wa daraja la juu kabisaaa,na ikumbukwe kuwa nafasi za kipa huwa ni nafasi ambazo mara nyingi huwa hazifanyiwi rotation,sasa kusajili kipa wa kigeni halafu aje akae benchi huko ni matumizi mabaya ya fedha pia kimbuni unajifunga mwenyewe kwenye zile nafasi kumi za kusajili wachezaji wa kigeni.
Kinachotakiwa kufanywa ni kocha achague mechi ambazo atacheza kakolanya mfano za FA, halafu za kirafiki na mapinduzi acheze Ally Salim na kwenye ligi kuu na Kimataifa acheze Manula.At least hapo atakuwa amewasaidia sana.
[emoji95]Kitu ambacho nakuunga mkono hapo ni swala la wachezaji kujiamini sana mpaka wakapitiliza.Nadhani hapo benchi la ufundi linapaswa kulitazama kwa jicho la pili.
Pia,swala la mipira ya header bado ni Tatizo sana kwenye beki line ya simba,ni Onyango pekee mwenye uwezo wa kuruka vichwa na Kennedy kwa mbali hawa wengine kina Kapombe, zimbwe,Ame,duchu na gadiel bado ni Tatizo sana.