Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,746
- 5,772
Kabla ya kujadili mada husika napenda kuwakumbusha wadau kuwa utawala wa kidikteta huwa unakuwa na sifa kubwa mbili, kwaza hakuna demokrasia hii ni sababu hakuna uchaguzi. Maana wanaotawala huingia madarakani kwa mabavu. Pili ni utawala usiofuata misingi ya katiba na sheria.
Kwa sifa hizo kubwa mbili tunapata jibu kuwa hapa Tanzania hakuna dictatorship.
Nimeamua kuwakumbusha watanzania wenzangu sababu kuna uongo na uzushi ambao watu wanapenda kuueneza ili kuichafua nchi yetu.
Hii nchi inaongozwa kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi,ndio maana hatuoni Rais akiongoza kwa amri zake. Hatuoni akiweka curfew na kuamlisha tulale ndani ikifika saa moja usiku.
Kwa mujibu wa sheria na katiba ya JMT nchi hii ndio tunaona wanaotumiwa kuwa wavunjifu wa sheria za nchi hii wanapelekwa mahakamani ili sheria ifuate mkondo.
Kwa mujibu wa sheria na katiba tunashudia wanaoleta uchochezi na kutaka kuchafua amani ya nchi yetu wakikamatwa na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Hivyo kupakaza maneno ya uongo kuwa watu wanabambikiwa kesi kisa ni wakosoaji wa serikali hakuna mantiki mpaka tupate uthibitisho,maana wengi huwa wanapelekwa mahakamani.
Na kuweka madai kuwa uhuru wa vyombo vya habari umebanwa napo ni kukosea kabisa maana tuna vyombo vya habari vingi tu ambavyo vinatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi hii.
My opinion; Watanzania wamekuwa ni watu ambao hawana msimamo,akitokea kiongozi ambae ni legelege kusimamia sheria wanaponda. Akipatikana msimamizi mzuri wa sheria za nchi kwa manufaa ya umma napo wanaleta figisu.