Nakumbuka wakati niko kidato cha pili katika shule moja ya dini huko kanda ya ziwa, nilikua mimi pamoja na wenzangu tulijiwekea utaratibu wa kubaki shuleni kujisomea mara baada ya muda wa masomo kuisha...siku hiyo ya ijumaa kama ilivyokuwa kawaida wakati natafuta darasa zuri kwaajili ya kujisomea na masela, nikaona darasa moja limefanyiwa usafi vizuuri lakini hawakuzoa takataka/ uchafu walioufagia,,,basi mimi nikachukua chaki nikaenda mbele ya uchafu nikaandika HATUZOI...kumbe mwalimu wa zamu alikua hajapita kukagua usafi asee...alipokuta uchafu na yale maneno alikasirika balaaa ,,,akatuita sisi tuwe mashahidi wake siku ya jumatatu, kwamba kuna wanafunzi wamefanya usafi lakini wamegoma kuzoa takataka..Ilipofika jumatatu wale wanafunzi walipata tabu sana...kipigo chake kilikua ni cha mbwaKoko...,iliniuma sana kwavile hawakuandika yale maneno na wamepata kichapo lakini kwa jinsi mwalimu alivyokua amewaka nisingejisema kuwa mimi ndiye nimeandika...