Tuambie Mechi yako Bora zaidi ya soka ambayo umewahi kuishuhudia

Tuambie Mechi yako Bora zaidi ya soka ambayo umewahi kuishuhudia

M

I nadhani aliyeimaliza hii game ni Di maria....kipindi game iko 1 bila....Atletico walikuwa wanaupiga mwingi sana. Baada ya kusawazishiwa, wakahisi kama wameonewa so wakapanic....extra time wakajikuta wanakula goals nne....Di Maria akiiua game
Goli alifunga Ramos, di Maria alijatahidi nae
 
Yes, ni bonge la mechi. Na hasa utamu wa mechi hii unanogeshwa na ukweli kwamba mimi ni TEAM MESSI lia lia....shabiki ambaye namkubali messi kama GOAT wa soka...niliangalia ile game nikiwa na presha kuanzia dakika ya 1 hadi ya mwisho. Hata pale Argentina alikuwa akiongoza bao mbili bado niliamini haijaisha hadi iishe....Ile save ya Martinez dhidi ya Kolo Muani ni Mungu tu anayejua.
Mpaka sasa hivi, nikiikumbuka ile save ya Martinez, bado najikuta naogopa. Ni sekunde kadhaa tu, mwanaume akaamua hatma ya michuano yote kwa save ya dakika ya mwisho kabisa!
 
International level : Argentina Vs France, 2022 worpd cup final.

Club level: Bayern Munich Vs Atletico Madrid 2016 UEFA nusu fainali ya pili pale Allianz Arena, baada ya mechi ya kwanza kuisha kwa ushindi wa moja bila kwa Atletico. Wakarudiana pale Allianz Arena, Pep Guardiola akaweka pembbeni mpira wa kihispaniola, akawaacha akina Frank Ribery wapige ule msako wa kijerumani.

Upande wa pili, Diego Simeone alienda na mission moja tu, kupaki bus. Hili ndicho kipindi ambacho Atletico Madrid walikua na defense bora zaidi duniani.

Ulipigwa mpira mwingi sana. Ilikua ni pressure kuanzia dakika ya kwanza, hadi ya mwisho. Bayern walishinda 2-1, ila wakatolewa kwa aggregate.


NB: Comeback ya Barcelona Vs PSG, ilikua ni total domination. Barca iliwazidia PSG kila kitu, ndio maana siioni kama ni mechi bora.
Mechi za kupaki Basi sijawahi kuziona kama zina ubora, japo zina msisimko wake kama timu yako ndio inayopalki basi halafu ikashinda, ila ni very frustrating kwa upande mwingine

Mfano UEFA aliyoshinda Chelsea 2012 kwa kupaki basi dhidi ya Barcelona Nusu Fainali na kupaki basi dhidi ya Bayern Fainali, japo nilifurahi Chelsea kushinda mechi zote na kuchukua UEFA kwa mara ya kwanza ila sio mechi bora
 
Man u vs real Madrid nadhan mwaka 2003.. ilikuwa piga nikupige.. united alifungwa 3-1 pale Santiago, mechi ya marudiano.. man kashinda 4-3 barthez akampa kichwa sana Ronaldo de lima Kwa kumpatia goli tatu za kibwege...Beckaham alikuwa na ugomvi na fergie lakn alipoingizwa akawa man wa Match upande wa united kwa kufunga goli mbili tamu..
 
1.Manchester United/Bayern Munich fainali UEFA champions league 1999.
2.Barcelona /Arsenal UEFA champions league final 2006.
👆usiku ule kwenye game ya pili sijui nini kilitokea ndoo ilikuwa ya Gunners kabisa.
 
Screenshot_20230128-153917_1674909679318.jpg
Kuna mechi ya UEFA hatua ya robo fainali Liverpool na Chelsea ya iliiisha magoli 4-4. Mechi ya kwanza Liver alikufa goli 3-1 nyumbani kwake marudiano yakae da kufanyika Starmford Bridge.

JamiiForums1682085511.jpg
Kuna hii mechi ya Madrid na Man City. Hii wengi tuliona namna mpira ulivyo na ukatili.

Mechi ya mwisho ni kama ya mleta mada fainali ya WC hii ya mwaka jana 2022 kiukweli hakuna ambaye hakuburudika ilijawa msisimko mkubwa. Kijana Mbappe hongera kwa burudani ile.
 
Real Madrid 4 vs atletico Madrid 1 -hii ilikuwa fainali ambapo atletico aliongoza Hadi dk ya 94.

Madrid wakapata kona, aisee Sergio Ramos ni zaidi ya fundi, cr7 akaimaliza mechi.
Hii mechi pepe aligombana na Simeone, maana atletico walihisi game imeisha
Atletico alikosa kwa simanzi sana ni kama ile final ya man u vs bayern munich mwaka 1999 kama uliiangalia., kufor alilia kama mtoto mdogo siku iyo
 
M

I nadhani aliyeimaliza hii game ni Di maria....kipindi game iko 1 bila....Atletico walikuwa wanaupiga mwingi sana. Baada ya kusawazishiwa, wakahisi kama wameonewa so wakapanic....extra time wakajikuta wanakula goals nne....Di Maria akiiua game
Alafu extra aliingia marcelo upande mmoja di maria upande mwingine marcelo atletico aliita maji mma ila ni kweli walionewa lile goli la ramos la kusawazisha lilikua offside
 
Mpaka sasa hivi, nikiikumbuka ile save ya Martinez, bado najikuta naogopa. Ni sekunde kadhaa tu, mwanaume akaamua hatma ya michuano yote kwa save ya dakika ya mwisho kabisa!
Hatari sana. Wakati kolo Muani anapiga ile shuti nilifumba macho sikutaka kuona hilo goli. Ni goli ambalo lingeniumiza sana sana. Ile save ni Mpango wa Mungu tu.
 
View attachment 2498362Kuna mechi ya UEFA hatua ya robo fainali Liverpool na Chelsea ya iliiisha magoli 4-4. Mechi ya kwanza Liver alikufa goli 3-1 nyumbani kwake marudiano yakae da kufanyika Starmford Bridge.

View attachment 2498360Kuna hii mechi ya Madrid na Man City. Hii wengi tuliona namna mpira ulivyo na ukatili.

Mechi ya mwisho ni kama ya mleta mada fainali ya WC hii ya mwaka jana 2022 kiukweli hakuna ambaye hakuburudika ilijawa msisimko mkubwa. Kijana Mbappe hongera kwa burudani ile.
Chelsea walianza lambwa mbili kwanza kipindi cha kwanza, nilikaa na kaka yangu shabiki wa Chelsea alinuna balaa yaani. Nikawa nacheka kama mwehu ndiyo kwanza nikamtia hasira, walivyosawazisha alishangilia kama hamnazo. Isingekuwa sub ya lampard ingeisha 4-2
 
Kuna hiyo ya Simba na Stella Abidjan mwaka 1993. Ilikuwa fainali ya ambayo sasa inajulikana kama CAF Confederation Championship. Ndio mechi ilifanya niwe shabiki wa Simba mpaka leo.
 
Back
Top Bottom