Tuambie Mechi yako Bora zaidi ya soka ambayo umewahi kuishuhudia

Tuambie Mechi yako Bora zaidi ya soka ambayo umewahi kuishuhudia

17 Nov 2015
Algeria 7 – 0 Tanzania

Y. Brahimi 1'
F. Ghoulam 23', 59' (P)
R. Mahrez 43'
I. Slimani 49' (P), 75'
C. Medjani 72'
 
Mechi zipo nyingi saaana.

Nashindwa kupanga kwa kuzingatia ugumu wa mechi ila acha nizitaje.

Chelsea v PSG
Ibrahimovic anapewa red card mapema, game ilikuwa ngumu, ngumu kwelikweli. Chelsea kila akifunga, PSG anachomoa, dakika za mwishoni Thiago Silva anachomoa goli na matokeo droo ya 2-2 Chelsea anaaga UEFA.

Inter Milan 3 Barcelona 1
Inter ya Mourinho na Barca ya Pep, Mourinho akajiona bado mbabe, yeye ndo muarobaini wa Barca, akahamia Madrid kabisa.

Manchester United v AC Milan
Kaka anawagonganisha vichwa mabeki bora kabisa wa Man U kipindi hiko, Ferdinand na Nemanja Vidic.

Manchester United 1 v Liverpool 4
Hataari saana hii game, Fernando Torres na Steven Gerald waliacha msiba mzito Old Trafford.

Game zipo nyingi sana mkuu.
 
iyo game ya united stev Gerrad anapiga chuma anakimbilia kushangilia kwenye kibendera anabusu camera iyo game ilpigwa old trafford united kipindi hicho tunavaa jezi za AIG

Game ya Inter milan hiyo San Siro wesley Snejider yupo kwenye ubora wake afu kuna muhuni mmoja alikua anacheza kati pale Chivu na Thiago motta kulia kuna Maicon Beki ya Kati kuna Javier martinez na Lucio kitambo sana mzee bila kumsahau Diego milto
 
Mancity vs QPR 2012...Mancity anachkua ubingwa baada ya miaka kadhaa magoli yakiwekwa kimyani Na Aguero Huku upande wa pili man u dhidi ya sunderland ameshinda anamsikilizia Mancity apigwe Au atoe sare man u anyangue kwapa.
Dakika ya 85 channel ya canal sport wanaikata screen katikati kuonyesha game zote mbili ile ya man u vs sunderland upande wa pili Mancity vs Qpr.....dakika ya 90 goli linasawazishwa Na dk 93 Aguero anamaliza biashara Mancity ananyanyua ndoo kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa, mashabiki Uwanja Mzima wanashindwa kujizuia wanavamia Uwanja kwa furaha....Aisee ile game
 
Nimekuwa shabiki wa soka kwa muda mrefu sana. Kwa muda wa miaka 20 sasa. Nimeangalia mechi nyingi sana na za kutosha, zaidi ya 1000 hadi leo hii.

Toka enzi za goli la dhahabu hadi leo hii ambapo goli la ugenini limefutwa kwenye mashindano ya Ulaya na technolojia ya VAR inatumika.

Nimeangalia fainali 6 za kombe la dunia, toka 2002 hadi 2022. Nimeangalia zaidi ya fainali 14 za Uefa Champions league. Nimeangalia mechi nyingi sana za mashindano tofauti tofauti na zenye matukio ya kusisimua na matokeo ya kustaajabisha....Jaribu kuwaza,,

Nani amesahau kuhusu usiku wa Liverpool dhidi ya Ac Milan 2005?..Je ile comeback ya Barcelona dhidi ya PSG 2017?...vipi kuhusu usiku wa Drogba pale Allianz Arena 2012?....Bila shaka wote tunakumbuka goli la Iniesta lilivyowapa ubingwa Spain mbele ya Uholanzi pale Soccer city kwa madiba....Na vipi kuhusu ile Acrobatic ya Wayne Rooney dhidi ya Man city dakika za kuelekea mwisho kabisa kwenye mechi muhimu ya kuamua bingwa wa EPL 2010/2011...Mungu amlaze pema Cheikh Tiote anayetukumbusha Comeback ya Newcastle dhidi ya Arsenal game ambayo Newcastle wanatoka nyuma kwa bao 4 na kufanya matokeo kuwa 4 kwa 4...vip kuhusu Madrid dhidi ya City UCL mwaka jana?

Hakika kuna mechi nyingi sana ambazo tumezishuhudia na kuzifurahia. Na ambazo zilituacha na kumbukumbu nzuri sana mioyoni mwetu. Lakini pamoja na hayo, kuna mechi moja ambayo kwangu mimi nimeiweka katika kilele cha ubora. Ndiyo, ni Mechi Bora zaidi ya soka ambayo nimewahi kuishuhudia. Unataka kuifahamu?

Usipate tabu, rudisha kumbukumbu zako hadi Jioni ya Tarehe 18.12.2022 pale Qatar...ARGENTINA vs FRANCE....Dakika 120 za dhahabu. Ni mechi kubwa iliyoamuliwa na wachezaji wakubwa katika hatua kubwa ya mshindano makubwa zaidi ya soka duniani.

Kwangu mimi Argentina Vs France ndio mechi yangu bora zaidi ya soka niliyowahi kuishuhudia toka nimeanza kuangalia soka....

Tuambie kwa upande wako, ipi mechi bora kwako!!!
Bayern Munich vs Manchester United-UEFA Champion League 1999.
Unforgettable.

Beckham na Oleguna wa Moto kabisa
 
World Cup final 2022

Hii game niliangalia uku natetemeka sana moyo unanienda mbio sitaki ata kukumbuka [emoji28][emoji28] ilivyo fika matuta nilipiga magoti nikasimama nikakaa yan nilifanya kila kitu ... moja ya moment mbaya sana kuishuhudia katika soka ni kuona Andunje akinyanyua world Cup ...ili ni moja ya tukio baya sana kuwahi kuliona katika mpira
 
iyo game ya united stev Gerrad anapiga chuma anakimbilia kushangilia kwenye kibendera anabusu camera iyo game ilpigwa old trafford united kipindi hicho tunavaa jezi za AIG

Game ya Inter milan hiyo San Siro wesley Snejider yupo kwenye ubora wake afu kuna muhuni mmoja alikua anacheza kati pale Chivu na Thiago motta kulia kuna Maicon Beki ya Kati kuna Javier martinez na Lucio kitambo sana mzee bila kumsahau Diego milto
Ile ya Man U kufa goli 4 mpaka Gerald anaenda kubusu Camera ilikuwa ni moto.
 
Sikumbuki ilikuwa Euro mwaka gani Russia chini ya mzee Guus Hiddink mbele wana Andry Arshavin na Roman Pavlyushenko walimpigia mpira flani wa jihadi Uholanzi, ile game niliipenda namna Uholanzi alivokufa kwa lazima.
 
Liverpool 4 VS Chelsea 4. UEFA Champion league 2008. Pia Chelsea 4 Vs Barcelona 2 mwaka 2005 bila kusahau November 5, 2023 pale ambapo Yanga 5 vs 5imba 1
 
Usilku wa ulaya Mei 21, 2008 pale Luzhniki stadium, Moscow

Fainali UCL
Man utd v Chelsea

Dk 26 Cr7 anaiandikia utd bao la kuongoza
Dk 45 Lampard anasawazisha
Ngoma inaisha 1-1
Game inaenda matuta
CR7 anakosa penalty, matumaini kwa united kubeba ndoo yanakwisha,
Mpira na maajabu yake,
Penalty kuipa ushindi chelsea, Terry anateleza anakosa
Shujaa Edwin Van der Sar anapangua mkwaju wa anelka, ndoo inaenda united
 
Burkina Faso 4 DR CONGO 4 .... Mpaka dakika ya 86 Congo keshapigwa 4-1 .... Nani ya dakika tatu akapiga goli 3 ngoma ikasimama 4-4 ...Congo wakashinda kwenye penalty....1998 ....
 
National team fainali yangu bora ni ARGENTINA na france.

France tuliwafanya mbaya na hawatosahau, wamecheza na timu bora na mchezaji bora kuwahi kutokea.
Uliangalia fainali ya euro 1996 ya Ujermani vs Czechoslovakia!?? ....
 
Back
Top Bottom