Barakoa
JF-Expert Member
- Apr 11, 2020
- 741
- 1,352
Na hivi kwa nini huyo mtu amekuwa akiulizwa sana juu ya jinsia yake ?
kuna Mkuu mmoja atapita hapa mda sio mrefu..anajiita cocastic ila mimi najua kwanini anajiita hivyo..najua hatatoboa hiyo siri ila ngoja niwaibie siri yake.
siku moja miaka mingi kidogo imepita mimi nayeye tukiwa wanafunzi kutoka shule mbili tofauti mkoani Dsm tulikutana sehemu kwa mdahalo maalumu wa wanafunzi. Wakati namalizia mchango wangu kwenye ule mdahalo, nilimalizia kwa maneno haya 'thank you so much organizers for the fantastic debate'.... Sasa ilipofika zamu ya huyu mkuu nae ikabidi apige chabo kidogo akasema 'I feel so lucky to participate in this cocastic debate'...Ukumbi mzima ulivunjika mbavu.
Basi ameona ndio iwe ID yake hiyo..